Muhimu Sana: Polisi wakikosea kidogo, isitufanye tukasahau mazuri na mema yote wanayoyatenda

Ayo mazuri ni yako ww unaelishwa na kununuliwa magari na vidume ili wale na kufaid iyo mali ya bure uliyobeba.
 
Ni bahati mbaya bunduki au risasi iliyopigwa juu ilikata kona na kulenga daladala, kuna uwezekana mkubwa kuwa bunduki au risasi kimoja wapo kilikuwa kime-expire, ndio tabia za AK.
 
Nimeamua kuandika hivi baada ya kuona jinsi watu wanavyorusha matusi na lugha chafu kwa jeshi kana kwamba wao huwa hawafanyi makosa katika kazi zao.
Wanatukanwa kwa kuwa ni watu wasiojitambua ktk kazi zao. Wao hawatumii akili bali nguvu tu.

Tunapokuwa tunalaumu pia tukumbuke ya kwamba ni polisi hawa hawa wa Tanzania na wala si wa kutoka nchi jirani kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ndio waliotokomeza wale wahalifu wa kule Kibiti waliokuwa wakiua watu kikatili.
Kibiti? Hapana kabisa, nipeni majibu ya suala hili
http://mtanzania.co.tz/watoto-1300-waliopotea-kibiti-wana-zaidi-ya-mwaka/
kwa hili jeshi lilifeli sana.

Ni polisi hawa hawa ndio wanaopambana na mitandao ya uhalifu kama panya road na magenge mengine ya wahuni.
Mitandao ya uarifu? Bado sana.

Ni polisi hawa hawa ndio wanaofanya patrol usiku kucha, wakati wa mvua na baridi kali, huku sisi tukiwa tumelala fofofo, tukiwa hatufahamu ni kipi kinaendelea nje ya mitaa yetu.

Na ni hao hao wataalamu wa kubambikizia watu kesi za udhuluraji, wakati kuna watu huwa wanatoka may be kwenye matamasha n.k

pale tunapokuwa tunalaumu ajali zinazotokea katika taaluma za watu (kama polisi) basi tusisahau pia na kazi njema wanazofanya to keep us safe and secure.
Nothing is easier than blaming others as if you're perfect katika kazi zako. Kilichotokea kwa polisi ni ajali kazini.

Si ajali kazini, Bali uzembe na ni makusudi kama haya hapa:

Mtuhumiwa wa Mauaji ya Mwangosi Akutwa na Kesi ya Kujibu - Global Publishers
Zombe na Wenzake Washinda Kesi, Christopher Bageni Kunyongwa - Global Publishers
 
Wangekuw wamemuua wakipambana na majambazi ingeeleweka sasa walikuwa wanapambana na adui yupi si wote ni ndugu.
Gpo inasema piga risasi juu kwanini usifanye hivyo
 
Sasa hapa umeandika nini? Acha uoga dogo, polisi tunawalipa kw kodi zetu ni wajibu wao kutulinda na sio msaada et tukae kuwashukuru, pumbavu sanaa... Mistake zingine zote zinavumilika ila sio mistake za kuondoa roho za watu.
Mwambie amlete mama au baba na hata mwanae tumnyonge na kamba kwa bahati mbaya, kushika bunduki ni hatua, kushika trigger ni hatua na kuibonyeza trigger ni hatua na kulenga ulipokusudia ni hatua. Hatua zote hizo zinahitaji mtu mwenye weledi na kazi yake na mwenye mwenye maamuzi yenye fikra(rationale). Sasa huyo form four failures waliosoma shule za kata zenye watoto wengi kama mimi.
 
Nakuunga mkono Mkuu,kwamba ni ajali kazini.

Ingekuwa na utata zaidi angepigwa risasi muandamanaji tena kiongozi wa siasa,lakini mpita njia!!!

Kwavile hatutambui mchango/mema ya polisi,labda wafanye zoezi la kusitisha huduma/kuchukua likizo nchi nzima kwa wiki moja tu alafu tupime kama wana umuhimu au la!
 
Nazijua hasa kuua watu wasio na hatia waliyo kwenye daladala!
Mkuu kwanza naomba nikuulize swali dogo tu hivi unazijua ethics za kipolisi? Kwamba ni muda gani watumie silaha za moto muda gani watumie blanc na muda gani watumie mabomu ya machozi/ maji ya kuwasha? Nijibu kwanza hapa kisha tuendelee.
 
Nakuunga mkono Mkuu,kwamba ni ajali kazini.

Ingekuwa na utata zaidi angepigwa risasi muandamanaji tena kiongozi wa siasa,lakini mpita njia!!!

Kwavile hatutambui mchango/mema ya polisi,labda wafanye zoezi la kusitisha huduma/kuchukua likizo nchi nzima kwa wiki moja tu alafu tupime kama wana umuhimu au la!
Mie silindwi na Polisi nalindwa na malaika wa Mungu na Mungu wenyewe!
 
Watu wanasubiri kuona viongozi wenye dhamana ya usalama wa raia na mali zao wakijiuzuru mara moja bila kusita!
 
Polis ya Tanzania imejaa siasa Ni wauaji

Fikiria kundi lile ambalo linashikaaga namba z darasan ndio linakabidhiwa silaha kulinda watu
 
Polisi yakiri kupiga mtu risasi maandamano ya CHADEMA

View attachment 697076

Hahari za wakati huu ndugu kaka na dada zangu hapa jukwaani.

Mimi kama kawaida yangu huwa siwezagi kuandika maneno meeeengi sana zaidi ya kwenda straight to the point.

Kuna habari nimezisikia zikisambaa na pia kuthibitishwa na kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam ndugu Lazaro Mambosasa juu ya tukio la kuuwawa kwa bahati mbaya kwa mtu mmoja huko Kinondoni.

Kwanza napenda kumpongeza kamanda Mambosasa kwa kitendo tu cha kukubali ya kuwa risasi iliyotoa uhai wa mtu yule ilifyatuliwa kutoka katika silaha zinazomilikiwa na jeshi lake.

Huu ni ukomavu wa kitaalum sana kwa kamanda. Ninasema ni ukomavu kwa maana ya kwamba, Polisi still walikuwa na uwezo wa kukana kuhusika na tukio hilo, wakaunda tume ya kufanya uchinguzi kisha wakaleta majibu tofauti na ambacho kamanda amethubutu kikiri mbele ya umma wa watanzania.

Pili, napenda kuwaambia watanzania wenzangu ya kuwa, si ndani ya jeshi la polisi tu, hapana, bali ajali ni risk ambayo ipo katika kila kazi na kila taaluma.

Ni kweli inauma sana hususan kwa ndugu na jamaa waliopotelewa na mpendwa wao na ninawapa pole sana (my sincere condolences)

Nimeamua kuandika hivi baada ya kuona jinsi watu wanavyorusha matusi na lugha chafu kwa jeshi kana kwamba wao huwa hawafanyi makosa katika kazi zao.

Tunapokuwa tunalaumu pia tukumbuke ya kwamba ni polisi hawa hawa wa Tanzania na wala si wa kutoka nchi jirani kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ndio waliotokomeza wale wahalifu wa kule Kibiti waliokuwa wakiua watu kikatili.

Ni polisi hawa hawa ndio wanaopambana na mitandao ya uhalifu kama panya road na magenge mengine ya wahuni.

Ni polisi hawa hawa ndio wanaofanya patrol usiku kucha, wakati wa mvua na baridi kali, huku sisi tukiwa tumelala fofofo, tukiwa hatufahamu ni kipi kinaendelea nje ya mitaa yetu.

Ni polisi hawa hawa ndio wanaopambana na majambazi wanaovamia banks kwa lengo la kupora fedha zetu ili kukwamisha shughuli za maendeleo.

Hivyo mimi ninachoona ni kwamba, pale tunapokuwa tunalaumu ajali zinazotokea katika taaluma za watu (kama polisi) basi tusisahau pia na kazi njema wanazofanya to keep us safe and secure.

Ushauri wangu ni kwamba hii coverup this time around ifanywe na Waziri Nchemba kama political figure ndani ya wizara. Sio tena mkuu wa wilaya.

Wakaongee na familia ya marehemu kama wataridhia basi jeshi lichangie gharama za mazishi ama libebe gharama zote, if and only if, the family of the deceased will give go ahead and consent without any fraction of reluctance.

Nothing is easier than blaming others as if you're perfect katika kazi zako. Kilichotokea kwa polisi ni ajali kazini. Full stop.

Ninajua kuna baadhi watanitukana na kunikejeli na kusema najipendekeza kwa police ila huo ndio ukweli.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Haya ni mawazo yangu and I stand to be corrected.

"KIJANA IPENDE NCHI YAKO, TOA MAONI NA USHAURI BADALA YA KUTUKANA"

Poleni sana wafiwa.

Naomba kuwasilisha.

Good evening.

View attachment 697527

View attachment 697881

Follow me;
===========
Military Intelligence Coup: Kisa cha rubani aliyeiba na kutoroka na Ndege ya Kijeshi ya Iraq
==========
K.G.B Espionage na Ujasusi kwa njia ya ngono kama silaha ya vita. Honey trap/Honeypot....Part One (1)
==========
Serikali na TRA, mnaweza kuwezesha utoaji wa risiti za VAT kwa njia ya mobile SMS. I stand to be corrected
==========
Ushauri kwa Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya, Wizara ya michezo, TFF pamoja na BMT
==========
Wahandisi wa kampuni za simu, kwanini tusikwangue vocha kisha tukaingiza kwenye mobile money accounts zetu?
==========
Rubbish
 
Tanzania hatuna polisi....tuna vibaka tu wauwaji na wachumia matumbo yao....huwezi kuwaita watu wanaofyatua risasi ovyo ovyo polisi! Unawapa cheo wasichostahili....ninapokutana na hawa vibaka barabarani hasira inanipanda ghafla..sina uwezo lakini ningekuwa nao.....ohooo
 
Tanzania hatuna polisi....tuna vibaka tu wauwaji na wachumia matumbo yao....huwezi kuwaita watu wanaofyatua risasi ovyo ovyo polisi! Unawapa cheo wasichostahili....ninapokutana na hawa vibaka barabarani hasira inanipanda ghafla..sina uwezo lakini ningekuwa nao.....ohooo
tusio na bunduki tupigane kwa maneno tu no way out
 
Jeshi la polisi wakisimamisha kazi zao (covert & overt) kwa muda wa dakika 45 tu hii nchi haitakalika.....!!!! Think Twice.....!!!!!
 
Back
Top Bottom