Narudia tena Hii ni kazi yao, uwepo wa polisi inamaanisha kunatakiwa kuwe rate ndogo Sana ya crime.sio kupunguza crime rate Kama unavyosema.Unamsifia mama kunyonyesha kichanga chake ?1) Wamefanikiwa kupunguza uhalifu kwa kiwango kikubwa sana hapa tanzania. Ukilinganisha miaka ya nyuma na sasa utakubaliana na mm kwamba uhalifu umepungua. Na kama unabisha kwenye hili basi jaribu kuwa mhalifu na utajua kitakachokupata
Angalia standard procedure ya kudeal na waandamaji Kwa mujibu wa utaalamu. halafu uje u comment tena. Risasi za moto zina wakati wake wa kutumika. Ni last option.Yani watu wanao laumu asikali nitofauti kabisa hawajui kua hawakua na makusudi kwaza walikua wanalinda laia na ikawa bahatimbaya leo watu wanalaumu jeshi wakati walisababisha waokuandamana jeshi kweli wamekubali lakini nibahatimbaya
mtoa mada anajielewa kweli, hivi anajua thamani ya uhai, binti huyu mdogo angekuwa dada yake angesema police wakikosea kidogo, dah ama kweli mabumunda wapoMimi kama mimi Nimekusamehe.....
Polisi yakiri kupiga mtu risasi maandamano ya CHADEMA
View attachment 697076
Hahari za wakati huu ndugu kaka na dada zangu hapa jukwaani.
Mimi kama kawaida yangu huwa siwezagi kuandika maneno meeeengi sana zaidi ya kwenda straight to the point.
Kuna habari nimezisikia zikisambaa na pia kuthibitishwa na kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam ndugu Lazaro Mambosasa juu ya tukio la kuuwawa kwa bahati mbaya kwa mtu mmoja huko Kinondoni.
Kwanza napenda kumpongeza kamanda Mambosasa kwa kitendo tu cha kukubali ya kuwa risasi iliyotoa uhai wa mtu yule ilifyatuliwa kutoka katika silaha zinazomilikiwa na jeshi lake.
Huu ni ukomavu wa kitaalum sana kwa kamanda. Ninasema ni ukomavu kwa maana ya kwamba, Polisi still walikuwa na uwezo wa kukana kuhusika na tukio hilo, wakaunda tume ya kufanya uchinguzi kisha wakaleta majibu tofauti na ambacho kamanda amethubutu kikiri mbele ya umma wa watanzania.
Pili, napenda kuwaambia watanzania wenzangu ya kuwa, si ndani ya jeshi la polisi tu, hapana, bali ajali ni risk ambayo ipo katika kila kazi na kila taaluma.
Ni kweli inauma sana hususan kwa ndugu na jamaa waliopotelewa na mpendwa wao na ninawapa pole sana (my sincere condolences)
Nimeamua kuandika hivi baada ya kuona jinsi watu wanavyorusha matusi na lugha chafu kwa jeshi kana kwamba wao huwa hawafanyi makosa katika kazi zao.
Tunapokuwa tunalaumu pia tukumbuke ya kwamba ni polisi hawa hawa wa Tanzania na wala si wa kutoka nchi jirani kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ndio waliotokomeza wale wahalifu wa kule Kibiti waliokuwa wakiua watu kikatili.
Ni polisi hawa hawa ndio wanaopambana na mitandao ya uhalifu kama panya road na magenge mengine ya wahuni.
Ni polisi hawa hawa ndio wanaofanya patrol usiku kucha, wakati wa mvua na baridi kali, huku sisi tukiwa tumelala fofofo, tukiwa hatufahamu ni kipi kinaendelea nje ya mitaa yetu.
Ni polisi hawa hawa ndio wanaopambana na majambazi wanaovamia banks kwa lengo la kupora fedha zetu ili kukwamisha shughuli za maendeleo.
Hivyo mimi ninachoona ni kwamba, pale tunapokuwa tunalaumu ajali zinazotokea katika taaluma za watu (kama polisi) basi tusisahau pia na kazi njema wanazofanya to keep us safe and secure.
Ushauri wangu ni kwamba hii coverup this time around ifanywe na Waziri Nchemba kama political figure ndani ya wizara. Sio tena mkuu wa wilaya.
Wakaongee na familia ya marehemu kama wataridhia basi jeshi lichangie gharama za mazishi ama libebe gharama zote, if and only if, the family of the deceased will give go ahead and consent without any fraction of reluctance.
Nothing is easier than blaming others as if you're perfect katika kazi zako. Kilichotokea kwa polisi ni ajali kazini. Full stop.
Ninajua kuna baadhi watanitukana na kunikejeli na kusema najipendekeza kwa police ila huo ndio ukweli.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Haya ni mawazo yangu and I stand to be corrected.
"KIJANA IPENDE NCHI YAKO, TOA MAONI NA USHAURI BADALA YA KUTUKANA"
Poleni sana wafiwa.
Naomba kuwasilisha.
Good evening.
View attachment 697527
View attachment 697881
Follow me;
===========
Military Intelligence Coup: Kisa cha rubani aliyeiba na kutoroka na Ndege ya Kijeshi ya Iraq
==========
K.G.B Espionage na Ujasusi kwa njia ya ngono kama silaha ya vita. Honey trap/Honeypot....Part One (1)
==========
Serikali na TRA, mnaweza kuwezesha utoaji wa risiti za VAT kwa njia ya mobile SMS. I stand to be corrected
==========
Ushauri kwa Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya, Wizara ya michezo, TFF pamoja na BMT
==========
Wahandisi wa kampuni za simu, kwanini tusikwangue vocha kisha tukaingiza kwenye mobile money accounts zetu?
==========
Acha upuuzi ww kuua sio kosa dogo
Wanafikii tuuu...!!Serikali imeguswa sana na tukio hili ndio maana wakaamua kugharimia shughuli zote za mazishi. Thanks to the ministries and government at large kwa kuguswa kwenu.
Ndugu wa marehemu Poleni sana. Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.