Mufti wa Tanzania: Bakwata haitavumilia kuvunjiwa heshima wala kunyanyaswa

miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Messages
2,102
Points
2,000
miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined May 18, 2014
2,102 2,000

Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakary Zuberi amesema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania halitavumilia tena kunyanyaswa, kuvunjiwa heshima au kuvunjiwa adabu na mtu yeyote.

Shehe Mkuu amesema, Bakwata haitaacha uislamu uchezewe na amewaomba mashehe, maimamu na maustaadhi waheshimu mamlaka na wawe watiifu kwa viongozi.

Amewataka Waislamu warudi kwenye mstari, wajenge mshikamano na amani, wajitambue, wabadilike, waache mazoea na kwamba, amewasamehe waliosema mabaya kuhusu Bakwata.

Ameomba Serikali ielewe kwamba, kwenye masuala ya Waislamu nchini wa kusikilizwa ni Bakwata na kwamba, baraza hilo linasema vitu sahihi kwa mujibu wa Katiba kwa kuwawakilisha Waislamu Tanzania.

“Haivumilii tena kama ilivyokuwa zamani, nikisema haivumilii tena kila mmoja atakuwa na tafsiri yake…hatuvumilii tena, lazima tuhakikishe kwamba Waislamu wanaelewa, na naomba Serikali inielewe wakati nazungumza mambo haya, mnielewe nazungumza kitu gani” amesema.

Ametoa mwito kwa Waislamu Tanzania wazidishe mshikamano, umoja, upendo, watengeneze utaratibu wa maendeleo na kuhimiza waumini mambo ya uchumi na kuwasaidia wenye shida wakiwemo wajane na yatima.
 
B

Beem

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Messages
1,358
Points
2,000
B

Beem

JF-Expert Member
Joined May 18, 2018
1,358 2,000
Japo sijamuelewa vizuri lakini naamini alichoongea kinaendana na Serikali maana kinyume na hapo hiyo nafasi ataiacha muda si mrefu. Yupo yule anayeitwa Sheikh wa Dar anayependa kujipeleka kwenye mikutano ya kisiasa na matamasha ya wasanii ni muda mrefu anaivizia hiyo nafasi hata Sheikh Mkuu analitambua hilo.
 
Mzito Kabwela

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Messages
17,942
Points
2,000
Mzito Kabwela

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2009
17,942 2,000
Japi sijamuelewa vizuru lakini naamini alichoongea kinaendana na Serikali maana kinyume na hapo hiyo nafasi ataiacha muda si mrefu. Yupo yule anayeitwa Sheikh wa Dar anayependa kujipeleka kwenye mikutano ya kisiasa na matamasha ya wasanii ni muda mrefu anaivizia hiyo nafasi hata Sheikh Mkuu analitambua hilo.
Anaroga kila siku mwenzie yamkute ya Gorogosi ila tatizo mzee baba naye yuko fit
 
pureView Zeiss

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2016
Messages
2,653
Points
2,000
pureView Zeiss

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Joined Sep 5, 2016
2,653 2,000
Kazi kubwa ya viongozi wa dini kuvumiliana iweje huyu sheikh anakuja na vitisho? Hizi ni kauli za vitisho dhidi ya wakosoaji...
Watu waliwakosoa manabii na matume sembuse yeye? Ukiwanyamazisha waislamu basi utakuwa umenyamazisha jamii mzima kitu ambacho hakitawezekana
 
Faru Kabula

Faru Kabula

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Messages
11,964
Points
2,000
Faru Kabula

Faru Kabula

JF-Expert Member
Joined Mar 26, 2009
11,964 2,000
...Shehe Mkuu amesema, Bakwata haitaacha uislamu uchezewe na amewaomba mashehe, maimamu na maustaadhi waheshimu mamlaka na wawe watiifu kwa viongozi.
...“Haivumilii tena kama ilivyokuwa zamani, nikisema haivumilii tena kila mmoja atakuwa na tafsiri yake…hatuvumilii tena, lazima tuhakikishe kwamba Waislamu wanaelewa, na naomba Serikali inielewe wakati nazungumza mambo haya, mnielewe nazungumza kitu gani” amesema.
Kila mtu ana tafsiri yake kama alivyosema, ila kuitaka serikali imuelewe, tafsiri yangu ni kwamba serikali ishiriki katika kuwadhibiti watakaoshindwa kuiheshimu BAKWATA
 
titimunda

titimunda

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2014
Messages
7,632
Points
2,000
titimunda

titimunda

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2014
7,632 2,000
Anaroga kila siku mwenzie yamkute ya Gorogosi ila tatizo mzee baba naye yuko fit
Huyo mufti yuko fit kweli kweli kwenye ulozi,nyumba anayoishi ilipokamilika walikuwa wanapishana washirikina wenzie kutoka kila pande kuja kuiwekea kinga.

Bakwata ni chombo cha serikali na hakuna muislamu yoyote anayejitambua anayeweza kuwachukulia siriaz.
 
mwanadome

mwanadome

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Messages
3,880
Points
2,000
mwanadome

mwanadome

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2015
3,880 2,000
Kuna mzee mmoja hapa mtaani alifanya kazi kiwanda cha baskeli pamoja na mufti, alishangaa sana kuona eti amechaguliwa kuwa mufti.

Niliyo hadithiwa nayahifadhi.
 
T

Trillion

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2018
Messages
242
Points
1,000
T

Trillion

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2018
242 1,000
Mtumeee..! Muft anaongea kama Magufuli au wakuu wa mikoa.
Unaweza sema kiongozi wa BAKWATA kaandikiwa hotuba na BASHITE.
Sasa ni mwendo wa kupotea ukikosoa BAKWATA.

Nchi imejamba hii tena shuzi mtengua udhu kabisa.
 
Prisoner of hope

Prisoner of hope

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2017
Messages
2,237
Points
2,000
Prisoner of hope

Prisoner of hope

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2017
2,237 2,000
Haya tumekuelewa Muft...
 
D2050

D2050

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Messages
1,604
Points
1,500
D2050

D2050

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2013
1,604 1,500
Bakwata ni taasisi iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria za nchini tanzania inakatiba yake na miongozo yake juu ya uendeshaji dini ya uislam.nchi yetu inaruhusu uhuru wa kuabudu kwa kila raia wake ilimladi hauvunji sheria za nchi.

BAKWATA siyo UISLAM bakwata ni taasisi kama zilivyo taasisi nyingine za ALHIKMA,ANSARI SUNNA.SALAFY.ISLAMIC F.hizi taasisi zote zina waislam wanaowaongoza kwa taratibu wanazozifaham wao kwa elimu waliyokuwa nayo.Bakwata wanapoendesha shughur zao waendeshe wanavyotaka wao tumewaacha na misikiti yao na madrasa zao

inaumiza sana kuona chombo kilichokuwa cha mwanzo hapa tanzania kusajiliwa leo hakina maendeleo yoyote zaidi ya kutumika kuudumaza uislam kilal kukicha.hatufurahi kuona waislam tumeshindwa kuwa na hospitar zetu zinazoendeshwa kwa taratibu za dini.tumeshindwa kuwalipa mishahara walimu wa madrasa zetu.tumekalia kuangalia suruali fupi na ndefu,mfuga ndevu na asiyefuga ndevu,kaswali leo iddi ataswali kesho idi.Bakwata fanyeni yenu nasisi tunafanya yetu hatupaswi kukaa majukwaani na kulishiana vitisho
 

Forum statistics

Threads 1,326,245
Members 509,448
Posts 32,215,659
Top