Mufti Simba angaka - Azuia misikiti kubeba wanasiasa

Mufti Simba angaka - Azuia misikiti kubeba wanasiasa

Status
Not open for further replies.
Sio misitini tu, hata makanisani na vikundi vya waalimu, wanawake na vijana. Hivi fedha zote hizo anapata wapi?
 
Muogopeni Lowassa jamani. Hizo pesa anapata wapi? Zawadi hizi tuwe makini nazo la sivyo tutazilipa huku tunalia kama mbweha...
 
kuna watu hasa akina mama wanagaiwa pesa eti za mikopo ya akina mama kwenye makundi ila lazima uwe na kadi ya ccm.
Hizi ni miongoni mwa pesa chafu zinalowekwa kwenye omo ili zitakate.Mie nimewashauri wengine wazile tu kama zikiwafikia na hata kama hazitawafikia basi wazifuate
 
Kama lowasa mwizi wa waziwazi nafiri watanzania wamesahau dhambi zake mtu mchafu hata wakimsafisha hatakati hata kidogo huyo mwenyewe dealer of drug watanzania tumemchoka mfugaji huyo, naona baadhi ya vyombo vya habari kavinunua vimsafishe,fisadi mkubwa huyo anataka kuimaliza nchi hi.
 
...Za marafiki zake katika mtandao wao wa wauza unga. Aliombwa atoe list ya majina ya hao marafiki zake na kiasi kilichochangwa na kila mmoja wa hao marafiki zake lakini hadi hii leo anang'aa macho.

Muogopeni Lowassa jamani. Hizo pesa anapata wapi? Zawadi hizi tuwe makini nazo la sivyo tutazilipa huku tunalia kama mbweha...
 
Anatumiwa tu na yeye, watu wameanza kutumia nyumba hizi muda mrefu tu na yeye yupo akiona, sasa leo imemuumaje!
Hapo watu ni lazma tukuhisi unatumika mzee!

hata kama mufti amechelwa lkn hajachelewa sana. 2015 bado. tunaomba na viongozi wengine wa dini wamuiige mufti
 
Mufti ameonyesha leadership.Ni wakati sasa viongozi wa makanisa nao wafuate njia.

Nampongeza kwa msimamo thabiti

Unajua kwa mtazamo wa haraka haraka wandugu hapa kuna kamchezo kametokea................ni kwamba,kuna asilimia kubwa kuwa sheikh wetu hajapenda wenzake wapate bakshishi donge nono halaf yee apigwe msasa,siku zote hizo alikuwa wapi,kaona mambo yamegonga mwamba ndo anajifanya kuongea.

Jitihada zimegonga mwamba thats why ana-blame,hata pia inawezekana ikawa anatumiwa na wapinzani ili kuchafua na kusafisha upande wa wapinzani,asifanye watu hawana akili hiyo ni posho tu imempitia mbali thats why ana-blame wakuu.
 
...Za marafiki zake katika mtandao wao wa wauza unga. Aliombwa atoe list ya majina ya hao marafiki zake na kiasi kilichochangwa na kila mmoja wa hao marafiki zake lakini hadi hii leo anang'aa macho.

Lowassa atatuliza vibaya mno maana huwa hatosheki huyo. Tutapigika sana tu. Ila ndani ya chama la Mgamba kuna dalili watambwaga kama gunia la pamba.
 
Sitaki kuamini Mzee wa BAKWATA amekuwa msahaulifu namna hii, Amesahahu hata hili tukio? si la mwaka jana tu?
images


images
 
Ila sms sent, bakwata pamoja na kuwa tawi la ccm ila chukueni tahadhari na huyu mwizi wa kimataifa low has,maaskofu igeni msimamo wa mufti,timueni lowassa na wanasiasa uchwara wa aina yake
 
1.JPG



[h=2]Wednesday, July 13, 2011
MH. LOWASA AKUTANA NA MUFTI SIMBA; AMWAGA MAMILIONI KWA AJILI YA ELIMU.[/h]Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akimkabidhi fedha Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Issa Shaaban bin Simba kiasi cha sh. milioni 13, kwa ajili ya kusaidia shule ya sekondari ya Edward Lowassa iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Mufti ambaye ni mlezi wa shule hiyo, Shule hiyo inatarajiwa kufunguliwa rasmi mwakani kwa kuanzia na wanafunzi 200 wa kidato cha kwanza, na kwamba fedha hizo zitatumika kukamilisha baadhi ya mambo ya shule hiyo ikiwemo kujenga bweni la watoto 30, choo cha shule, kisima cha maji na shule itajihusisha zaidi kusomesha yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Kulia ni aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana ambaye pia ni mlezi wa shule hiyo.
 
[h=2]Wednesday, April 10, 2013[/h][h=3]Mh. Lowassa atoa msaada wa sh. mil. 5 kwa Baraza la Misikiti Tanzania[/h]

[h=3][/h]

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi msaada wa shilingi mil. 5 kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Sheikh Salum Sung'he kwa ajili ya kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa.Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) wakati wa kukabidhi msaada wa sh. mil 5 kwa Viongozi wa Baraza la Misikiti Tanzana,katika makabidhiano yaliyofanyika leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika mazungumzo na Viongozi wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe (kushoto) na Sheikh Salum Sung'he waliofika ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam kupokea msaada wa shilingi mil. 5 kwa ajili ya kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa.

Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA) ,Sheikh Salum Sung'he akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha) wakati akitoa shukrani zake kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa,mara baada ya kuwakabidhi msaada wa shilingi mil. 5 kwa ajili ya kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa.Makabidhiano hayo yamefanyika leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.

Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA) ,Sheikh Salum Sung'he akikabidhi kwa Mh. Lowassa barua ya shukrani kutoka Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA).Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.​



 
Hivi Lowasa hana aibu ? Kiukweli huyu mufti namkubali sana .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom