Kama sio loliondo, twalazwa ka mitumba,
Usidhani ni uhondo, hatulali kwenye nyumba
Drip kwenye mipodo,zahanati kwa kuyumba,
Miaka 50 ya Uhuru, hakika tumesonga mbele
Wamama na yao matumbo, bajaji wazipakia
Kweli hawana tambo, sakafuni wajifungulia,
Matabibu huwa jambo, wagonjwa kuangaliia,
Miaka 50 ya Uhuru, hakika tumesonga mbele
Nani anabisha??????
Jeuri ya chama Twawala.