Muhimbili wamethubutu na wameweza

Huku mwaisela hata shuka hakuna.mgonjwa wangu ameshindwa kupima vipimo vya nerve kisa ups ya computer hakuna inatia kinyaa hospitali hii
 
Bila hela ya ku push utasubiri sana. Juzi kuna daktari katuambia tutafute laki tisa ili mgonjwa wetu apelekwe chumba cha operation fasta!
 
Kwa kupenda vitu vipya na maonyesho waswahili hatujambo....

Kwanini tusiboreshe kwanza huku
 

Attachments

  • 1437509038373.jpg
    25 KB · Views: 181
Huku ni sawa na kumsifia muuza duka kwa kukuta sabuni mbuni ya kufulia (that is if kama kiwanda chenyewe akijafa bado mpaka leo) au kukuta sukari dukani kwake.

Hospitali inatakiwa kutibu na si kingine kuchelewa kwa kutoa huduma hizo ni kukosa priority au kufanya kazi chini ya kiwango, leo huduma ya matibabu ya moyo yanapatikana hospitali moja Tanzania nzima halafu unataka kusifia ndio "kipofu kaona mwezi" wakati vitu vya kawaida kabisa hospitalini.

Kuthubutu na kuweza ungekuja hapa kusifia jinsi wafanyakazi wanavyojali wagonjwa, smooth operation ya hospitali, usafi wa mazingira yao and all aspects of health quality.

Mpaka leo hospitali imejaa kunguru wanaovizia utupaji mmbovu wa uchafu wa hospitali hakuna ata incinerator ya kuchomea vitu, uitaji kuingia ndani na kujua ukienda kuna so much hazards zinazo weza leta milipuko mingi ya magonjwa ndani hospitali iliyojaa wataalamu wa afya.

Kila kitu ovyo mara dawa hakuna mara sijui hiki akipo, mara watu awajalipwa au awako happy na kiwango cha mishahara sitegemii morale hapo, halafu kuna mtu anaweza sifia vitu ambavyo vinatakiwa hospitali in the first place na bunge lijalo sijui itakuwaje kwenye kuisimamia serikari wakiingia hakina nanilii wakiongozwa na raisi wao Steven Nyerere; kaazi kweli kweli.
 
Kwa kupenda vitu vipya na maonyesho waswahili hatujambo....

Kwanini tusiboreshe kwanza huku

Na usishangae baada ya miezi miwili kusikia hyo machine imeharibika na husiisikie tena milele...tatizo la serikali yetu wanakimbilia makubwa wakati hata madogo yamewashinda....tatizo ni kwamba tangia tupate uhuru hatujawa na mtiririko mzuri wa kufanya mambo...tumekuwa watu wa kukurupuka tu ..leo tunashika hapa tunaacha...kesho pale...keshokutwa kule...yaani kero tupu..
 
Mkuu, Mleta mada.

Badala ya kuwatuhumu unaowaita "wapinzani" ingekuwa jambo jema pamoja na mambo mengine ungetuletea idadi ya viongozi wa CCM na serikali yake ambao wanatibiwa katika hizo zinazoitwa hospitali "zilizoboreshwa"

Lakini jambo jingine nikiri hapa kwamba mimi sina utalaamu wa masuala ya utabibu, hivyo naomba msaada wa mto mada kama tatizo la moyo ni matundu pekee?
 
Sisi tuliokuwa huku Muhimbili ndio tunaojua uhalisia wa mambo, hakuna OC toka Serikalini zinazokuja so unatarajia nini hasa kwa Mtanzania wa kawaida? Tafakari & Chukua hatua.
 

Kuwa na mitambo ni jambo moja na kupata huduma ni jambo lingine

Binafsi ndugu yangu amelazwa pale wiki ya tatu sasa hajapata huduma simply salio hamna inatakiwa 2m Iliafanyiwe manuva apate matibabu.

Nimejaribu kukomaa lakini hizo danadana nimeona naweza kumpoteza ndugu yangu tuna tafuta salio.
 

Afya ni ghari ndugu yangu, pole sana ndio maana Serikali inawahamasisha wananchi kuwa na bima ya afya katika maeneo yao maana tiba ni gharama! Maana hata machinga na wajasiriamali wanahimizwa kila leo kuwekeza kwenye Bima ya afya kwa sababu hiyo hiyo maana ugonjwa hauna taarifa!Nakushauri kama na wewe hauna bima ya Afya kata ili baadaye usiilaumu Serikali yako kwa mambo ambayo yako ndani ya uwezo wako kwa manufaa yako! Juhudi unayoitumia kukomaa kupata mil. 2 nakuomba uitumie hivyo hivyo kukata Bima ya Afya!Uguza salama ndugu!
 
Mkuu ni majanga, yahani taifa lenye
watu zaidi ya milioni 45 wanatumia ct-scan machines moja! huku mkiongeza idadi ya magari ya washa washa

Miaka yote hii ya uhuru, suala la kununua mashine ya moyo, CT-scan, MRI, haikustahili kuwa suala la kutangaziwa kitaifa.
Sasa hata kujenga flyover nchi nzima inatangaziwa na rais wa nchi na makamu wake wanaitwa kufungua daraja!
 
Miaka yote hii ya uhuru, suala la kununua mashine ya moyo, CT-scan, MRI, haikustahili kuwa suala la kutangaziwa kitaifa.
Sasa hata kujenga flyover nchi nzima inatangaziwa na rais wa nchi na makamu wake wanaitwa kufungua daraja!

Ushauri tu!Afya haina siasa!ni vizuri kufuatilia kwa makini elimu ya Afya ili kuepuka kupata magonjwa ambayo kimsingi yanaepukika!ulevi kupindukia,uvutaji wa sigara, madawa ya kulevya, utumiaji na unywaji wa vitu vikali kwa afya, matumizi ya kemikali, vipodozi na mazingira hatarishi!! Haya mambo ndo yanafanya watu kuteseka na magonjwa makubwa!Pia tatizo la watu kutokujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara kunafanya taifa lisiwe na watu wenye afya bali uwepo wa wingi wa watu wenye afya mgogoro!

Huduma za afya ni ghari hakuna asiyejua hilo ndo maana kuna baadhi ya mambo yanafanywa kwa awamu na sasa yamefanyika na hali iko tofauti na mchangiaji alivyosema!nimesema Siasa hazina nafasi kwenye afya, maaana afya ni uhai!Kama mchangiaji huna jipya bora ukae kimya tu na kupita kimyakimya kwenye uzi huu!
 

Huwezi kutenganisha ubovu wa huduma za afya na siasa, huwezi kutenganisha ubovu wa shule zetu na siasa, nk. Sijui una uelewa wa kiwango gani, lakini lazima ujiulize kwa nini urefu wa barabara za rami ndo mtaji wa kisiasa wa CCM? Mtoa mada anaandika kiusahihi kabisa kama CCM walivyozoea kwamba hata walipojenga bomba la maji shinyanga, waliamini ndo mtaji wao kisiasa. Waliponunua MRI machine, kila siku tulionyeshwa kuwa ndo mafanikio ya CCM! Of course tyhat is rubbish, lakini ndo walivyozoea!

Mimi nasema hivi bila kujali shida ya afya uliyonayo, haikustahili kusubiri miaka 54 ya uhuru bila kuwa na mashine ya moyo. Ni uzembe na upungufu wa akili za kupanga mambo ya maendeleo. Miaka 54 serikali haijajenga hospitali yoyote mpya, lakini serikali hiyo hiyo ina ofisi za CCM za magorofa kwa kila mkoa! Kila katibu na mwenyekiti ana gari la milioni 200.
Amua mwenyewe unachotetea.
 

Tatizo litabakia pale pale, Jee atahudumiwa hata masikini asiekuwa Hela au kigezo kitakuwa ni ni nani katowa Pesa mzuri ahudumiwe kwanza?
Hata kwa wezentu Ulaya matibabu yanalipiwa, lakini unapouguwa bila ya kuangalia kama unazo pesa au huna kitu cha kwanza ni madaktari kutimiza wajibu kukutibu na baadae wanaangalie Pesa za matibabu watazipata wapi?
Madaktari wetu wanaolipwa kwa kodi zetu wanamuacha Mgonjwa anakufa Kitandani, kisa hana pesa za kulipia.
Kwao pesa ni muhimu kulikoni maisha ya watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…