Mufti wa Tanzania: Bakwata haitavumilia kuvunjiwa heshima wala kunyanyaswa

Al ikhtilafu l ulaamu rahmah
Ikhtilafu iwe katika matawi lakini sio katika shina. Lakini cha ajabu ikhtilafu hizi ndogo baadhi ya walio na uwezo mdogo wa kufikiri wanayashadadia na kutia tashtiti mpaka kuleta farqa. Ndio maana ulimwenguni fasad imetawala.
 
Naomba ufafanuzi zaidi na wala siyo namvunjia adabu Mufti....
Je itakuwa sawa kwa Ansar Sunna kufunga au kuswali kwa kufuata mwezi wa kimataifa
Vipi kuhusu hawa Ibadhi hawafungi mikono wakati wa swala
Shia wanachanganya swala nao pia itakuwaje
Mbona hatuna hata Sheikh mmoja wa Mkoa Mshia au Bohora
Mbona watendaji woote wa Bakwata ni wa dhehebu moja tu...
Tushikane na kamba ya ALLAH na wala tusifarakane na tuendelee kumcha ALLAH kwa kumtwii na pia kumtwii Mtume wake (SAW) na walioko kwenye Mamlaka
 
Matamshi ya huyu mufti ni kuvunja sheria na katiba ya nchi. Labda kama anadhani ana mamlaka ya kuminya uhuru wa waislam kwa kuiga jinsi vyama vya siasa vinavyodhibitiwa.
 
Matamshi ya huyu mufti ni kuvunja sheria na katiba ya nchi. Labda kama anadhani ana mamlaka ya kuminya uhuru wa waislam kwa kuiga jinsi vyama vya siasa vinavyodhibitiwa.
ANATAKA kuchomoa betri ya gari, kaona waislam wametulia kimya anaanza chokochoko
 
Hiv kwann WAISLAMU wengi waliosoma huwa wanatofautiana na BAKWATA????
BAKWATA wanawaendesha wale wazee vigoigoi ndiyo mzee.ukienda kwenye ofisi zao utawakuta wamechoka kanzu zimetoboka ndio wanavyopenda bakwata.
leo unasema unamwezi mwandamo wako ilihali ukienda Makka unafuata mwezi wa huko wakati makka na tanzania hatujapishana hata lisaa
 
Kuna mzee mmoja hapa mtaani alifanya kazi kiwanda cha baskeli pamoja na mufti, alishangaa sana kuona eti amechaguliwa kuwa mufti.

Niliyo hadithiwa nayahifadhi.
Mi sio muislam ila sion tatizo kwa Mufti. Kama alikua na historia mbaya nyuma haimaanishi kwamba hawezi kuwa kiongozi mzuri.
Kila mtu ana mabaya yake ingawa kuna ambao hayajafahamika ndio maana tunawaona wasafi.
Kama kuna matatizo BAKWATA inabidi yajadiliwe yapatiwe ufumbuzi na sio kuidharau au kuibeza BAKWATA.
 
Kuna mzee mmoja hapa mtaani alifanya kazi kiwanda cha baskeli pamoja na mufti, alishangaa sana kuona eti amechaguliwa kuwa mufti.

Niliyo hadithiwa nayahifadhi.
Sema Neno Na Roho Zipate Kupona
Itapendeza Ukitiririka Hapa Ama Kufungua Thread Kwaajili Ya Kiongozi Huyo
 
Mi sio muislam ila sion tatizo kwa Mufti. Kama alikua na historia mbaya nyuma haimaanishi kwamba hawezi kuwa kiongozi mzuri.
Kila mtu ana mabaya yake ingawa kuna ambao hayajafahamika ndio maana tunawaona wasafi.
Kama kuna matatizo BAKWATA inabidi yajadiliwe yapatiwe ufumbuzi na sio kuidharau au kuibeza BAKWATA.
Kuna sifa mtu akiwa nazo hafai kuwa Kiongozi au hafai kwenye nafasi Fulani,
Mfano kama mtu alikuwa shoga huyo hafai kuwa Mkuu wa Majeshi vilevile
Mchawi hafai kuwa kiongozi wa dini. Sina maana kuwa najua lolote kuhusu Mufti.
 
Iacheni BAKWATA, kaendelezeni harakati zenu na vitaasisi vyenu huko mitaani. Sisi Waislam tunaitambua BAKWATA kama Baraza letu linalosimamia maslahi ya Waislam wote nchini bila kujali itikadi zetu. Kama kuna mapungufu ni issue ya kuzungumza na kuyarekebisha na siyo kukebehi.
 
Naomba ufafanuzi zaidi na wala siyo namvunjia adabu Mufti....
Je itakuwa sawa kwa Ansar Sunna kufunga au kuswali kwa kufuata mwezi wa kimataifa
Vipi kuhusu hawa Ibadhi hawafungi mikono wakati wa swala
Shia wanachanganya swala nao pia itakuwaje
Mbona hatuna hata Sheikh mmoja wa Mkoa Mshia au Bohora
Mbona watendaji woote wa Bakwata ni wa dhehebu moja tu...
Tushikane na kamba ya ALLAH na wala tusifarakane na tuendelee kumcha ALLAH kwa kumtwii na pia kumtwii Mtume wake (SAW) na walioko kwenye Mamlaka

swali lako la kwanza kama mwezi umeoneka sehemu yoyote wanaruhusiwa kufunga au kufungua sio bakwata wanavyotaka wao kufungua mpaka rais au waziri awe na nafasi ya kuhudhuria sherehe ya eid ndio wapange. swali la pili kufunga mkono na kufungua hakuna tatizo lolote hata ansar sunna anaweza kufungua mikono na sala ikawa ipo pale pale.swali la tatu shia wanachanganya swala, ndugu yangu shia hawapo katika uislamu wao na makatoliki wapo sawa . mfano huwezi wewe umtukane mke wa rais makufuli halafu rais makufuli akupende sio rahisi. mashia wanamtukana mke wa mtume bibi aisha halafu vipi wawe kipenzi wa mtume wanawatukana maswahaba marafiki wa mtume vipi wawe waislamu unaweza ukatamka ashhadu leo kesho bila wewe kujua ukawa kafiri kwa maneno yako na matendo yako. pia hatuwezi kuongozwa na mshia au bohora maana hao wawili wanafanana tabia zao
 
Iacheni BAKWATA, kaendelezeni harakati zenu na vitaasisi vyenu huko mitaani. Sisi Waislam tunaitambua BAKWATA kama Baraza letu linalosimamia maslahi ya Waislam wote nchini bila kujali itikadi zetu. Kama kuna mapungufu ni issue ya kuzungumza na kuyarekebisha na siyo kukebehi.

mpigaji huyu anasapoti bakwata mlaji
 
Picha

Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakary Zuberi amesema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania halitavumilia tena kunyanyaswa, kuvunjiwa heshima au kuvunjiwa adabu na mtu yeyote.

Shehe Mkuu amesema, Bakwata haitaacha uislamu uchezewe na amewaomba mashehe, maimamu na maustaadhi waheshimu mamlaka na wawe watiifu kwa viongozi.

Amewataka Waislamu warudi kwenye mstari, wajenge mshikamano na amani, wajitambue, wabadilike, waache mazoea na kwamba, amewasamehe waliosema mabaya kuhusu Bakwata.

Ameomba Serikali ielewe kwamba, kwenye masuala ya Waislamu nchini wa kusikilizwa ni Bakwata na kwamba, baraza hilo linasema vitu sahihi kwa mujibu wa Katiba kwa kuwawakilisha Waislamu Tanzania.

“Haivumilii tena kama ilivyokuwa zamani, nikisema haivumilii tena kila mmoja atakuwa na tafsiri yake…hatuvumilii tena, lazima tuhakikishe kwamba Waislamu wanaelewa, na naomba Serikali inielewe wakati nazungumza mambo haya, mnielewe nazungumza kitu gani” amesema.

Ametoa mwito kwa Waislamu Tanzania wazidishe mshikamano, umoja, upendo, watengeneze utaratibu wa maendeleo na kuhimiza waumini mambo ya uchumi na kuwasaidia wenye shida wakiwemo wajane na yatima.
Mwanasiasa tu huyu.... Kama Pengo.

Why biting about the Bush...!?
 
Mtu amkumbushe Mufti kuwa Masheikh wa Uamsho wako Jela mpaka sasa, kama yeye ni mtetezi wa Waislamu wote amefanya nini hadi sasa kuhakikisha hao masheikh wanatoka?
 
Picha

Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakary Zuberi amesema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania halitavumilia tena kunyanyaswa, kuvunjiwa heshima au kuvunjiwa adabu na mtu yeyote.

Shehe Mkuu amesema, Bakwata haitaacha uislamu uchezewe na amewaomba mashehe, maimamu na maustaadhi waheshimu mamlaka na wawe watiifu kwa viongozi.

Amewataka Waislamu warudi kwenye mstari, wajenge mshikamano na amani, wajitambue, wabadilike, waache mazoea na kwamba, amewasamehe waliosema mabaya kuhusu Bakwata.

Ameomba Serikali ielewe kwamba, kwenye masuala ya Waislamu nchini wa kusikilizwa ni Bakwata na kwamba, baraza hilo linasema vitu sahihi kwa mujibu wa Katiba kwa kuwawakilisha Waislamu Tanzania.

“Haivumilii tena kama ilivyokuwa zamani, nikisema haivumilii tena kila mmoja atakuwa na tafsiri yake…hatuvumilii tena, lazima tuhakikishe kwamba Waislamu wanaelewa, na naomba Serikali inielewe wakati nazungumza mambo haya, mnielewe nazungumza kitu gani” amesema.

Ametoa mwito kwa Waislamu Tanzania wazidishe mshikamano, umoja, upendo, watengeneze utaratibu wa maendeleo na kuhimiza waumini mambo ya uchumi na kuwasaidia wenye shida wakiwemo wajane na yatima.
Tatizo la BAKWATA lina umri wa miaka 50 sasa na ni muhimu kujua historia yake.

Kuna watafiti wawili walioandika historia ya BAKWATA na utafiti wao kuchapwa wa kwanza ni Dr K. Mayanja Kiwanuka, ‘The Politics of Islam in Bukoba District’ (1973) Undergraduate Thesis na mtafiti wa pili ni Mohamed Said ‘Islam and Politics in Tanzania,’ Al Haq International, Karachi, Vol.1/no. 3 August- December, 1993.

Lakini mwaka wa 1989 hii paper ilitolewa Nairobi kwenye Study Circle Conference iliyoandaliwa na King Abdul Aziz University.

Muhimu sana kwa Waislam wakajua sababu zilizopelekea serikali kuivunja EAMWS na kuunda BAKWATA kwani hapa ndipo lilipo tatizo lenyewe na sababu ambazo hadi leo baada ya miaka 50 ya uwepo wa BAKWATA bado BAKWATA haijaweza kukubalika na Waislam.

Inawezekana kabisa Mufti wa hivi sasa ana nia njema ya kuleta umoja wa Waislam wote na hiki ni kitu kizuri lakini umoja huu hauwezi kujengwa juu ya msingi wa historia ya BAKWATA.

Mufti wetu anajitahidi sana lakini kazi hii ni ngumu.

Atakae kujua vizuri historia ya BAKWATA na kwa nini Waislam leo wamejikuta katika haya matatizo ni lazima kwanza aijue historia ya Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na uhusiano wake na EAMWS na matatizo yaliyotokea yaliyosababisha Sheikh Hassan bin Ameir kukamatwa na kufukuzwa Tanzania Bara na EAMWS kupigwa marufuku kuwa si jumuiya halali.

Ikumbukwe kuwa EAMWS ilivunjwa wakati ikiwa inajitayarisha kujenga Chuo Kikuu.

Soma kitabu cha Abdul Sykes kisa kizima kimo mle kwa matukio, tarehe, vyanzo vya taarifa na majina ya wahusika.

Ikawa sasa Waislam wanasema huyu anaewasaidia wanaotaka kuivunja EAMWS nia yake ni kuzuia ujenzi wa Chuo Kikuu na miradi yote ya elimu ili Waislam wabakie nyuma kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni.

Hapa ndipo lilipo tatizo la Waislam na BAKWATA.

Kazi ya mwisho iliyokamilishwa na EAMWS kabla haijapigwa marufuku ni hiyo Shule ya Sekondari ya Kinondoni ilipo ofisi ya Mufti.
 
Back
Top Bottom