Muda mwingine wanaume kuchapiwa wake zetu tunatakaga wenyewe

Mtanzanyika

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
368
425
Habari wana MMU,

Hili suala nimelifikiria kwa kipindi kirefu sana., naona mifano mingi kupitia kwa marafiki zangu na hata ndugu zangu na watu wangu wa karibu. Unakuta mwanaume upo kwenye mahusiano ya kawaida na msichana bado hamjafunga ndoa alafu migogoro na kuachana mara kwa mara, tena unakuta wewe ndo unaachwa na huyo mwanamke alafu unambembeleza mnarudiana. Mwanamke haonyeshi upendo wowote kwako lakini wewe unaendelea kumpenda na kumjali sana. Hayo yote haujifunzi unaamua kumng'ang'ania na mwisho wa siku mnafunga ndoa.
Hivi mwanamke kama huyo akiwa anakusaliti katika ndoa utamlaumu nani.?
Kuna rafiki yangu wa karibu aliwahi kuoa mwanamke wa aina hiyo, ndoa yao ilidumu kwa miaka 5 tu na mimi nilikuwa best man wake, maana mwisho wa siku ikaja kugundulika hata watoto wawili ambao walikuwa wameshazaa hawakuwa wa kwake.
Wanaume tujifunze jamani tunapochagua mwanamke wa kuishi naye kwa maisha yote, tusiziendekeze akili za nyege wakati wa kuchagua wenzi wa maisha.
 
Mkuu upo sahihi sana, ukilazimisha maji kupanda mlima, madhara yake ni kuachwa mbele ya safari au kufanywa mwanaume bwege sasa maana kila kitu itakuwa yes kuepusha kumkwaza.
 
Kulalamika tu...kulialia tu aah tumechoka sasa. Mtachapiwa tu maana hakuna namna
 
unajua hakuna mtu anayependa tabu ila pale ambapo vitisho vya kuachwa vinapokuja na maumivu yake ila unapolinganisha na uzuri wake au anachokupa ni kizuri kuliko vitisho bora ung'ang'anie tu
 
Habari wana MMU,

Unakuta mwanaume upo kwenye mahusiano ya kawaida na msichana bado hamjafunga ndoa alafu migogoro na kuachana mara kwa mara, tena unakuta wewe ndo unaachwa na huyo mwanamke alafu unambembeleza mnarudiana. Mwanamke haonyeshi upendo wowote kwako lakini wewe unaendelea kumpenda na kumjali sana. Hayo yote haujifunzi unaamua kumng'ang'ania na mwisho wa siku mnafunga ndoa.
Hivi mwanamke kama huyo akiwa anakusaliti katika ndoa utamlaumu nani.?
Hapo kwenye red kunawaathiri wengi sana.
Lakini tunashauriwa tuushinde ubaya kwa wema. Ndo maana mtu hapendwi lakini anamtendea wema huyo mwenzake akiamini kwamba atabadilika, kumbe wapi.
 
Habari wana MMU,

Hili suala nimelifikiria kwa kipindi kirefu sana., naona mifano mingi kupitia kwa marafiki zangu na hata ndugu zangu na watu wangu wa karibu. Unakuta mwanaume upo kwenye mahusiano ya kawaida na msichana bado hamjafunga ndoa alafu migogoro na kuachana mara kwa mara, tena unakuta wewe ndo unaachwa na huyo mwanamke alafu unambembeleza mnarudiana. Mwanamke haonyeshi upendo wowote kwako lakini wewe unaendelea kumpenda na kumjali sana. Hayo yote haujifunzi unaamua kumng'ang'ania na mwisho wa siku mnafunga ndoa.
Hivi mwanamke kama huyo akiwa anakusaliti katika ndoa utamlaumu nani.?
Kuna rafiki yangu wa karibu aliwahi kuoa mwanamke wa aina hiyo, ndoa yao ilidumu kwa miaka 5 tu na mimi nilikuwa best man wake, maana mwisho wa siku ikaja kugundulika hata watoto wawili ambao walikuwa wameshazaa hawakuwa wa kwake.
Wanaume tujifunze jamani tunapochagua mwanamke wa kuishi naye kwa maisha yote, tusiziendekeze akili za nyege wakati wa kuchagua wenzi wa maisha.
Hii mara nyingi inachangiwa na kuoa wanawake kwa kutaka kusifiwa,unakuta mwanamke hakutaki lakini wewe unalazimisha kumuoa kisa mrembo ili usifiwe kuwa umeweka ndani mrembo.
 
Hapo kwenye red kunawaathiri wengi sana.
Lakini tunashauriwa tuushinde ubaya kwa wema. Ndo maana mtu hapendwi lakini anamtendea wema huyo mwenzake akiamini kwamba atabadilika, kumbe wapi.

Sidhani kama huwo msemo una maana hiyo uliyoiandika wewe, hapo maana yake ni kwamba usilipize kisasi bali wewe samehe na endelea na maisha yako lkn haimaanishi kwamba uendelee kuwa mjinga na kutumiwa na mtu ambaye unajua kabisa kwamba hakuzimikiii hapana, hiyo ni tafsiri mbaya ya huwo msemo!
 
Ni aliyeumizwa/kutendwa tu ndo huwa ana ujanja wa kupenda kwa tahadhari ama kutopenda kabisa.
Fact ni kwamba mapenzi hayana formula maalum ya kufuata mkuu.
 
Tatizo kuna wanajifanya wanajua sana kupenda kuliko upendo wenyewe.

Nikiachana na msichana sirudi nyuma. Mbele kwa mbele. Kwanza unaepusha mambo kama Hayo ya kuchapiwa.
 
Sidhani kama huwo msemo una maana hiyo uliyoiandika wewe, hapo maana yake ni kwamba usilipize kisasi bali wewe samehe na endelea na maisha yako lkn haimaanishi kwamba uendelee kuwa mjinga na kutumiwa na mtu ambaye unajua kabisa kwamba hakuzimikiii hapana, hiyo ni tafsiri mbaya ya huwo msemo!
Asante kwa kudadafua.
 
Ukiona demu anatishia muachane piga chini haraka hilo ni jipu
tena bila kuremba nikupiga chini kabisa aise mdau maana wanawake wako wengi ata tukioa kumi kumi kila mwanamme bado kuna wengine watabaki bila kuolewa
 
Wale wanaoa kwa imani ya kutokujachapiwa wanajisumbua bure kwani kuchapiwa hakuna fomula.
Moyo wa mtu kichaka. Ukiamua kuoa wewe oa tu kisha mtunze mke wako na familia kwa kufuata misingi bora.
Kama ni muumini usisahau kumuomba Mwenyezi Mungu akupiganie ili jinamizi kuchapiwa au kuchapa nje lisiingie kwenye ndoa yako.
 
Wa awake wakiamua kufanya hivyo wanaamua tu,wengine hawana shida ya pesa,wala hawana magomvi ila anaamua tu kwa starehe amuonje huyu na yule.
 
Back
Top Bottom