Muchana - Kasie Matata......

Muchana - Kasie Matata......

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,801
Reaction score
43,177
Heri ya mwaka mpya nyote hasa kwa wale ambao sijawatumia jumbe maalum za kuwatakia heri ya mwaka mpya 2018.

Basi mwaka mpya ndo umeanza taratibu tuu bila madoido ya sikuzote ya Kasie, ila......... Niko mahali hapa na niko na mtu......

Hapa mahali hata sijui ni wapi maana kiasi flani network imekata japo nilikuja mwenyewe nikiwa pekeyangu alhamdullah nimekutana na huyu mtu hukuhuku nilipo.

Nilikuwa nimekaa mwenyewe kwenye meza ya watu wawili napata upepo mwanana wa baharini huku naperuzi JF. Baada ya masaa kadhaa na kagiza kuanza kuingia ndo akaja huyu mtu na alipofika mezani akakaa kwenye kiti cha pili kisha akanisabahi na kuniuliza kama anaweza kukaa na mie. Nikatabasamu nikamwambia ok, but at your own bill. Basi waiter akaja, atapata anachohitaji.......

Hadi naandika hapa jamaa yuko so happy kama vile tumefahamiana miaka 5 iliyopita. Hapa tulipo kuna mziki laini unasikika kwa mbali kuongezea burudani kwa wateja, basi zikafululiza nyimbo za bolingo tukawa tunatikisa miguu na mikono huku tunaendelea kuongea na kucheka.
Ulipopigwawimbo wa muchana by kanda bongo man tulinyanyuka kwenye viti vyetu tukaanza kucheza rhumba daaah.......

Basi tuu ila sijui hadi asubuhi itakuweje na hivi leo sina mpango wa kurudi kulala nyumbani, bora wiki hii iishe nirudi kazini looh sio kwa kujilipua huku au sijui ndo nyota ya mahaba....!! hehehee basi ndo mwaka mpya umeanza hivyo.


Tuburudike wote na jiwimbo lililotufanya mie na mtu wangu tukaachia viti kusakata rhumba huku tunapata upepo mwanana wa baharini.

Kama kawaida wale watakao toka kapa, waulize notisi kwa jirani. Masimulizi ya Kasinde ya siku zote.

Kasie Mahabat Matata.
 
Nawaona ujue.
Ila hicho kivazi chako umenoga balaa!
 
Kama kawa kama dawa. Pita ndani ujipatie simu yenye watsap fesibuku na twita kwa garama ya elufu kumi na ine tu. Karibuni sana wateja
 
Nawaona ujue.
Ila hicho kivazi chako umenoga balaa!

Hahahahhahahaaa weweee acha fujo banaa, usije ukaanza kunipiga mipicha buree. Utanifanya nihame hapa tuhamie kiota kingine....

Asante I just put on my sundae best.
 
Kama kawa kama dawa. Pita ndani ujipatie simu yenye watsap fesibuku na twita kwa garama ya elufu kumi na ine tu. Karibuni sana wateja

Hahahahahaa uko vizuri kwwnye kutumia fursa looh.
 
Back
Top Bottom