Muige panya katika harakati za utafutaji, utatoboa

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
1,195
1,661
panya.JPG

Nadhani wote tunamjua mnyama panya, sasa bwana panya anajua kabisa akisema amkimbie binadamu kwa kuogopa kifo na kuhamia porini, atakufa njaa. Tena kabla ya njaa huenda akauliwa na wanyama wakali zaidi.

Anachofanya panya ni kusoma ratiba ya binadamu ndani ya nyumba, saa ngapi anaenda kazini anafunga mlango, saa ngapi analala anazima taa. Jiko liko usawa upi akajipimie misosi na stoo au dari ni wapi akaandae bed room yake na familia.

Pia anawafunza wanae kutambua chakula kilichodondoka ndio chao, wakiona kisafi, kimenona, juu ya gazeti, huo mtego, wasile! Kwa mtindo huo,panya hunenepa na kuzaliana kizazi hadi kizazi.

Sasa wewe, bosi kakufokea ushawaza kukimbia kazi, mteja kakujibu jeuri, sijui kakopa hajalipa, unataka kufunga biashara. Utakufa NJAA wewee!
 
Nadhani wote tunamjua mnyama panya, sasa bwana panya anajua kabisa akisema amkimbie binadamu kwa kuogopa kifo na kuhamia porini, atakufa njaa. Tena kabla ya njaa huenda akauliwa na wanyama wakali zaidi.

Anachofanya panya ni kusoma ratiba ya binadamu ndani ya nyumba, saa ngapi anaenda kazini anafunga mlango, saa ngapi analala anazima taa. Jiko liko usawa upi akajipimie misosi na stoo au dari ni wapi akaandae bed room yake na familia.

Pia anawafunza wanae kutambua chakula kilichodondoka ndio chao, wakiona kisafi, kimenona, juu ya gazeti, huo mtego, wasile! Kwa mtindo panya hunenepa na kuzaliana kizazi hadi kizazi.

Sasa wewe, bosi kakufokea ushawaza kukimbia kazi, mteja kakujibu jeuri, sijui kakopa hajalipa, unataka kufunga biashara. Utakufa wewee!
Toa na ufafanuzi mkuu juu ya mfano wa panya kama ulivyoelezea hapo juu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom