Muhimbili wakanusha habari za gazeti la uwazi.

Nkungulume

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
2,988
1,209
Katika gazeti la uwazi la tarehe 29/12/2015 ukurasa wa 3 kulikuwa na habari yenye kichwa cha "Aliyetoa siri ya Muhimbili alazwa chini".
Uongozi wa taasisi ya Moi ya unauarifu uma kwamba habari hiyo siyo ya kweli kwani mhariri hakufanya mahojiano na uongozi ili kubaini ukweli.
Taasisi ya Moi ilimpokea mgonjwa Chacha Makenga tarehe 18/09/2015 kwa madai kwamba ameshambuliwa na kuumizwa uti wa mgongo.
Chacha alitibiwa katika hospital ya Moi na katika kipindi chote alichokuwepo Muhimbili iligundulika kuwa hakuwa na ndugu aliyemtembea.
Baada ya kupatiwa matibabu mgonjwa aliruhusiwa lakini aligoma kutoka hospital hata pale alipokatiwa tiketi ya kwenda kwao Mgumu Msoma bado aligoma.
Uwazi watupe taarifa za ukweli njinsi walivyolishughulikia jambo hili.
 
Sasa baada ya hapo alipogoma kuondoka, nini kilifuata? Sasa yuko wapi anafanya nini?

Kwa nini useme alikuja kwa madai wakati wewe kama mtaaluma ulitakiwa kusema nini tatizo la mgonjwa wako?

Ulimlaza kwa kuwa alidai anaumwa ama kwa kuwa hata wewe uliona kuna tatizo la kushughulikia? Ulimtibu kwa madai yake ya kuumia uti wa mgongo ama ulimtibu kwa mujibu wa kile ulichokithibitisha kwamba ni tatizo?

Kutokutembelewa na ndugu nalo ni tatizo la kitabibu?

Je kama hakuwa na ndugu w akumtembelea ama mwenye uwezo wakusafiri hadi muhimbili kutoka Mugumu, wewe shida yako ninni? Hili nalo ni tatizo hadi uliandike hapa?


Ulitakiwa kusema hapana. Hajalazwa chini na badala yake amefanywa abc. Au ndiyo amelazwa chini kw asababu ya abc.

Ukijibu bila hoja ukiwa off point, ujue unazidi kuonyesha kweli kuna tatizo kati ya ko na mgonjw awako.

Tuambie sasa yuko wapi. Kama mnaye hapo a halaziwi chini ama analzwa chini kwa nini lakini si kutuambia eti alikja ikabainika hana ndugu wa kumtembelea. Je ndiyo sababu ya kumlaza chini?
 
Back
Top Bottom