MULA matapel wapya hawa! *150*78#

MULA matapel wapya hawa! *150*78#

ntamaholo

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
12,950
Reaction score
6,981
Wana bodi,

Siku moja nikiwa naendelea na mishe zangu, nilipigiwa simu na watoa huduma ya mula *150*78# kuwa naweza nujua bundle la king'amuzi kupitia kwao kwa njia rahisi zaidi. Niliwajibu poa ntajaribu njia yenu hiyo mwezi ukiisha.

Juzi nimenunua kifurushi cha startimes ili kuwahi muda uliotolewa kabla ya gharama mpya kuanza kutumika. Nasubiri kuona kama kimekubali au la.

Wakati nasubiri kuona kama manunuzi ya startimes yekubali, nikaamua kununua vocha(muda wa maongezi) kupitia mula kwa vocha ya halotel.

Nilimaliza manunuzi lkn masaa 24 yamekatika vocha yangu sijaiona. Nimeaapigia simu wakasema wanashughulikia, lakini sasa siku nzima imeisha. Asubuhi nawapigia hawapokei simu.

Nawatahadharisha ndugu zangu, tuendelee kununu kupitia njia za zamani. Hawa MULA wanaweza kuwa wamekuja kutuibia kama deci tu.

Sms za manunuzi hizi hapa.

5E5619GI8 Imethibitishwa. Tsh1,000.00 imetumwa kwa CELLULANT MULA kwenye akaunti namba 1882968 tarehe 5/5/18 saa 1:08 PM. salio lako la M-Pesa ni Tsh137,550.76.

Na waketa nyingine hapa:-

Mpendwa mteja, umefanikiwa kununua muda wa maongezi kupitia Mula, pia unaweza kununua LUKU kwa urahisi zaidi. Piga *150*78#. Kwa msaada piga 0755400006
 
Mm niwaombe tu ndugu zanguni, tuwe tunajipa muda kufuatilia umakini, ufanisi na ubora wa huduma zinazotangazwa na makampuni mapyq kqbla ya kuanza kuzitumia.

Jina tu Mula...! Mm nikajua ni gaidi fulani hivi toka Afghanistan.
Ulijua Mula Muhammad wa Afghanistan kwenye Milima ya Toh-rabola
 
Kikubwa ni kuepuka mteremko wa Tanzania tunapenda mteremko sana bila kuchunguza athari zake Serkali yetu ipo kwenye Siasa masuala ya msingi kama haya hawayaoni wanaichi wanaibiwa mchana kweupe hakuna msaada
 
Mm niwaombe tu ndugu zanguni, tuwe tunajipa muda kufuatilia umakini, ufanisi na ubora wa huduma zinazotangazwa na makampuni mapyq kqbla ya kuanza kuzitumia.

Jina tu Mula...! Mm nikajua ni gaidi fulani hivi toka Afghanistan.
Duh, haya buana.
 
Kikubwa ni kuepuka mteremko wa Tanzania tunapenda mteremko sana bila kuchunguza athari zake Serkali yetu ipo kwenye Siasa masuala ya msingi kama haya hawayaoni wanaichi wanaibiwa mchana kweupe hakuna msaada
Basi ni tahadhari kwa wengine au mula waje na solutions za malalamiko ya wateja. 24hrs bado buku yangu sijapata, nimewachukia kwelikweli
 
Hao kina Mula hatari sana,,,sasa embu ngoja nikupe option nzuri kwa salio lililobak
 
Hapana si wezi hata kidogo. Na wangekuwa wezi hata hiyo risiti wasingekupa kuthibitisha kuwa umewalipa kiasi hicho cha fedha.
1. Mimi nimewahi kununua umeme mara mbili kupitia huduma hii. Mara ya kwanza walichelewa sana mpaka nikaamini kuwa nimeibiwa lakini baadaye walinitumia tochen yangu. Mara ya pili walikuwa fasta sana.

2. Nilichowapendea hawa jamaa (nisiowafahamu) ni kwamba ukishatumia manue yao mara moja kumbukumbu zako zinabaki mfano huitaji tena kunakili namba ya luku yako ama kingamuzi chako. Ukianza tu malipo unakuta tayari namba zako zipo kwenye list unachagua tuu.

3. Niachokiona kwa hawa jamaa, bada hawajawa vizuri kimfumo kuweza kuendana na kasi ndio maana matatizo kama hayo ya kuhisi kuibiwa yanatokea pale huduma inapochelewa ama kwa bahati mbaya mtandao ukashindwa kuchanganuavizuri.

4. Kwangu naona kama wakiweza kutatua hizo changamoto watakuwa ni moja kati ya watoa huduma wa kidigitali bora kuliko wote. Tanzania. Yawezekana wameleta changamoto mpya kwenye soko na wanakupamba na vita ya kibiashara na watangulizi wao
 
hahaaa MULA "" nilidhani ni MURA ila nikahisi ulikosea spelling"" kumbe MULA nijina La kampuni ""?? makubwa ..jina lenyew mbona limekaa kitapeli tapeli
 
Kikubwa ni kuepuka mteremko wa Tanzania tunapenda mteremko sana bila kuchunguza athari zake Serkali yetu ipo kwenye Siasa masuala ya msingi kama haya hawayaoni wanaichi wanaibiwa mchana kweupe hakuna msaada
Mkuu unaweza kuelezea kidogo kwa wasiojua kama mimi, ni kwanini mnunuzi atumia middle man kama huyu? Hakuna uwezekena wa kununua moja kwa moja? Kuna faida gani ya kuwatumia bila kununua moja kwa moja?
 
Hapana si wezi hata kidogo. Na wangekuwa wezi hata hiyo risiti wasingekupa kuthibitisha kuwa umewalipa kiasi hicho cha fedha.
1. Mimi nimewahi kununua umeme mara mbili kupitia huduma hii. Mara ya kwanza walichelewa sana mpaka nikaamini kuwa nimeibiwa lakini baadaye walinitumia tochen yangu. Mara ya pili walikuwa fasta sana.

2. Nilichowapendea hawa jamaa (nisiowafahamu) ni kwamba ukishatumia manue yao mara moja kumbukumbu zako zinabaki mfano huitaji tena kunakili namba ya luku yako ama kingamuzi chako. Ukianza tu malipo unakuta tayari namba zako zipo kwenye list unachagua tuu.

3. Niachokiona kwa hawa jamaa, bada hawajawa vizuri kimfumo kuweza kuendana na kasi ndio maana matatizo kama hayo ya kuhisi kuibiwa yanatokea pale huduma inapochelewa ama kwa bahati mbaya mtandao ukashindwa kuchanganuavizuri.

4. Kwangu naona kama wakiweza kutatua hizo changamoto watakuwa ni moja kati ya watoa huduma wa kidigitali bora kuliko wote. Tanzania. Yawezekana wameleta changamoto mpya kwenye soko na wanakupamba na vita ya kibiashara na watangulizi wao
Nakusupport mkuu. Mi pia huwa nawatumia coz siwezi kila mara kukumbuka namba ya Dstv na Startimes except ya LUKU hii naijua vizuri.
Hawa jamaa kweli wanachangamoto kama hizo ila huduma yao iko poa.
Walishawahi kuchelewa kuniunganisha na Dstv nkawapigia wakanirudishia pesa na wakaniunganisha na kifurushi pia kwa hiyo nikawa nimepata kifurushi bure na pesa yangu mfukoni.
Hawana longo longo sana.

Haya mambo mengine ni ya kimtandao tu. Na kila sehemu yapo.
 
Mkuu unaweza kuelezea kidogo kwa wasiojua kama mimi, ni kwanini mnunuzi atumia middle man kama huyu? Hakuna uwezekena wa kununua moja kwa moja? Kuna faida gani ya kuwatumia bila kununua moja kwa moja?
Hawa jamaa nafikiri wanapata commission kutoka kwenye makampuni yanayouza mija kwa moja coz vifurushi gharama ni zile zile kama watoa huduma wengine hawaongezi hata senti moja wa kupunguza.

Faida ya kutumia Mula kufanya payment ni pale tu unapoingiza namba ya kadi ya king'amuzi au mita ya luku au vinginevyo hutunza kumbukumbu you don't need to have your card au namba ili upate huduma, so huduma utaipata popote coz namba wanaitunza. We ni kubofya tu *150*78#
 
Back
Top Bottom