BlackPanther
JF-Expert Member
- Nov 25, 2015
- 9,554
- 9,243
Bado nasisitiza kuwa haya mambo si ya kushangaza barani ulaya hasa kwa mtu mwenye utimamu wa akili.....
Maelfu ya wakimbizi kutoka mashariki ya kati ambako msamiati wa amani na ubinaadamu umeshapotea vichwani mwao....huku wakionekana kukata tamaa na maisha kwani hawana cha kupoteza mwao....mambo kama haya yalitarajiwa.......
Huwezi kuwapokea wakimbizi ambao wanajua mateso yao na mahangaiko yao yamesababishwa na wewe alafu wewe ukabaki salama.......
Yaani ni sawa na mfano wa mtu ambaye umemgombanisha na ndugu zake kiasi cha kuondosha amani miongoni mwao alafu mtu huyo unampa hifadhi kwenye familia yako yenye amani.....hapo unadhani nini kitatokea....!!???
Dunia haipaswi kupumbazwa na haya yanayotokea sasa hivi balani ulaya kupitia CNN na BBC bali pia wanapaswa kuwafikiria mayatima na walemavu waliobakia huko mashariki ya kati yaliyosababishwa na makombora ya NATO na Marekani nyuma ya kichaka cha UGAIDI NA DEMOKRASIA........
Bahati mbya propaganda zimetawala kwenye vyombo vya habari vya magharibi kiasi ulimwengu mzima kumuonea huruma mzungu aliyechomwa kisu....kuliko mtoto au mwanamke asiyekua na hatia aliyesambaratishwa na makombora ya NATO......na Marekani.......
Kikulacho..post zako huwa zinavutia sana, ulichokisema ni ukweli halisi big up