Wakuu wanaohoji imani katoliki ni bible au nini jibu jepesi ni kuwa imani katoliki ni katika biblia takatifu pamoja na mapokeo matakatifu.kufafanua kidogo mfano wenzetu waislamu wanaamini ktk kuruani tu sababu wao wanaamini kilishushwa direct na Mungu na kuwaagiza kufata kilichoandikwa mle tu.sisi tunaoamini ktk Yesu hakuacha maagizo yote aliyofanya na kufundisha yaandikwe na waandishi wa biblia hawakuandika biblia kama kitabu cha historia bali kama chemchem ya kuamsha imani vizazi na vizazi na hasa watu wa nyakati za Yesu walipoanza kuisha duniani.kuna mengi hayapo kwenye biblia ni masimulizi ya kweli tunayoamini ambayo kanisa kama lilivyochambua vitabu vya kuwepo ktk biblia ndivyo lilivyochambua mapokeo hayo.Kanisa limepewa funguo na Yesu mwenyewe kufunga na kufungua ya duniani hadi mbinguni hivyo kanisa kwa muongozo wa Roho Mtakatifu wanaweza kufatilia na kumtangaza mtu mtakatifu ili awe mfano kwetu tuliobaki na pia watakatifu wanaweza kutuombea kwa yesu mwenyewe maana wapo pamoja mbinguni.
Kama unaamini mchungaji anaweza kukuombea na ukapona kwa nini usiamini Musa,Eliya,Bikira Maria walio mbinguni ktk hali ya utakatifu washindwe?
Je waliokufa wanaweza kutusaidia tulio hai?
Mhubiri 9:5-6: kwa sababu
walio hai wanajua ya kwamba watakufa;
lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.6. Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.
Ayubu 7:8-9: Jicho lake huyo anionaye halitaniangalia tena,
macho yake yatanielekea lakini sitakuwepo. Kama vile wingu likomavyo na kutoweka,
Ni vivyovivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa.
Waebrania 9:27: Kama Watu walivyowekewa kufa mara moja,
na baada ya kufa hukumu.
Aliye kufa hana kazi nyingine ya kufanya zaidi ya kusubiri hukumu.
Biblia imetuagiza tuombe kwa nani?
Yohana 14:13-14: Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya
Yohana 16:23: Amin, amin nawaambia, Mkimwomba Baba neno lolote kwa jina langu atawapa. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu;ombeni, nanyi mtapewa ili furaha yenu iwe timilifu.
Kwanini Mungu aponye kupitia Watakatifu walio hai na sio wale waliokufa?
Ni agizo la Mungu.
Luka 20:38: Yeye si Mungu wa Wafu bali wa walio hai....
Luka 16:29: ...Walio hai..wanao Musa na Manabii duniani, na wanapaswa wawasikilize wao..Wasipowasikiliza hawatashawishika
hata akifufuliwa aliye kati ya wau..
Kwa maana nyingine, binadamu hana nguvu yeyote,uweza wote upo kwa Mungu, hivyo hakuna kitu kinakachomshinda
Mungu kufanya kupitia Watakatifu waliopo duniani mpaka imlazimu amtafute aliyepo katika wafu amsaidie.
Zaburi 16:3 Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora, hao ndio ninaopendezwa nao......
Marko 16:15-18:...Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio, kwa jina langu watatoa pepo,watasema kwa lugha mpya, watashika nyoka,hata wakila vitu vya kufisha havitawadhuru kabisa,wataweka mikono yao juu ya wagonjwa,nao watapata afya....
...Kimsingi Mafundisho haya ya "walio hai" kumuomba Mungu kupitia "Wafu" sio ya kibiblia..