Muhidini Issa Michuzi Huu Sasa ni Uhuni!

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
Wakuu nilikuwa napitia pitia katika blogu mbalimbali nikabahatika kuangukia kwa inayoitwa blogu ya jamii ya Muhidini Issa Michuzi. Nimeshangazwa na habari picha nilizoziona zikionyesha mikutano ya kampeni ya chama cha upinzani chadema huku baadhi ya picha zikiwa na ujumbe wa bango la chama tawala. Nionavyo hapa blogu ya jamii imekiuka maadili ya uandishi kwa makusudi.

Maana kwa kufanya hivyo ni sawa na habari ile kuwa inapotosha mtazamaji/msomaji wake. Ujumbe wake hauendani na taswira inayoonekana au mwandishi alivyokusudia.

Picha inaonyesha kampeni za chadema sehumu kubwa ya picha hiyo imetolewa bango la CCM, huu si upotoshwaji wa makusudi na kukiuka maadili ya kihabari yanayotaka habari isipotoshe umma kwa muonekano wake ama kwa ujumbe wake?

Mimi si mwandishi/mpiga picha ila najuwa kuwa hakukuwa na ulazima kwa blogu ya jamii kupiga picha zile kwa namna ile huku wakijuwa kuwa haitaleta tafsiri sawa, vinginenvyo niamini kuwa imefanywa makusudi kuwadhalilisha na kuwafedhehesha wapinzani na kampeni zao, kwa kuipendelea CCM!

Picha, kwa wataalamu wanajuwa, kuwa inaweza kupigwa ama horizontal, aerial or oblique...na angle zote hizo unaweza kuepuka object ambayo hutaki itokee katika picha, tuseme Michuzi hafahamu hili au anafanya makusudi uhuni huu?

Kama blogu ya jamii inaona kero kuweka picha za vyama vya upinzani si wasiweke tu, kwani nani anawalazimisha waweke kihuni huni kama vile?

Hivi Michuzi akiambiwa anaipendelea CCM ndiyo anafanya inadi na inda kwa kufanya uhuni wake kama vile!
Michuzi haoni haya kuwa anajishusha kikazi kwa kuweka picha zenye ujumbe wa kupotosha kama zile?

Wapenda mageuzi na maadili ya uandishi wanapaswa kulani uhuni huu wa golobu ya jamii ya kupotosha kwa makusudi maadili ya picha za kihabari na uandishi kwa ujumla.http://www.issamichuzi.blogspot.com/
 
Shouldn't he be told via his blog so that ujumbe umfikie kwa haraka zaidi...?
 
..Chadema na vyama vingine vianzishe blogs zao ili kuepuka upendeleo wa Muhidin Michuzi.

..Michuzi ni nyinyi wenyewe ndiyo mnaompa umaarufu.
 
mi wala hiyo blogs wala hata, siifungui, kutokana, michuzi ni kama TBC, yaani TBC+MICHUZI=CCM
 
Watu kama hawa ni kuwasusia tu. Kwanza tunamjua - Michuzi mtu wa system - kila safari ya nje ya JK naye yumo! Analinda maslahi ya wakubwa!
 
Wahuni ni wana Chadema wenywe, Michuzi sie aliepiga hizo picha. Wamepiga wenyewe wakamtumia ili "arushe" sasa hapo kosa la nani? asipotoa picha za Chadema taabu akitoa "uhuni" ukisikia wivi wa fadhila ndio huo sasa....
 
una hakika gani kuwa wanachadema ndio wamepiga picha? kwani wewe ni michuzi? mijitu mingine bana inaboa kweli
 
MKUU KAMA MICHUZI ANAKUKERA ANZISHA YA KWAKO NI BUREE KABISA .. ALAFU USITEMBELEE TENA BLOG YAKE! SIMPLE:becky:
 
nimeona hii kweli noma,
halafu duh CCM wana mabango makubwa namna jile mbona wanatumia pesa nyingi sana ,kweli wana hofu.
 
Kwanini Tunarudia Masuala ya Issa Michuzi; Yeye ni Mfanyakazi wa Serikali ya CCM, anaishi na kula kwasababu ya Serikali ya CCM kwahiyo ni lazima awe na mapenzi ya hicho chama... sidhani kama kuna waandishi wa serikali kwenye Chadema au CUF.

Kwahiyo hiyo BLOG yake ni one sided --- let it be --- Siiangalii Tena it is one sided

"Up to five goals is journalism. After that, it becomes statistics."
 
Jamani Broda michuzi msimlaumu shida elimu pale ni mgogoro ujanja ujanja wa mjini tu!
 
Yote ni njaaaaa izo nashindwa waelewa hawa watu ni nini matatizo yao kweli wanashindwa fikisha ujumbe kwa viongozi wa wa juu wa CCM kuwa kuna baadhi hawatakiwiii
 
wa kumlaumu ni huyo wa chadema aliyeamua kufanya mhadhara pale akiwa na mabango yale nyuma yake, kama hakuwa na alternative basi angeweka cover ya mashuka kwa nyuma

we blame too much these days
 
Wakuu nilikuwa napitia pitia katika globu mbalimbali nikabahatika kuangukia kwa inayoitwa globu ya jamii ya Muhidini Issa Michuzi. Nimeshangazwa na habari picha nilizoziona zikionyesha mikutano ya kampeni ya chama cha upinzani chadema huku baadhi ya picha zikiwa na ujumbe wa bango la chama tawala. Nionavyo hapa golobu ya jamii imekiuka maadili ya uandishi kwa makusudi.

Maana kwa kufanya hivyo ni sawa na habari ile kuwa inapotosha mtazamaji/msomaji wake. Ujumbe wake hauendani na taswira inayoonekana au mwandishi alivyokusudia.

Picha inaonyesha kampeni za chadema sehumu kubwa ya picha hiyo imetolewa bango la CCM, huu si upotoshwaji wa makusudi na kukiuka maadili ya kihabari yanayotaka habari isipotoshe umma kwa muonekano wake ama kwa ujumbe wake?

Mimi si mwandishi/mpiga picha ila najuwa kuwa hakukuwa na ulazima kwa globu ya jamii kupiga picha zile kwa namna ile huku wakijuwa kuwa haitaleta tafsiri sawa, vinginenvyo niamini kuwa imefanywa makusudi kuwadhalilisha na kuwafedhehesha wapinzani na kampeni zao, kwa kuipendelea CCM!

Picha, kwa wataalamu wanajuwa, kuwa inaweza kupigwa ama horizontal, aerial or oblique...na angle zote hizo unaweza kuepuka object ambayo hutaki itokee katika picha, tuseme Michuzi hafahamu hili au anafanya makusudi uhuni huu?

Kama golobu ya jamii inaona kero kuweka picha za vyama vya upinzani si wasiweke tu, kwani nani anawalazimisha waweke kihuni huni kama vile?

Hivi Michuzi akiambiwa anaipendelea CCM ndiyo anafanya inadi na inda kwa kufanya uhuni wake kama vile!
Michuzi haoni haya kuwa anajishusha kikazi kwa kuweka picha zenye ujumbe wa kupotosha kama zile?

Wapenda mageuzi na maadili ya uandishi wanapaswa kulani uhuni huu wa golobu ya jamii ya kupotosha kwa makusudi maadili ya picha za kihabari na uandishi kwa ujumla.
Mwenye shida ni wewe. Ulifuata nini huko wakati wenzio tulishaacha kupatembelea miaka mingi? hata link yao sijui.

Ni makosa kwenda mtoni kuoga ukakuta na mama yako anaoga na ukaendelea kuchungulia chungulia. We ukishaona mama yu uchi kwa haraka geuza shingo na usiangalie huko tena. Kosa si kumuona mama uchi kosa ni kuendelea kumuangalia akiwa uchi.
 
Back
Top Bottom