Muhidini Issa Michuzi Huu Sasa ni Uhuni!

Hivi globu ni nini?

Jabulani globu inakujaje hapa? kwa kiswahili kungine naweza kusema globu ni taa, balbu au kitu kama hicho, inaweza kuwa tufe au kitu chenye umbo kama dinia.

Kama ulitaka kuuliza kuhusu blogu hii ni kitu nyingine kabisa. Hii ndiyo inazungumziwa hapa. Ni free online forum inayoweza kuanzishwa na mtu yoyote kwa kutumia domaina name ya blogspot. Kama aliyoanzisha michuzi.

It is a cheap thing, hata watoto wa shule za msingi wanaweza kuanzisha. Ni tofauti sana na kitu kama Jamiiforums kwa uendeshaji na professionalism.
 
Mwenye shida ni wewe. Ulifuata nini huko wakati wenzio tulishaacha kupatembelea miaka mingi? hata link yao sijui.

Ni makosa kwenda mtoni kuoga ukakuta na mama yako anaoga na ukaendelea kuchungulia chungulia. We ukishaona mama yu uchi kwa haraka geuza shingo na usiangalie huko tena. Kosa si kumuona mama uchi kosa ni kuendelea kumuangalia akiwa uchi.

Majibu kama haya ndo nayachukia kupita yote! He is a civil servant and the simplicity of the matter is that, HE SHOULD NOT BE BIASED! Kama ni hivyo, aache kabisa kuweka picha za serkali na aanze za chama. Maana jinsi alivyo-potrait blog yake, ni tofauti na anavyofanya sasa ivi!
 
Kwanini Tunarudia Masuala ya Issa Michuzi; Yeye ni Mfanyakazi wa Serikali ya CCM, anaishi na kula kwasababu ya Serikali ya CCM kwahiyo ni lazima awe na mapenzi ya hicho chama... sidhani kama kuna waandishi wa serikali kwenye Chadema au CUF.

Kwahiyo hiyo BLOG yake ni one sided --- let it be --- Siiangalii Tena it is one sided

"Up to five goals is journalism. After that, it becomes statistics."

:A S-danger:Je serikali ikichukuliwa na upinzani na yeye atabadilika? Kama ni hivyo basi yeye ni opportunist and therefore a dangerous blogger.
 
Wanakarilikuwa ukiwa mpiga debe wa ccm nirahisi kupata kacheo ka upendeleo kama hivi udc etc!Ujinga uliotawala mawazo yao tena kwa mwana habari wanatia kinyaa! nakuharibu tasinia hiyo:mad2:
 
Yule jamaa ni mshikaji wake na JK, hivi nyie hamuonagi kila press-conference zinazofanyika Ikulu mchizi lazima awemo na lazima aulize swali la kinafiki.
 
nimeona hii kweli noma,
halafu duh CCM wana mabango makubwa namna jile mbona wanatumia pesa nyingi sana ,kweli wana hofu.


Hawayalipii ushuru, ni bure kila kitu bure kuanzia kutengeneza hadi kuyaweka pale, kuna watu wameumizwa hapo. wanasubiri fadhila za JK & Family Co. Limited baada ya kampeni.
 
Kwa jinsi hii kama ndio ukuu wa wilaya utakavyopatikana basi viongozi nchini kutakuwa hakuna kitu ambcho sidhani labda ni kujipendekeza tu. wengine wameumbwa hivyo. hata kule Afrika jkusini wakati weusi wakipigania haki zao toka kwa weupe miongono mwao kulikuwa na "mapappet" wa kuwakumbatia weupe(sina maana ya ubaguzi wa rangi ila nina maana natakla kuonyesha watu wa aina ya kujikomba wakati taabu wanaiona na wanaihitaji uhuru.
Ukuu wa wilayaaaa huanza poooole pole...
 
Wakuu nilikuwa napitia pitia katika globu mbalimbali nikabahatika kuangukia kwa inayoitwa globu ya jamii ya Muhidini Issa Michuzi. Nimeshangazwa na habari picha nilizoziona zikionyesha mikutano ya kampeni ya chama cha upinzani chadema huku baadhi ya picha zikiwa na ujumbe wa bango la chama tawala. Nionavyo hapa golobu ya jamii imekiuka maadili ya uandishi kwa makusudi.

Maana kwa kufanya hivyo ni sawa na habari ile kuwa inapotosha mtazamaji/msomaji wake. Ujumbe wake hauendani na taswira inayoonekana au mwandishi alivyokusudia.

Picha inaonyesha kampeni za chadema sehumu kubwa ya picha hiyo imetolewa bango la CCM, huu si upotoshwaji wa makusudi na kukiuka maadili ya kihabari yanayotaka habari isipotoshe umma kwa muonekano wake ama kwa ujumbe wake?

Mimi si mwandishi/mpiga picha ila najuwa kuwa hakukuwa na ulazima kwa globu ya jamii kupiga picha zile kwa namna ile huku wakijuwa kuwa haitaleta tafsiri sawa, vinginenvyo niamini kuwa imefanywa makusudi kuwadhalilisha na kuwafedhehesha wapinzani na kampeni zao, kwa kuipendelea CCM!

Picha, kwa wataalamu wanajuwa, kuwa inaweza kupigwa ama horizontal, aerial or oblique...na angle zote hizo unaweza kuepuka object ambayo hutaki itokee katika picha, tuseme Michuzi hafahamu hili au anafanya makusudi uhuni huu?

Kama golobu ya jamii inaona kero kuweka picha za vyama vya upinzani si wasiweke tu, kwani nani anawalazimisha waweke kihuni huni kama vile?

Hivi Michuzi akiambiwa anaipendelea CCM ndiyo anafanya inadi na inda kwa kufanya uhuni wake kama vile!
Michuzi haoni haya kuwa anajishusha kikazi kwa kuweka picha zenye ujumbe wa kupotosha kama zile?

Wapenda mageuzi na maadili ya uandishi wanapaswa kulani uhuni huu wa golobu ya jamii ya kupotosha kwa makusudi maadili ya picha za kihabari na uandishi kwa ujumla.

Hili tamko halijamtendea haki Issa. Nimetembelea blog hiyo na kuziangalia picha kwa umakini. Nilichogundua ni waandaaji wa Mkutano wa CHADEMA hawakuwa au si makini kwani waliandaa mkutano kwenye uwanja ambapo kuna Bango la CCM angalia picha hapa chini. Tuzungumze hoja na si Ushabiki. KATIBU MWENEZI WA CHADEMA MORO_.JPG
 
wa kumlaumu ni huyo wa chadema aliyeamua kufanya mhadhara pale akiwa na mabango yale nyuma yake, kama hakuwa na alternative basi angeweka cover ya mashuka kwa nyuma

we blame too much these days
...Ashajichokea huyo mwandishi unapaswa kuheshimu maadili ya uandishi wa Habari angekuwa nchi za watu huyu tayari angekuwa tayari keshawajabishwa kwa kushindwa kuilinda kazi yake na maadili ya kikazi
 
inavyoonekana Chadema hawakuwa na jinsi, vibali vya kufanyia mikutano vinatolewa na serikali ya ccm hiyo ilikuwa ni moja ya njia kuhujumu kampeni za chadema, huyu Michuzi si mwandishi wa habari anatumia blog yake kuganga njaa, hana ujanja wa maisha ndio maana haishi kujikomba, michuzi ni kama changudoa fulani hana mpango ! Tatizo linamkabili michuzi hana vyeti wala haijui fani ya uandishi wa habari, unakumbuka JK alipoanguka jangwani aliweka clip jiulize ilikaa kwa muda gani?
 
Wana jf mnaosema kuwa mithupu kakosea kutoa ile picha ur all wrong: walaumuni chadema kwa kuweka jukwaa chini/mbele ya bango la sisiem.
 
Ilishangaza sana, kampeni za chadema lakini bango linasema chagua ccm!!! huu ni upotoshaji aksini!!!
 
...Ashajichokea huyo mwandishi unapaswa kuheshimu maadili ya uandishi wa Habari angekuwa nchi za watu huyu tayari angekuwa tayari keshawajabishwa kwa kushindwa kuilinda kazi yake na maadili ya kikazi

Manchester; you are not being fair on this. Hata angekuwa mpiga picha kutoka ughaibuni lazima bango hilo lingeonekana. Pamoja na mapenzi yako kwa CHEDEMA; lakini kwa hili Chadema wajilaumu wenyewe na si mpiga picha.
 
Mwambieni prof Baregu kwamba Chadema hawawezi kupata ushindi kwa startegy ya JF na magazeti tu. Inabid kwenda mbali zaidi. Kuna wagombea wanajitoa na hamtaki hayo yasemwe. JF mara kadhaa wanafuta thread zinazoisema chadema na slaa vinginevyo. Nawatakia kujifariji kwema.
 
Hapo njia ni moja tu ! msiitembelee kama ina waboa. Binafsi huwa naingia jamiiforums nikitoka naingia facebook na yahoo siku imeisha.
 
Mwenye shida ni wewe. Ulifuata nini huko wakati wenzio tulishaacha kupatembelea miaka mingi? hata link yao sijui.

Ni makosa kwenda mtoni kuoga ukakuta na mama yako anaoga na ukaendelea kuchungulia chungulia. We ukishaona mama yu uchi kwa haraka geuza shingo na usiangalie huko tena. Kosa si kumuona mama uchi kosa ni kuendelea kumuangalia akiwa uchi.


Asante!!!!!!!
 
Sijui watasema nini baada ya 31.10.2010 hawa watu TSN na TBC, maana wamempiga sana vijembe bosi wao mpya. Wangeanza kutafuta ajira kule Global Publishers wakaandike udaku wao huko.
 
Back
Top Bottom