Ikhtilafu iwe katika matawi lakini sio katika shina. Lakini cha ajabu ikhtilafu hizi ndogo baadhi ya walio na uwezo mdogo wa kufikiri wanayashadadia na kutia tashtiti mpaka kuleta farqa. Ndio maana ulimwenguni fasad imetawala.Al ikhtilafu l ulaamu rahmah
ANATAKA kuchomoa betri ya gari, kaona waislam wametulia kimya anaanza chokochokoMatamshi ya huyu mufti ni kuvunja sheria na katiba ya nchi. Labda kama anadhani ana mamlaka ya kuminya uhuru wa waislam kwa kuiga jinsi vyama vya siasa vinavyodhibitiwa.
BAKWATA wanawaendesha wale wazee vigoigoi ndiyo mzee.ukienda kwenye ofisi zao utawakuta wamechoka kanzu zimetoboka ndio wanavyopenda bakwata.Hiv kwann WAISLAMU wengi waliosoma huwa wanatofautiana na BAKWATA????
Mi sio muislam ila sion tatizo kwa Mufti. Kama alikua na historia mbaya nyuma haimaanishi kwamba hawezi kuwa kiongozi mzuri.Kuna mzee mmoja hapa mtaani alifanya kazi kiwanda cha baskeli pamoja na mufti, alishangaa sana kuona eti amechaguliwa kuwa mufti.
Niliyo hadithiwa nayahifadhi.
Sema Neno Na Roho Zipate KuponaKuna mzee mmoja hapa mtaani alifanya kazi kiwanda cha baskeli pamoja na mufti, alishangaa sana kuona eti amechaguliwa kuwa mufti.
Niliyo hadithiwa nayahifadhi.
Al ikhtilafu l ulaamu rahmah
Mi napita tu Wasomi wangu ila mmenifurahisha.🚶♂️ 🚶♂️ 🚶♂️ 🚶♂️ 🚶♂️ 🚶♂️Wa ikhtilaafu al juhalaa nakmah.
Kuna sifa mtu akiwa nazo hafai kuwa Kiongozi au hafai kwenye nafasi Fulani,Mi sio muislam ila sion tatizo kwa Mufti. Kama alikua na historia mbaya nyuma haimaanishi kwamba hawezi kuwa kiongozi mzuri.
Kila mtu ana mabaya yake ingawa kuna ambao hayajafahamika ndio maana tunawaona wasafi.
Kama kuna matatizo BAKWATA inabidi yajadiliwe yapatiwe ufumbuzi na sio kuidharau au kuibeza BAKWATA.
Haahaaaahaaaaa...Tarehe 14/10/2019 Bakwata inatimiza Miaka 20 ya Uyatima
Naomba ufafanuzi zaidi na wala siyo namvunjia adabu Mufti....
Je itakuwa sawa kwa Ansar Sunna kufunga au kuswali kwa kufuata mwezi wa kimataifa
Vipi kuhusu hawa Ibadhi hawafungi mikono wakati wa swala
Shia wanachanganya swala nao pia itakuwaje
Mbona hatuna hata Sheikh mmoja wa Mkoa Mshia au Bohora
Mbona watendaji woote wa Bakwata ni wa dhehebu moja tu...
Tushikane na kamba ya ALLAH na wala tusifarakane na tuendelee kumcha ALLAH kwa kumtwii na pia kumtwii Mtume wake (SAW) na walioko kwenye Mamlaka
Iacheni BAKWATA, kaendelezeni harakati zenu na vitaasisi vyenu huko mitaani. Sisi Waislam tunaitambua BAKWATA kama Baraza letu linalosimamia maslahi ya Waislam wote nchini bila kujali itikadi zetu. Kama kuna mapungufu ni issue ya kuzungumza na kuyarekebisha na siyo kukebehi.
Mwanasiasa tu huyu.... Kama Pengo.
Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakary Zuberi amesema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania halitavumilia tena kunyanyaswa, kuvunjiwa heshima au kuvunjiwa adabu na mtu yeyote.
Shehe Mkuu amesema, Bakwata haitaacha uislamu uchezewe na amewaomba mashehe, maimamu na maustaadhi waheshimu mamlaka na wawe watiifu kwa viongozi.
Amewataka Waislamu warudi kwenye mstari, wajenge mshikamano na amani, wajitambue, wabadilike, waache mazoea na kwamba, amewasamehe waliosema mabaya kuhusu Bakwata.
Ameomba Serikali ielewe kwamba, kwenye masuala ya Waislamu nchini wa kusikilizwa ni Bakwata na kwamba, baraza hilo linasema vitu sahihi kwa mujibu wa Katiba kwa kuwawakilisha Waislamu Tanzania.
“Haivumilii tena kama ilivyokuwa zamani, nikisema haivumilii tena kila mmoja atakuwa na tafsiri yake…hatuvumilii tena, lazima tuhakikishe kwamba Waislamu wanaelewa, na naomba Serikali inielewe wakati nazungumza mambo haya, mnielewe nazungumza kitu gani” amesema.
Ametoa mwito kwa Waislamu Tanzania wazidishe mshikamano, umoja, upendo, watengeneze utaratibu wa maendeleo na kuhimiza waumini mambo ya uchumi na kuwasaidia wenye shida wakiwemo wajane na yatima.
Hiv kwann WAISLAMU wengi waliosoma huwa wanatofautiana na BAKWATA????
Tatizo la BAKWATA lina umri wa miaka 50 sasa na ni muhimu kujua historia yake.