Muda umewadia kwa waliojifungua kurejea masomoni

Peter Stephano 809

Senior Member
Feb 29, 2020
120
162
Baada ya kilio cha muda mrefu kuhusu Wanafunzi wa kike kufukuzwa masomoni pindi wanapopata ujauzito hatimae serikali imeridhia kuwarudisha masomoni.

Katika walaka uliotolewa mwezi Novemba mwaka 2021 na aliyekuwa Waziri wa elimu Professa Joyce Ndalichako ukibainisha kuwa wanafunzi wote walio achishwa masomo kwa sababu mbalimbali katika shule za umma sasa watapewa nafasi kurejea masomoni kuanzia mwaka 2022.

Walaka huo naeleza kuwa wanaopaswa kurejea masomoni ni wale walio achishwa masomo kwa sababu mbalimbali kama vile kupata ujauzito, sababu za kiuchumi na kiafya katika kipindi kisichozidi miaka miwili iliyopita.

Wanafunzi walioachishwa masomo kwa makosa ya kinidhamu hawataruhusiwa kurudi masomoni chini ya walaka huu.

Aidha wizara ya elimu inawataka wanafunzi hao kurejea katika shule ambazo walihudhuria hapo awali na kuripoti ili waweze kuanza katika madarasa waliyokuwepo kipindi wanaacha au kuachishwa masomo.

Kadharika walaka huu unatoa fursa kwa wanafunzi wa elimu ya msingi walio shindwa kufaulu katika mtihani wa darasa la saba kurudia mitihani huo kwa utaratibu maalumu kama inavyofanyika kwenye ngazi zingine za elimu ikiwemo elimu ya sekondari.

Hatua hii ni neema kwa wanafunzi wote wenye vigezo vya kurejea masomoni ili waweze kuendelea na masomo katika mwaka wa masomo wa 2022 kwa Kufuata utaratibu uliowekwa na wizara.

Peter Mwaihola kitaaluma ni mwandishi wa habari na mchambuzi wa masuala mbalimbali ya kijamii.

1641871555923.jpg

(Picha kwa hisani ya Mtandao)
 
^Mwalimu, samahani naomba nikanyonyeshe kwanza, then nitarudi kwenye kipindi cha mchana.^

^Mwalimu, samahani, leo ni siku yangu ya kuhudhuria kiliniki.^

^Mwalimu, samahani, mwanangu anaumwa. So, lakini nikampeleke hospital kwanza.^

#Car-taaWar-who-knee!
 
^Mwalimu, samahani naomba nikanyonyeshe kwanza, then nitarudi kwenye kipindi cha mchana.^

^Mwalimu, samahani, leo ni siku yangu ya kuhudhuria kiliniki.^

^Mwalimu, samahani, mwanangu anaumwa. So, lakini nikampeleke hospital kwanza.^

#Car-taaWar-who-knee!
 
Back
Top Bottom