Muhimbili kuna utaalamu, dawa na vifaa tiba vya kutosha? Mbona majeruhi wengi wa moto wa lori la mafuta wanafariki?

G4N

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
1,458
3,585
Inasikitisha sana kwamba manusura wa ajali ya moto wa lori la mafuta lililoanguka pale Itigi Msamvu Morogoro wanazidi kufariki pale Muhimbili.

Madaktari walituhakikishia kwamba watatumia kila aina ya ujuzi wao ili kuokoa maisha. Sasa kwann vifo vinazidi kuongezeka?

Je, ni utaalamu duni wa madaktari wetu? Ndiyo maana wakashindwa kuelewa uzito wa tatizo na kukubali kubeba dhamana ya kuwatibu majeruhi wale badala ya kuwapeleka nje ya nchi?

Je, ni serikali iliona aibu kuwapeleka majeruhi hao nje? Maana imejinasibu sana kwamba kwa sasa tiba zote zinapatikana nchini.

Swali la msingi hapa ni kwanini majeruhi wale kila siku wanafariki? Hivi sasa wamebakia 20 tu.


UPDATES from my inbox and comments

*sasa majeruhi wamebakia 17 tu kati ya 47 waliopelekwa MNH, maana yake 64% wamefariki..

*yawezekana kulikuwa na delay ktk kuwapatia huduma wagonjwa, hasa dawa na vifaa tiba. Yasemekana pale Morogoro dawa na baadhi ya Vifaa tiba vlitolewa na Aboud. Now you can imagine hiyo delay iliyotokea tangu kubaini uhaba WA madawa na vifaa tiba hospitalini mpk mtu binafsi kuamua kuvipeleka..

* pale MNH madawa pia yalikuwa pungufu na madaktari walikuwa wachache ikabidi serikali iagize madawa toka MSD na kuazima madaktari toka jeshini. Think of the delay.

*wagonjwa wa majeraha makubwa ya moto walipaswa kuwekwa kwenye majokofu maalumu na siyo kulazwa kwenye vitanda kama ilivyokuwa. Nadhani yule mgonjwa aliyekuwa anatetemeka alionekana kwenye TV. Hii si sawa..

*wagonjwa wengi walienda MNH wakiwa wanajitambua, wanaongea na mpk siku ya pili yake(baada ya kuwa MNH kwa masaa 24) waliweza kuongea na kupokea hela toka kwa mhe Rais alipowatembelea.
. Sasa hii excuse inayotolewa eti wagonjwa waliungua 80% na zaidi haiingii akilini kabisa kwa hali waliyokuwa nayo siku ya pili na vifo vingi namna hii kutokea.

MASWALI yasiyojibika..

Wangekuwa ni wabunge/mawaziri/wakubwa serikalini ndiyo wameungua, kweli wangepelekwa MNH na kuachwa wafe mmoja mmoja kama hao walalahoi wa Morogoro?

MAPENDEKEKEZO toka inbox.
Wengi wanapendekeza wagonjwa wangepelekwa kutibiwa nje ya nchi
 
Labda mtoa mada wagonjwa tuliowapeleka nnje wakafariki tatizo huwa linakua nini?
Nwanzisha uzi anafikiri huko nnje kuna miujiza, kuna baadhi ya mambo hayawexekani kutibika hata uende nchi Gani. Mtu kaungua more than 80% halafu unataka kuwalaumu madaktari
 
Nadhani kama kuna watu wa kulipwa hela nyingi ni Madk hasa katika nchi hizi za Dunia ya tatu..Wanafanya kazi kubwa sana kwa kweli halafu hawatoshi.

Ni mhimu kuangalia pia vifaa na utayari wa Hospitali zetu kwa kupeleka vifaa zaidi
 
vingekuwepo watu wangekuwa wanapelekwa India?

sidhani kama Spika Ndugai alipenda kuspendi billions za kodi zetu kutibiwa nje...
 
Back
Top Bottom