Muathirika wa Madawa ya kulevya

Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
3,056
5,361
Ndugu wanaboard,

kuna Rafiki yangu katembelewa na rafiki yake kipenzi kutoka bongo kaja hapa Japan kwa ajili ya XMASS. cha kusikitisha huyu jamaa anafika mahali anakuwa kama kavamiwa na mapepo, anafanya vitu vya ajabu ajabu (in 20minutes) then anakuwa tena kawaida kabisa.

Kwa maelezo ya washikaji zake bongo jamaa alikua mkandamizaji maji sana na kuvuta sigara kwa wingi.

swali: Nini dalili za mtu aliyekuwa addicted na madawa ya kulevya au bangi? Je akikosa hayo madawa anakuwa na dalili gani?

Je mtu aliyekuwa addicted na pombe say safari lager akiikosa anakuwaaje?

Ili kumsaidia mtu kama huyu tufanye nini??

yeye mwenyewe hajasema kama aliwahi kutumia hivy vitu lakini tunataka kuona jinsi ya kumsaidia (ila sio kumpatia hivyo vitu tafadhali), je nini kifanyike???

Please only those who can provide the solution are welcome to comment maana ni serious case na tunapenda kupata ufafanuzi. asanteni
 
Sidhani kama ni madawa hayo, at least siyo hard drugs kama heroin,cocaine etc. Mtu ambaye ni addict wa hivyo vitu hawezi kutulia mpaka apate dozi. Mlevi wa bombe anakuwa hana raha tu, kama hajapata naye hawezi kutulia ghafla.

Hujasema anafanya vitu gani vya ajabu? Lakini labda ana matatizo ya akili au chemical imbalance ambavyo vinaweza kusababishwa na vitu vingi. Ni vizuri mumpeleke kwa daktari.
 
Sidhani kama ni madawa hayo, at least siyo hard drugs kama heroin,cocaine etc. Mtu ambaye ni addict wa hivyo vitu hawezi kutulia mpaka apate dozi. Mlevi wa bombe anakuwa hana raha tu, kama hajapata naye hawezi kutulia ghafla.

Hujasema anafanya vitu gani vya ajabu? Lakini labda ana matatizo ya akili au chemical imbalance ambavyo vinaweza kusababishwa na vitu vingi. Ni vizuri mumpeleke kwa daktari.

Huyu ni mtu alikua mzima kabisa tangu utoto wake hakuwahi kufanya lolote la ajabu hata ndugu zake wanashangaa. Mnaweza kua mnaongea ghafla anachukua viatu anaweka mezani, anaweza kuwa anaongea na wewe story tofauti kabisa na mliokuwa mnazungumza dakika moja iliyopita, anatamani kumwaga ana kupasua chochote kilicho mbele yake na au wakati mwingine anakaa kimya tu haongei chochote ukimsemesha hajibu wala hakutazami then mwishowe (baada ya 20minutes) anaweza kusema samahani kama nimewauzi ama anaweza kuuliza mlikuwa mnasema...

Kuhusu kwenda kwa daktary, nadhani walishakwenda sijafahamu outcome yake. Tumeshamuombea sana kama ni mapepo basi yarudi huko yaliko toka lakini bado haijasaidia sana sana sigara havuti tena (alikua anavuta paketi 3 kwa siku) amesema haoni tena kiu ya kuvuta.
 
Kulingana na maelezo yako hapo juu sidhani kama kuna addiction yoyote, it sounds more like a mental health case na ningeshauri mumpeleke akaonwe na daktari haraka kabla madhara hayajawa makubwa.
 
Yawezekana kapigwa kipapai........Tanga kuna maprofesa hodari wa kuagua vipapai vya namna hiyo.Mkimbizeni fasta TA pombe na bwibwihalimfanyi mtu namna hiyo.....
 
Hiyo definitely mental issue, siyo lazima uzaliwe nazo, zinaweza kudevelope ukubwani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom