Muhimbili na Utata Mkubwa

American nigga

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
667
944
Nilipata dharula Usiku baada ya Mdogo wangu kuugua Ghafla ikabidi twende Muhimbili kwa Matibabu ya dharula, Cha kushangaza ni Maswali niliyoulizwa Reception. "Mmekuja na usafiri gani!," "Unafanya kazi Gani,!" Haya maswali unaweza kuyaona ni maswali ya kawaida ila ni maswali yenye utata sana hasa Hospitali ya Serikali ( Ya watu wote)

Je ikiwa Nimeletwa Na Guta Sio naweza kutupiwa mochwari kabla hata ya matibabu! Na ikiwa Nimekuja na Benz mazingira ya rushwa hayatazuka hapo?

Vipi nikisema kazi yangu ni waziri Au Meneja wa Vodacom! matibabu yangu yanaweza kufanana na mwenye kazi ya kubrash viatu, au mgonga ulimbo mtaani?

Kwanini Msiulize maswali basic yanayohusiana na tiba kwa ujumla kama Umri, bima, na hali ya mgonjwa. huku kuulizana umekuja na usafiri gani mnataka mjue ili mfanye nini, mbona siwaelewi.
 
Duh hii nchi hii 😅😅😅
 
Ndugu wa wagonjwa kuweni wastaarabu kuna details zingine ni za kujaza kwenye file la mgonjwa ,lakini mkiulizwa mnawaona madaktari masnitch ,hebu jaribuni kuwatibu wagonjwa wenu nyumbani muone Kama mtaweza,
 
Hapo mazingira ya rushwa yanatengenezwa kwa ulazima. Hizi hospitali kubwa za Serikali wanaupuuzi mwingi sana, lakini ukiwakuta wanavyojinasibu huko nje utafikiri ni Malaika wameshushwa kutoka Mbinguni.
 
Kama wewe ni daktari tuambie kazi ya Mgonjwa Itasaidia nini kwenye kumtibu mtu aliepata ajali
Kazi ya mtu ni moja ya details muhimu kwenye matibabu ya mgonjwa
Na ndio sehemu muhimu ya kupata risk factors
Mfano
Kazi za ofisini (kukaa Sana kwa muda mrefu)_ risk ya kisukari , hypertension/presha
Kazi za migodini /viwandani : pneumoconiosis, occupational lung diseases, lung cancer
Uvuvi /watu wanaoishi ziwani : risk ya kichocho nk
Siwezi kukueleza yote Ila jaribu kuheshimu professions za watu
 
Back
Top Bottom