50thebe
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 4,139
- 4,124
Hakika lile neno la kimombo linalotafsirika haraka haraka kama 'kwenye siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu' limejidhihirisha kwa moja ya nchi zinazounda umoja wa jumuia ya maendeleo ya kusini mwa Afrika (SADC). Nchini Zimbabwe, chama kilichowaongoza Wananchi wake kuung'oa ukoloni wa Mwingereza chini ya Rhodes Smith kimeripotiwa kuwa na mgogoro uliotuama kwenye shutuma za upendeleo wa wazi unaofanywa na Raisi Robert Mugabe.
Shutuma za upendeleo wa makundi 'fulani' pamoja na shutuma za ubaguzi wa kikabila unaoigawa nchi hiyo kwenye makundi makubwa mawili ya Washona na Matebele umechukua sura mpya baada ya Raisi Mugabe kumtunuku Mkewe Bi Grace Mugabe nafasi ya juu ya uongozi ndani ya ZANU-PF. Ripoti zinaarifu kwamba, uteuzi wa Bi Grace kuchukua nafasi hiyo haukuzingatia endapo anazo sifa muafaka kwa nafasi hiyo, bali umezingatia ukaribu wake na mkuu wa nchi. Matokeo ya upendeleo huu ni kuibuka kwa makundi yanayohasimiana wazi wazi ndani ya ZANU-PF kiasi kwamba Raisi wa Zimbabwe,Bw Mugabe ambaye pia ni mwenyekiti wa ZANU-PF ameingiwa hofu kuu.
Swali linalobakia kwetu Tanzania kama moja ya nchi za SADC ni je, shutuma za viongozi waandamizi wa CCM kuwagawa nafasi za uongozi kwa ndugu, jamaa na marafiki zao wasio na sifa stahili za vigezo muafaka zinahatarisha umoja wa CCM kwa kiasi gani?
Habari ya Kugawanyika kwa Zanu-PF hii hapa: Mugabe says Zanu PF divided