Muhimu: Channel 10 mbona mnadanganya

Mkimbizi

JF-Expert Member
Aug 23, 2008
222
34
Jana katika mechi ya Chelsea na Bordeaux, Channel 10 iliahidi kuonyesha.
Ilituonyesha mpira sisi wadanganyika lakini kwa uongo mkubwa. Mechi waliirekodi Channel e na bila kuwa na AIBU MIOYONI MWAO, walituwekea kuwa mechi ni LIVE.

Hivi mnajua sisi tumechoka kudanganywa? Maskini wenzangu na mimi wakakaa wakiangalia mechi kumbe wako takribani dakika 23 nyuma. NA MMEWEKA LIVE!!!!
MNABOA, iko siku mkiendeleza mambo ya uongo wa namna hii mtaonja joto ya jiwe.
Kama ilishindikana kuonyesha muda ule ulipoanza, mngetoa taarifa na pia LIVE mngetoa.
 
Badilisha hiyo title, ni tatizo la kiufundi,kwanza ulifuata nini huko Ch10, si ungeendelea kuangalia hiyo e channel.
 
Tatizo la kiufundi kwa 23 mins?? Kumbuka walitangaza wataonyesha mpira na muda ulipofika hawakuonyesha wala kutoa taarifa yoyote. After 20+ mins ndio wakaonyesha huku wameacha live mpaka mpira unaisha....?

Kuhusu kuangalia channel 10, kiila mtu ana uhuru wa kuangalia channel yoyote, ni mtazamo na ukweli ndugu
 
Jana katika mechi ya Chelsea na Bordeaux, Channel 10 iliahidi kuonyesha.
Ilituonyesha mpira sisi wadanganyika lakini kwa uongo mkubwa. Mechi waliirekodi Channel e na bila kuwa na AIBU MIOYONI MWAO, walituwekea kuwa mechi ni LIVE.

Hivi mnajua sisi tumechoka kudanganywa? Maskini wenzangu na mimi wakakaa wakiangalia mechi kumbe wako takribani dakika 23 nyuma. NA MMEWEKA LIVE!!!!
MNABOA, iko siku mkiendeleza mambo ya uongo wa namna hii mtaonja joto ya jiwe.
Kama ilishindikana kuonyesha muda ule ulipoanza, mngetoa taarifa na pia LIVE mngetoa.

Wabongo hatupendeki!

Kwangu mimi ambaye sina hiyo channel e ambayo nahis ipo dstv au GTV naona sawa tu, hata kama wangekuwa nyuma dakika 90 mwisho wa siku nimeona mpira wote mwanzo mwisho tena katika siku le ile kwa kweli nawashukuru tu, liwe tatizo la kiufundi au laa ni juu yao.
 
Kuhusu kuangalia channel 10, kiila mtu ana uhuru wa kuangalia channel yoyote, ni mtazamo na ukweli ndugu

Mkuu huna shukurani.....si ununue hiyo DSTV au G sport uwe unaangalia LIVE ya kikweli kweli.........tatizo la wa bongo bwana kulalamika lalamika tu watu wamewawekea muone mpira mnalalamika niambie station gani ya hapa bongo jana ilionyesha LIVE mpira........kitu unaonyeshwa bure unalalamika........weweee unalipia kuangalia chanel 10?????
 
Sio mbaya kwa sababu dakika 23 si nyingi kama ingekuwa siku nzima. Kwani Hapa watanzania tushazoea kupata taarifa baada ya tukio
 
Jana katika mechi ya Chelsea na Bordeaux, Channel 10 iliahidi kuonyesha.
Ilituonyesha mpira sisi wadanganyika lakini kwa uongo mkubwa. Mechi waliirekodi Channel e na bila kuwa na AIBU MIOYONI MWAO, walituwekea kuwa mechi ni LIVE.

Hivi mnajua sisi tumechoka kudanganywa? Maskini wenzangu na mimi wakakaa wakiangalia mechi kumbe wako takribani dakika 23 nyuma. NA MMEWEKA LIVE!!!!
MNABOA, iko siku mkiendeleza mambo ya uongo wa namna hii mtaonja joto ya jiwe.
Kama ilishindikana kuonyesha muda ule ulipoanza, mngetoa taarifa na pia LIVE mngetoa.

....Hawa si ndio hawaishi kujipigia upatu kuwa ...LIVE BILA ZENGWE!...??
wafahamu sasa kuwa wenzao wanapokuwa na 'matatizo ya kiufundi' sio kuwa wanapenda!!! teh teh.
 
nafikiri tusimlaumu mkimbizi. mimi pia nilikaa kusubiri huo mpira ambao nilijua unaanza saa tatu na nusu usiku. Ilipofika muda huo wao wakawa wanaonyesha kipindi cha dini ambacho walishasema tangu mchana kwamba kipo muda huo. Kwa hiyo tusiseme ni matatizo ya kiufundi bali ni maamuzi na wangepaswa watuombe radhi kwa walichokifanya. whether wanatuonyesha bure au la lakini kama wanatuonyesha mpira ambao si live waseme ili kila mtu anyeangalia ajue ukweli. live ni real time sio 23 minutes behind !
channel e wanakotoa mpira kule walionyesha kama kawaida na mimi nilipoona channel10 wamechelewa kujiunga nikaangalia channel e. kwa siku ya leo channel e wataonyesha mpira wakiwa wamechelewa maana wao huonyesha mieleka kwanza siku ya jumatano lakini pamoja na hayo watakapoonesha mpira huo ambao ni delayed hawasemi live. nafikiri mmenipata wandugu.
Ni vizuri kuacha maneno ya kejeli kwa mkimbizi maana ametoa dukuduku lake ambalo ni sahihi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom