Muhenga unakumbuka wapi sindano za kuchemsha?

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,197
Reaction score
10,710
Miaka ya nyuma, sindano baada ya matumizi zilikuwa hazitupwi. Zikitumika zinachemshwa kwenye maji ya moto kama inavyoonekana pichani na baadaye hutumika kuchoma tena watu wengine. Sindano inatoka kwenye sufuria huku maji yakiwa moto balaa.

Nakumbuka kuna kipindi bro alikwenda shule na wakapewa chanjo walichomwa sindano moja darasa zima. Aliporudi alikuwa analia hatari akidai sindano ni ya moto kupita maelezo.

Siku hizi ni sindano moja mtu mmoja, ukishachomwa inatupwa. Unakumbuka wapi Muhenga?
 
Kuna siku ilivyokaribia muda wa kuchoma sindano nikaenda kucheza mbali, basi waktumwa njemba kunitafuta, nilipowaona zikaanza mbio za marathon, aisee , walinikamata wote tupo hoi.., wakanibeba juu gadi hospitali, nilipofika na kuona lile bomba, nikawaponyoka.., kazi ikaanza upyaaa
 
Kulwenge -Bwasi -MAJITA 1989 surua ikiwe imenipiga kisawasawa.
 
Sindano ya moto inawekewa kristapeni.Atakayedungwa hiyo sindano lazima ateme mate kwa kutumia macho.
 
Kuchoma sindano ni kazi kama kazi zingine 😃
 
krista pen dawa ile ni balaa unahisi inapita mpaka kwenye moyo
Niliowahi kuchomwa hiyo sindano kukausha kidonda,nilienda hospital nimevaa sandals(sendo), nilirudi nimezishika mkononi,niliziona nzito siziwezi kuvaa mguuni!
 
Niliowahi kuchomwa hiyo sindano kukausha kidonda,nilienda hospital nimevaa sandals(sendo), nilirudi nimezishika mkononi,niliziona nzito siziwezi kuvaa mguuni!
Aisee unaweza kuziacha sendo huko huko ukazisahau!
 
Sindani zilikuwa zinauma hizo. Ukiumwa Chochote ni mwendo wa sindano tu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…