Mugabe: Sikutegemea kuondolewa madarakani na Mnangagwa

Mugabe: Sikutegemea kuondolewa madarakani na Mnangagwa

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
DOqMQDjUEAA7GEQ.jpg
​

Aliyekua Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amevunja ukimya kwa mara ya kwanza tangu aondolewe Madarakani, amesema kuwa amekua muhanga wa mapinduzi ya kijeshi.

Akiongea na televisheni ya SABC ya Afrika kusini Mugabe amesema kuwa Rais wa sasa Emerson Mnangagwa asingeweza kuingia madarakani bila kutumika kwa jeshi.

Akiwa katika nyumba yake ya kifahari mjini Harare Mugabe amekemea mbinu zilizotumika kumuondoa madarakani.

Amesema alikua tayari kufanya mazungumzo na Rais wa sasa Emerson mnangagwa na angehakikisha mabadiliko ya madaraka ya uhalali na si yale ya kulazimishwa.

Mugabe amesema kuwa Yuko tayari kwa ajili ya Mazugumzo na Mnangagwa ili kulinda katiba yao.

Hakuna uhakika kama rais huyo wa zamani mwenye Umri wa miaka 94 Anataka kurudi madarakani ama la, lakini ni wazi kuwa anadhani amesalitiwa na rais wa sasa Emerson Mnangagwa.

Amesema kuwa hakudhani kama angepoteza imani yake kwa Mnangagwa kwani yeye ndie alimsaidia kuingia serikalini.

''siamini kama yeye Mnangagwa angeweza kuniondoa madaraki , nimemuingiza serikalini, nimemsaidia alipokua jela anataka kunyongwa, sikuwaza kabisa kama siku moja yeye ndio atakua mtu wa kunitoa madarakani''

Aidha Mugabe ameogeza kuwa madaraka ya sasa yameingia kwa njia zisizo halali.

''Lazima tufute aibu hii, ambayo tumejiletea wenyewe, hatuistahili, hatuistahili, hatuistahili , tafadhali hatuistahili kabisa.Tunatakiwa kuwa nchi inayoheshimu katiba, ndio tunaweza kuwa na mapungufu hapa na pale lakini bado lazima tuheshimu sheria.''

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii, baadhi ya wazimbabwe wanashangazwa na mkongwe huyo wa miaka 94, na wengine wanaamini kuwa amepoteza uhalisia kabisa baada ya kuongoza kwa miaka 38 , wakati wake sasa umekwisha.

Chanzo: BBC
 
Mzee yan bado haamin Kama kwel Amekuwa raia WA kawaida
 
March 15, 2018
Harare, Zimbabwe

Robert Mugabe speaks out : called for dialogue and Zimbabwe 'must undo disgrace'. ..a man whom I nurtured (Ermeson Munangangwa) came against me...we prouded ourselves being very democratic. ..

Former Zimbabwean president Robert Mugabe has called for dialogue following the events that led to his resignation last year. He spoke for the first time to the media about his removal from office. Speaking in Harare, the former leader said he's still aggrieved by what transpired last year.


Source : SABC digital news
 
Poor old RGM, amesahau kwamba "kiendacho hurudi"! Au alifikiri Wazim ni malofa wamelala usingizi wa pono?! Wako wengi sana hapa afrika wanaopashwa kuanza kutia maji vichwani wanaofokiri kupewa dhamana ya kuongoza ni kununua nchi mazima!!!!!
 
Back
Top Bottom