Mugabe akanusha kufanyiwa upasuaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mugabe akanusha kufanyiwa upasuaji

Discussion in 'International Forum' started by Saint Ivuga, Jan 25, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,382
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Picha AP

  Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe

  Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anasema ripoti kwamba alifanyiwa upasuaji huko Malaysia kwa maneno yake ni uongo mtupu uliosambazwa na vyombo vya habari vinavyodhaminiwa na Magharibi.

  Rais huyo ambaye anatimiza miaka 87 mwezi ujao, alirudi Harare kutoka safari yake nje ya nchi Jumapili.Katika mahojiano na televisheni ya taifa, bwana Mugabe alisema alikuwa kwenye likizo ya mwaka huko Singapore na alikanusha kwamba alikuwa Malaysia.

  Wiki iliyopita, vyanzo vya kidiplomasia huko Zimbabwe na Afrika Kusini vilisema Rais Mugabe alikuwa Malaysia akifanyiwa matibabu ya tatizo la korodani.

  Bwana Mugabe alionekana kuwa salama na anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika-AU huko Addis Ababa nchini Ethiopia baadaye wiki hii.
  Rais pia alisema Jumapili kwamba kama serikali ya Zimbabwe iliyopo madarakani haikubaliani juu ya katiba mpya, ana haki ya kuvunja bunge na kuitisha uchaguzi mpya chini ya mfumo wa zamani.

  Taratibu za kuandika katiba zipo nyuma ya ratiba kwa miezi kadhaa. Rais Mugabe na chama chake cha ZANU-PF kilitia saini ya mkataba wa kushirikiana madaraka mwaka 2008 na Waziri Mkuu, Morgan Tsvangirai, kiongozi wa chama cha Movement for Democratic Change.

  Chini ya vipengele vya mkataba, serikali inaweza kuendelea hadi mwaka 2013. Hata hivyo wengi katika chama cha ZANU-PF wanasema serikali inamaliza maadhimisho ya pili ya muda wake mwezi ujao.

  Bwana Mugabe ameitawala Zimbabwe tangu mwaka 1980, wakati nchi ilipopata uhuru kutoka kwa Mwingereza.
   
 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Dah!!! Huyu mzee naye mbishi kweli naona ameamua kuzungumza on behalf of himself najua hata kama ni kweli amefanyiwa uchunguzi huko hawezi kusema ni kweli
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  87! Ama kweli king'ang'anizi!
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,467
  Likes Received: 4,126
  Trophy Points: 280
  Dah! huyu mzee mtata!!!!
   
 5. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Nadhani ataingia kwenye Guinness book of records
   
 6. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,890
  Likes Received: 997
  Trophy Points: 280
  Our Land Our Sovereignty. Concept of Land and Home. No Land no Home. No Land no Freedom.
   
 7. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2011
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hii ngoma nzito hasa. Nadhani atafia kifuani mwa yule secretary siku za karibuni..
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mwanawasa and Yaradua also used to have their ill-health status as a top national secrets. We all know what happened later. Comes down to that famous swahili saying "Mficha maradhi..."
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  what goes around always comes around. mugabe mwisho wako waja baba
   
Loading...