Muhimbili hii ni aibu, msipotumbuliwa ntashangaa

Muhimbili hii ni aibu, msipotumbuliwa ntashangaa

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,341
Reaction score
15,842
lab.jpg


Wakuu nimekutana na habari hii kutoka gazeti la The citizen kuhusu maabara ya kisasa iliyogharimu zaidi ya Tsh 2 Billion kwa ufadhili kutoka Uturuki lakini cha kusikitisha inamiaka karibu miwili eti bila matumizi na badala yake sampuli zinapelekwa India licha ya maabara hiyo kutoa majibu sawasawa na yale ya India.

Tena bila aibu viongozi wa Muhimbili wanasema kabisa sample kupelekwa kwenye hiyo maabara na nyingine inapelekwa India na majibu kurudi yaleyale. Mtaalam kutoka Uturuki Prof Fatmahan Atalar ambae anasimamia mradi huo kuhakikisha wataalamu wetu wanajua kutumia maabara hiyo amelalamika hali ya kushangaza ya wataalamu wetu kukwepa kabisa kujifunza na kutumia maabara hiyo achilia mbali kupeleka tu sampuli hapo licha za juhudi zake binafsi kuzunguka idara zote kuwahamasisha lakini wote wanakacha.

Cha kushangaza zaidi hata reagents tu kuhudumia hiyo maabara hawataki kununua hali iliyopelekea mtaalam huyo kutoka Uturuki kutumia pesa yake binafsi kiasi cha shilingi milioni 140 ambazo aliahidiwa kurudishiwa lakini kapigwa changa la macho.
Maabara hiyo ya aina yake inaweza kuokoa maisha ya watu wengi afrika mashariki na kati kwa mujibu wa Prof huyo.

My Take; Waziri wa afya anapaswa kutoa tamko juu ya nini hasa kimepelekea hii hali na kwanini baada ya The citizen kuanika hii ndio waseme sasa wataanza kuitumia?

Pili uwezo wao wa akili na shule zao upimwe kwanini wakimbie mitini hata kujifunza tu kama shule zao sio za magumashi?

Mwisho ikiwezekana wakapimwe mkojo igundulike kama kuna vitu wanatumia vinavyodhoofisha uwezo wao wa kufikiri.

Sh2 billion lab stands idle for nearly 2 years
 
lab.jpg


Wakuu nimekutana na habari hii kutoka gazeti la The citizen kuhusu maabara ya kisasa iliyogharimu zaidi ya Tsh 2 Billion kwa ufadhili kutoka Uturuki lakini cha kusikitisha inamiaka karibu miwili eti bila matumizi na badala yake sampuli zinapelekwa India licha ya maabara hiyo kutoa majibu sawasawa na yale ya India. Tena bila aibu viongozi wa muhimbili wanasema kabisa sample ikipelekwa kwenye hiyo maabara na nyingine inapelekwa India na majibu kurudi yaleyale. Mtaalam kutoka Uturuki Prof Fatmahan Atalar ambae anasimamia mradi huo kuhakikisha wataalamu wetu wanajua kutumia maabara hiyo amelalamika hali ya kushangaza ya wataalamu wetu kukwepa kabisa kujifunza na kutumia maabara hiyo achilia mbali kupeleka tu sampuli hapo licha za juhudi zake binafsi kuzunguka idara zote kuwahamasisha lakini wote wanakacha. Maabara hiyo ya aina yake inaweza kuokoa maisha ya watu wengi afrika mashariki na kati kwa mujibu wa Prof huyo.

My Take; Waziri wa afya anapaswa kutoa tamko juu ya nini hasa kimepelekea hii hali na kwanini baada ya The citizen kuanika hii ndio waseme sasa wataanza kuitumia?
Pili uwezo wao wa akili na shule zao upimwe kwanini wakimbie mitini hata kujifunza tu kama shule zao sio za magumashi?
Mwisho ikiwezekana wakapimwe mkojo igundulike kama kuna vitu wanatumia vinavyodhoofisha uwezo wao wa kufikiri.

Sh2 billion lab stands idle for nearly 2 years
Umeandika vizuri ila mkojo kapime wewe na familia yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa singida,kuna hospital ya rufaa ilijengwa na akonay akiwa mkuu wa mkoa,kwa msaada wa marafiki zake kutoka ulaya,imekamilika na inakila kitu.sasa ni mwaka wa pili,haijazinduliwa,sababu hakuna wataalum hasa madaktari bingwa.kwahiyo hilo la muhimbili siwez kushangaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbunge wa Singida kwanini akiwa siku she haya bungeni?
 
Andika vizur kwanza sio maabara tu sema maabara ya mambo ya GENETICS.

Maana kama ni hiyo inayihusiana na mambo ya genetics sio ishu ndogo wewe mambo ya DNA
ngeshanga kuwa ni kitengo cha parasitology,au haematology ndo wanapeleka sample nje hapo kungekuwa na walakin maana hayo mambo sio complcate kivile
Lakin hiyo ya genetic sio kitoto mkuu na kama walokuwa wapeleka ili kulinganisha majibu watakayotoa waindia na yao mbona hakuna shida maana ni kujipa uhakika zaidi .
 
Serikali iwekeze hela nyingi kwa hawa madaktari ili tuwe nao wakitaalamu zaidi na kwa wingi

Hizo mashine na reagents zitapatikana tu. Ni sawa na kununua gari wakati hakuna anayejua kuliendesha, litapata kutu na kukongoroka.

Kwa wastani hatuna wataalamu kabisa
 
Dr. Maseru, RIP,
Mwambie mturuki awe makini kwa kweli, hii ni "bongo bahati mbaya" ni nchi ya mizengwe na vituko show.

Mwambie, Prof, ajiangalie wasije wakamtuma kwenye futi sita na pembe nne kabla ya siku zake.
 
Serikali iwekeze hela nyingi kwa hawa madaktari ili tuwe nao wakitaalamu zaidi na kwa wingi

Hizo mashine na reagents zitapatikana tu. Ni sawa na kununua gari wakati hakuna anayejua kuliendesha, litapata kutu na kukongoroka.

Kwa wastani hatuna wataalamu kabisa
Ukiisoma habar vizur inaonsha kuwa mama kaja kuchek alichowekeza kama kinafanya kazi
Kafika amegonga kila mlango
Hajakuta utendaji unafanyika

Kaambiwa kuwa wamepeleka sample India kutest sawa sio mbaya sanaa hii ishu ilivokaa
Ni kuwa huenda machine na reagents alizonunua mama kwa bei nyingi atakuwa kabigwa cha
Juu.
Watu wamenunua kiasi kidogo wamesepa na ela nyingi ndo maana hata kama sample imeenda nje kutestiwa ila pangebaki hata zile amshaamsha kuwa sehem hiyo panafanyiwaga testing.

CHUKUA CHAKO MAPEMA [emoji23][emoji23]
 
Afundushe kienyeji and then mtu aache majukumu yake and baadae naibu wazuri akijakukuomba cheti huna sababu unefundishwa kienyeji wengi tulimkatalia huyo mama and then huwa anajirahisisha sana
 
Ni aibu kwa kweli yaani tunatesana wenyewe Mungu anatuona watanzania.
 
Back
Top Bottom