Muhimu Sana: Polisi wakikosea kidogo, isitufanye tukasahau mazuri na mema yote wanayoyatenda

Mi natamani nikutusi.
Unalenga watu wasio na hata mshale, na kuwafyatulia risasi then unasema bahati mbaya? What are you, an imbecile? Nkt!
 
Kama ni mm ndie niliefiwa na huyo mchicha mliepiga risasi nisingetaka hata sent tano yenu yaani mmeua kwa makusudi halafu mnaleta dharau ya kutuandikia maneno ya kifedhuri humu eti polisi wanfanya kazi kubwa ya kulinda majambazi
Et hamlali kwa kuhakikisha usalama unakuepo na kutolea mfano wa majambazi ya kibiti hiyo ni kazi yenu mlioichagua na mnalipwa na kodi zetu yaani tunawalioa kwa kodi zetu halafu sisi tunaowalioa ndio mnatuua si dharau hizo mm binafsi naona hizo zote mlioandika hapo ni pointe less ni upuuzi mtupu
 
Yani watu wanao laumu asikali nitofauti kabisa hawajui kua hawakua na makusudi kwaza walikua wanalinda laia na ikawa bahatimbaya leo watu wanalaumu jeshi wakati walisababisha waokuandamana jeshi kweli wamekubali lakini nibahatimbaya
 
1) Wamefanikiwa kupunguza uhalifu kwa kiwango kikubwa sana hapa tanzania. Ukilinganisha miaka ya nyuma na sasa utakubaliana na mm kwamba uhalifu umepungua. Na kama unabisha kwenye hili basi jaribu kuwa mhalifu na utajua kitakachokupata
Narudia tena Hii ni kazi yao, uwepo wa polisi inamaanisha kunatakiwa kuwe rate ndogo Sana ya crime.sio kupunguza crime rate Kama unavyosema.Unamsifia mama kunyonyesha kichanga chake ?
 
Yani watu wanao laumu asikali nitofauti kabisa hawajui kua hawakua na makusudi kwaza walikua wanalinda laia na ikawa bahatimbaya leo watu wanalaumu jeshi wakati walisababisha waokuandamana jeshi kweli wamekubali lakini nibahatimbaya
Angalia standard procedure ya kudeal na waandamaji Kwa mujibu wa utaalamu. halafu uje u comment tena. Risasi za moto zina wakati wake wa kutumika. Ni last option.
 
Ni kosa kubwa sanah walilofanya kutumia silaha za moto.. Haikupaswa kufanya hivo.. Mara ngap hutumia magar yao ya washa washa na mabom ya machozi..???? Na naamin hazikuwa vurugu kubwa sanah mpaka kuamua kutumia bastola na kurusha hewan ungali kuna mamia ya watu.. Hivyo muhusika anapaswa kuadhibiwa kwa uzembe wake.. !! Ili next time wawe more careful... Kakatusha ndoto za marehemu hadi familia ya marehem.. Let them pay for what they did..!! No Mercy on that..!!!
 
Eti wakikosea kidogo kwanza haifai kutumia silaha za moto kwa jambo hili usiseme walikosea kidogo
 
Nimesoma huu ujina ulioandikwa na mtoa mada!! Swali la msingi kwanini walitumia risasi za moto? Nguvu hiyo wameitumia siyo mara moja na kuumiza na kuua raia...why?
Kauli iliyowahi kutolewa na kiongozi mkuu nchini eti "WAANDAMANE WAKIONE" ilimaanisha nini? Ndohichi alitaka tukione?
 
Hivi polisi wa Tanzania ni lipi jema waliwahi kulifanya zaidi ya kulinda ccm , halafu zaidi ya risasi 30 walizofyatua walilenga kumuua nani ?
 
Eti kidogo, uko sawa kwa kuwa madhara yake ni madogo. Subiri yakufike, na ninaomba iwe hivyo kwako.
 
Mtoa mada ivi unajua uchungu wa kuondokewa na mtu wako wa karibu??!! Hivi marehemu angekuwa binti yako ungeongea huu upuuzi?? Wewe ni bwege au una bwana polisi ndio umekuja kumtetea. Muuaji ni muuaji na halibadiliki na kutulinda ni sehemu ya malipo yetu wananchi kwani si tunawalipa!
 
Polisi yakiri kupiga mtu risasi maandamano ya CHADEMA

View attachment 697076

Hahari za wakati huu ndugu kaka na dada zangu hapa jukwaani.

Mimi kama kawaida yangu huwa siwezagi kuandika maneno meeeengi sana zaidi ya kwenda straight to the point.

Kuna habari nimezisikia zikisambaa na pia kuthibitishwa na kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam ndugu Lazaro Mambosasa juu ya tukio la kuuwawa kwa bahati mbaya kwa mtu mmoja huko Kinondoni.

Kwanza napenda kumpongeza kamanda Mambosasa kwa kitendo tu cha kukubali ya kuwa risasi iliyotoa uhai wa mtu yule ilifyatuliwa kutoka katika silaha zinazomilikiwa na jeshi lake.

Huu ni ukomavu wa kitaalum sana kwa kamanda. Ninasema ni ukomavu kwa maana ya kwamba, Polisi still walikuwa na uwezo wa kukana kuhusika na tukio hilo, wakaunda tume ya kufanya uchinguzi kisha wakaleta majibu tofauti na ambacho kamanda amethubutu kikiri mbele ya umma wa watanzania.

Pili, napenda kuwaambia watanzania wenzangu ya kuwa, si ndani ya jeshi la polisi tu, hapana, bali ajali ni risk ambayo ipo katika kila kazi na kila taaluma.

Ni kweli inauma sana hususan kwa ndugu na jamaa waliopotelewa na mpendwa wao na ninawapa pole sana (my sincere condolences)

Nimeamua kuandika hivi baada ya kuona jinsi watu wanavyorusha matusi na lugha chafu kwa jeshi kana kwamba wao huwa hawafanyi makosa katika kazi zao.

Tunapokuwa tunalaumu pia tukumbuke ya kwamba ni polisi hawa hawa wa Tanzania na wala si wa kutoka nchi jirani kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ndio waliotokomeza wale wahalifu wa kule Kibiti waliokuwa wakiua watu kikatili.

Ni polisi hawa hawa ndio wanaopambana na mitandao ya uhalifu kama panya road na magenge mengine ya wahuni.

Ni polisi hawa hawa ndio wanaofanya patrol usiku kucha, wakati wa mvua na baridi kali, huku sisi tukiwa tumelala fofofo, tukiwa hatufahamu ni kipi kinaendelea nje ya mitaa yetu.

Ni polisi hawa hawa ndio wanaopambana na majambazi wanaovamia banks kwa lengo la kupora fedha zetu ili kukwamisha shughuli za maendeleo.

Hivyo mimi ninachoona ni kwamba, pale tunapokuwa tunalaumu ajali zinazotokea katika taaluma za watu (kama polisi) basi tusisahau pia na kazi njema wanazofanya to keep us safe and secure.

Ushauri wangu ni kwamba hii coverup this time around ifanywe na Waziri Nchemba kama political figure ndani ya wizara. Sio tena mkuu wa wilaya.

Wakaongee na familia ya marehemu kama wataridhia basi jeshi lichangie gharama za mazishi ama libebe gharama zote, if and only if, the family of the deceased will give go ahead and consent without any fraction of reluctance.

Nothing is easier than blaming others as if you're perfect katika kazi zako. Kilichotokea kwa polisi ni ajali kazini. Full stop.

Ninajua kuna baadhi watanitukana na kunikejeli na kusema najipendekeza kwa police ila huo ndio ukweli.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Haya ni mawazo yangu and I stand to be corrected.

"KIJANA IPENDE NCHI YAKO, TOA MAONI NA USHAURI BADALA YA KUTUKANA"

Poleni sana wafiwa.

Naomba kuwasilisha.

Good evening.

View attachment 697527

View attachment 697881

Follow me;
===========
Military Intelligence Coup: Kisa cha rubani aliyeiba na kutoroka na Ndege ya Kijeshi ya Iraq
==========
K.G.B Espionage na Ujasusi kwa njia ya ngono kama silaha ya vita. Honey trap/Honeypot....Part One (1)
==========
Serikali na TRA, mnaweza kuwezesha utoaji wa risiti za VAT kwa njia ya mobile SMS. I stand to be corrected
==========
Ushauri kwa Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya, Wizara ya michezo, TFF pamoja na BMT
==========
Wahandisi wa kampuni za simu, kwanini tusikwangue vocha kisha tukaingiza kwenye mobile money accounts zetu?
==========

Hivi hizi picha hazioneshi watu wasiojulikana kweli????
 
Serikali imeguswa sana na tukio hili ndio maana wakaamua kugharimia shughuli zote za mazishi. Thanks to the ministries and government at large kwa kuguswa kwenu.

Ndugu wa marehemu Poleni sana. Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.
 
Serikali imeguswa sana na tukio hili ndio maana wakaamua kugharimia shughuli zote za mazishi. Thanks to the ministries and government at large kwa kuguswa kwenu.

Ndugu wa marehemu Poleni sana. Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.
Wanafikii tuuu...!!
 
Back
Top Bottom