Muigizaji Richard Norton afariki dunia

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,195
Reaction score
10,709
Richard Norton, mwigizaji, staa katika filamu ya Mad Max, amefariki akiwa na umri wa miaka 75, mkewe Judy Green ametoa taarifa kwenye Instagram.

"Nimevunjika moyo, sina maneno nimepoteza kila kitu changu," aliandika kwenye maelezo, pamoja na picha. "Najua kuna, na kutakuwa na upendo na mshtuko mwingi kwamba tumempoteza mwanadamu huyu wa ajabu. Upendo ❀️ wa maisha yangu. Ninatumia wakati huu kukubaliana na msiba wangu mkubwa."


Mwaka 1980 ulitupatia ubora wa filamu ukiwa na Chuck Norris kwenye filamu ya The Octagon, dunia haitasahau kazi zako bora ulizofanya na Jackie Chan, Sammo Hung, Yasuaki Kurata, Benny Urquidez, Don Wilson pamoja na Cynthia Rothrock.

PUMZIKA KWA AMANI RICHARD NORTON πŸ•―
 
Huyu mwamba namfahamu toka kitambo sana. Katika uhai wake alikuwa ni muigizaji mzuri na mwenye bidii ya kile anachoigiza.

Mungu ampe pumziko jema huko alipo.
 
Huyu jamaa namkubali sana, enzi hizo wakati nikiwa kama director wa movies zake hakuwahi kurudia kushoot mara mbili, yani yeye n mara moja tuu tayari tumemaliza scene yake πŸ”₯
 
Huyu jamaa namkubali sana, enzi hizo wakati nikiwa kama director wa movies zake hakuwahi kurudia kushoot mara mbili, yani yeye n mara moja tuu tayari tumemaliza scene yake πŸ”₯
Mwezi mtukufu umeisha naona umerudia kula mmea
 
RIP Mwamba u died empty ur talent remain in our mind forever.
 
R I
R I P
 
Tulikuwa wadogo, tukaaminishwa Cynthia Rothrock ndio mkewe.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…