Yuko wapi Mujuni Kataraia?

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
Naomba kuuliza yeyote ambaye ana habari za Mujuni Kataraia. Alshawahi kuwa mbunge wa jimbo fulani mkoa wa Kagera.
 
Kuna wakati alikuwa mkuu wa wilaya nilisikia ila sina uhakika lakini sasa......................
 
Naomba kuuliza yeyote ambaye ana habari za Mujuni Kataraia. Alshawahi kuwa mbunge wa jimbo fulani mkoa wa Kagera.

Huyo Mzee alishapata kuwa Mwanasiasa maarufu na haswa Ukada wake wa CCM,kama walivyo viongozi wengine alikumbwa na siasa za makundi zilizoundwa katika Uchaguzi mchafu wa mwaka 2005.Licha ya kuwa Mbunge kipindi cha 1995/2000 na kuwa mmoja kati ya Wajumbe wenye ushawishi mkubwa kwenye Kamati ya Bunge ya Mahesabu ya mashirika ya Umma (Kipindi cha kuuzwa kwa mashirika mengi ya Umma).Mwaka 2000 alishindwa kurudi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Mwaka 2001 alijaribu kugombea nafasi 9 za Ubunge wa East African lakini pia alitupwa Nje nafasi ambazo ziligombewa na watanzania karibu 70.Katika Vipindi tofauti kati ya 2001 - 2007 aliteuliwa na Mwenyekiti wa CCM kuwa Katibu wa Chama hicho katika Mikoa ya Mwanza na Singida.
Katika vikao vya CC/NEC vilivyofanyika April/2008 kule Mwitongo - Butiama pamoja na ajenda ya mambo ya Mafisadi kulikuwa na ajenda iliyomuhusu Mzee Kataraia na Mzee Maregesi ambapo wajumbe wengi akiwamo Mzee Msuya na Makongoro Nyerere walipendekeza watu hao(Kataraia na Maregeresi) wafukuzwe CCM kutokana ubadhirifu wao wa pesa za Chama kutokana na vyeo vyao.Mzee Kataraia alikuwa Katibu wa chama Mkoani Singida na Mzee Abiud Maregeresi alikuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi.

Katika kipindi alichokuwa Mwanza kama Katibu wa CCM,Kataraia alishutumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha za chama,kutoka katika michango ya hiari na malipo ya vibanda vya Uwanja wa Kirumba.alishawahi kutupiwa shutuma za ununuzi wa magari binafsi (Landcruisers) kutoka katika fedha za chama.Shutuma hizo ndio zilizomfanya akavuliwa wadhifa wake wa Ukatibu wa CCM.
Inasemekana Mzee Katarai anaishi Marekani na Vijana wake.
 
Alikuwa Marekani kwa mapumziko na naona karudi ili atimize haki yake kikatiba ya kupiga kura. Sina shaka atampa kura yake Dr wa ukweli Dr Slaa, maana hakuwa na mausihano mazuri na kikwete tokana na siasa za kimtandao. Yeye alikuwa upande wa Sumaye na alisimamia hilo hadi mwisho wa maisha yake ndani ya sisi m.
Jamani hiyo ndio sisi m kama hamuijui subiri yakikufika na wewe utaibwaga.
 
Actually habari za ndani zinaonyesha huyu jamaa alitakiwa kutemwa katika vile visasi vya jk. Akiwa Singida kesi za mambo ya ubadhirifu Mwz yakajitokeza. Ubadhirifu huu unaonekana ulikuwa wa kutafutiliza maana kipindi hicho hela ya EPA ilikuwa nje nje ikitawanywa bila accoutability yoyote kwa njia sizokuwa rasmi. Any way yeye sasa na kina Sumaye, Mangula et al wanayatazama mambo kwa mbali. Siasaaaaah !!!!
 
Alionekana week ya juzi mitaa ya Westheimer/Hayes-Houston,Texas;kama karudi TZ basi ni week ya jana!Hivi sasa ni mkimywa sana na hapendi kuongea ongea hasa kuhusu mambo ya siasa,hata vijana walipomchokoza aseme lolote kuhusu mustakabali wa CCM haku respond!

Kada mashuhuri mwingine ambaye ni victim wa siasa za makundi kwenye CCM mpya ya JK!
 
IMG-20231010-WA0098.jpg


Huyu hapa mwamba, anaishi huko kwa Biden.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom