Kuna watu na viatu kwa kweli. Ninaanza kuamini baadhi ya maprofesa ni makanjanja! Huyu ni profesa wa nn hasa? Mimi nategemea angetueleza anafanya nini tupate umeme wa uhakika! Anafanya nini watanzania wawezeshwe ili wachangie nchi yao kupata maendeleo na zaidi waweze hata kujenga vyanzo vya nishati! Hawa ndo wale wanaoamini hatabwatoto wao hawawezi kusoma na kuandika! Sishangai kwa baadhi ya maprofesa kama huyu kuwasha gari toka UDSM kwenda Ubungo kusaga mahindi debe moja kwa kuogopa tu kuwa kijana wa kazi akienda na baiskeli atakwiba! Badala ya kukaa na kutafiti tufanye hivi ama vile tutapiga hatua! Afanye tafiti gani ili tukwamuke hapa au pale yeye kesharidhika kuwa mimi Profesa bwana! Ama anakiri na anaamini kuwa Mengi anamiliki eneo kubwa hivyo aoni kuwa atakuwa na uwezo angalao naye wa kuwekeza kwenye gesi! Kwani Reginald atawekeza wapi zaidi ya hapa kwake. Believe me non of those you call foreign investors ambaye ana mapenzi mema na hii nchi. Wote wanachuma tu na watatimka baada ya kushiba.
Niwape mfano, kuna mlalahoi mmoja naye anajiita mzungu, akaja hapa baada ya kuona fursa zilizopo akakimbilia kuoa binti wa kitanzania, akamtumia kusajili kampuni na baada ya muda akapata na uraia! Wengi wetu tulijiuliza hii kampuni ina wageni wengi lakini fedha hatuzioni. So hata watu wa TRA walikuwa hawaoni kama kampuni ina generate income. Uchunguzi nilioufanya nikagundua kuwa yeye hulipwa kupitia account yake huko uingereza na yeye hudraw kiwango kinachotosheleza wageni wake na mishahara nyingine hubakia huko huko kwao. Tulipokuja kumconfront alikimbia na sasa karudi kwao. Nilichotaka kusema tu ni kuwa Muhongo anajaribu kuwakumbatia hao anaoamini kuwa wana fedha na kudharau eti sisi watanzania hatuna hela! Kama hana hela aseme yeye hana hela na siomkila mtu hana hela. Huo ni upofu wa fikra! Changamoto ka hizi ndugu zangu Watanzania tusikubali kuamini kuwa sisi ni maskini bali viongozi wetu ndio wenye fikra za kimaskini. Wenye kuamini kuwa kila kitu cha mzungu na mzungu! Wafike mahali sasa wajuenkuwa Watanzania wameamka na wanaweza!