GE2025 Muliro awaonya wanaotaka kuandamana oktoba 29

GE2025 Muliro awaonya wanaotaka kuandamana oktoba 29

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Baadaye ikawaje
Mlilo ndiyo alichochea mandamano kwa kutembeza mikwara hata vurugu zote chanzo ni yeye kwa kuwatuma Polisiccm wake kuwapiga risasi kuwaua waandamanaji wapita njia na watu waliokuwa majumbani mwao
 
Waandamanaji waliandamana kwenda kwake Mbezi kimara wakazuiwa na Asikari kwa kutupiwa Risasi nyingi wakatawanyika, kinyume na hapo nyumba yake ingechomwa moto, sasa wapo wanamngojea Asitaafu akiwa nyumbani mda wote wamdai ndugu zao aliowaua
Jinga kabisa na mimacho yake, ataenda kujibu mahakamani kwa mauaji hayo.
 
Mlilo afikishwe mahakamani ICC The Hague kwa mauaji ya kimbali
 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amewaonya wale wote wanaopanga, kuratibu ama kutaka kushiriki kwenye uvunjifu wa amani ikiwemo kufanya vurugu na maandamano Oktoba 29, 2025, akisema Jeshi hilo limekula kiapo kulinda nchi pamoja na raia na mali zao.

Soma pia: Kamanda Muliro kuelekea Oktoba 29, tumejipanga kwa kila tishio la kiusalama

View attachment 3493221

Kamanda Muliro ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 24, 2025 wakati wa kongamano la Vyuo na Vyuo Vikuu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Kongamano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza na kuwashirikisha wanafunzi wa shule za Sekondari, Vyuo na Vyuo Vikuu, akiwataka Vijana pia kuwa waangalifu na kutafakari kuhusu misukumo na mihemko yao kulingana na aina na makundi ama watu wanaoambatana nao.

"Tukiwa kama watu tuliokula kiapo tunawaleza kuwa tutatimiza jukumu letu la kuhakikisha kuwa watu wanakuwa salama, watu wajitokeze kwa wingi kupiga kura, wafuate sheria na sisi tutakuwepo barabara kuwalinda wote wanaoenda kutimiza jukumu lao la Kikatiba la kwenda kupigakura. Siku hiyo kutakuwa hakuna maandamano wala hakuna vurugu, siku hiyo ni ya upigaji wa kura bila hofu."Amesema.
A twit at his best
 
Back
Top Bottom