Muleba: Afungwa Jela miaka 3 kwa kupokea Rushwa ya Tsh. 250,000

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Hukumu hiyo imetolewa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Muleba, Kagera dhidi ya Mashaka Magesa Ngereja baada ya kumkuta na hatia ya kupokea Hongo kwa lengo la kuuza Ardhi ya Kijiji cha Kahangaza kitongoji cha Kanyamlima.

Mshtakiwa alikutwa na kosa hilo ambalo ni kinyume na Kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa Sura ya 329 Mapitio ya 2022 baada Mahakama kujiridhisha kwa kusikiliza ushahidi wa pande zote.

Mshtakiwa alitakiwa kulipa faini ya Tsh. 500,000 au kwenda Jela miaka 3 ambapo alikosa Fedha hiyo. Pia, ametakiwa kurejesha Tsh. 250,000 alizopokea pamoja na Ardhi iliyouzwa irejeshwe katika Serikali ya Kijiji.
 
Jamani watu wa Muleba Mungu asaidie akili zifunguke, kweli mtu unaweza kukubali kifungo cha miaka mitatu kisa umekosa laki tano, kwa mtu aliyejitambua hii ni fedha ya kutafuta ndani ya mwezi mmoja tu hata kama watu mtajiita masikini ila huu sio umasikini wa kifedha bali ni umasikini wa kiakili aiseee. Muleba rise, once again rise tutoke huku kwenye kufungwa akili tuache kuchezea Muda, dakika moja ni kubwa kule mapinduzi duniani ndugu zangu.NAWAPENDA WOTE,NAIPENDA MULEBA KAGERA NAIPENDA TANZANIA.
 
Mpaka alifikia hatua ya kuuza ardhi ya kijiji/umma zaidi sana sema ya Wanamuleba inaonekana hiyo zone ina raia fulani vilaza kwanza hawakipendi kijiji chao na hawapendani wao kwa wao hasa upande wa ndugu.

Haiyumkiniki inakuwaje ndugu wasichangishane hata kuweka bond asset ya mfungwa mtarajiwa ili zipatikane hizo 500K asiende ngome ili aje apambane mtaani akiwa huru kulipa hayo madeni.
 
Hukumu hiyo imetolewa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Muleba, Kagera dhidi ya Mashaka Magesa Ngereja baada ya kumkuta na hatia ya kupokea Hongo kwa lengo la kuuza Ardhi ya Kijiji cha Kahangaza kitongoji cha Kanyamlima.
Na wale wengine
 
Jamani watu wa Muleba Mungu asaidie akili zifunguke, kweli mtu unaweza kukubali kifungo cha miaka mitatu kisa umekosa laki tano, kwa mtu aliyejitambua hii ni fedha ya kutafuta ndani ya mwezi mmoja tu hata kama watu mtajiita masikini ila huu sio umasikini wa kifedha bali ni umasikini wa kiakili aiseee. Muleba rise, once again rise tutoke huku kwenye kufungwa akili tuache kuchezea Muda, dakika moja ni kubwa kule mapinduzi duniani ndugu zangu.NAWAPENDA WOTE,NAIPENDA MULEBA KAGERA NAIPENDA TANZANIA.
Unaishi dunia ya wapi ?

Unaongelea Laki Tano wakati kuna watu wanakufa kwa kukosa elfu 20 ya dawa ? Usiangalie dunia kwa macho yako au kidogo kwako ukadhani ni kidogo kwa wote...; Tena huenda mwingine anaona bora aende huko atapata chakula kwa ajira ya kufanya kazi nzito huenda angebaki mtaani wangemmaliza na wanaomdai viwanja alivyouza vikarudishwa wangempatia haki yake....

Penda kuangalia the whole equation kwa kujaribu kuvaa viatu vya muhusika kwa wakati huo (utaona kwamba most things people do there is a reason behind)
 
Elfu ishirini kubwa sana,kuna jamaa mwaka 2017 alilazwa hospital pale kahama pamoja na mzee wangu,huyu jamaa alikuwa kapata ajali na hali take haikuwa mbaya sana ,na ili wamtibu wahudumu wa afya waliomba walipie sh 15,000 ya X-Ray ,familia na ukoo mzima walikosa na mgonjwa akapoteza uhai!!

Hatari sana, watu wenyeshibe wanakauli za kushangaza sana
 
Naam...,

Shibe inabidi iishie wenye tumbo, ukiwa na shibe mpaka kwenye macho ni upofu ambao unakufanya ushindwe kuona vitu kwa uhalisia wake....
 
Mahama za nchi hii zilivyo za hovyoo...

Waliouza Bandari wamepewa shng ngapi..

Pumbavu.
 
Elfu ishirini kubwa sana,kuna jamaa mwaka 2017 alilazwa hospital pale kahama pamoja na mzee wangu,huyu jamaa alikuwa kapata ajali na hali take haikuwa mbaya sana ,na ili wamtibu wahudumu wa afya waliomba walipie sh 15,000 ya X-Ray ,familia na ukoo mzima walikosa na mgonjwa akapoteza uhai!!

Hatari sana, watu wenyeshibe wanakauli za kushangaza sana
Mkuu nahisi ume exaggerate hapo kwenye "15,000" kushindwa kupatikana kwenye ukoo mzima.
 
Mpaka alifikia hatua ya kuuza ardhi ya kijiji/umma zaidi sana sema ya Wanamuleba inaonekana hiyo zone ina raia fulani vilaza kwanza hawakipendi kijiji chao na hawapendani wao kwa wao hasa upande wa ndugu.

Haiyumkiniki inakuwaje ndugu wasichangishane hata kuweka bond asset ya mfungwa mtarajiwa ili zipatikane hizo 500K asiende ngome ili aje apambane mtaani akiwa huru kulipa hayo madeni.
Huyo jamaa ni Msukuma kwa hiyo kahamia Muleba siyo mwenyeji.
 
Back
Top Bottom