Muafaka unaponukia macho yote kwa Maalim Seif

Hili la kurudia uchaguzi ni Mbingu na ardhi sitegemei kusikia wala kuona hiki kinafanyika mbele ya chama Tawala!

Mkuu ni kwa kutambua unyeti wa hayo unayoongelea ndiyo maana yakawepo pia haya:

Palipo na nia pana njia.

Kila la kheri kwenu Maalim Seif na Dk. Mwinyi:

1. Duniani pana nobeli inanukia.
2. Akhera pana thawabu kubwa kwenu.
3. Nchini mtakuwa machampioni halisi wa amani na mshikamano wetu.

Eeh mola wetu fukuzilia mbali roho mchafu tokea kwa mzandiki yeyote. Ukayawezeshe haya kutokea ndani siku kadhaa wala si miezi!

Nobeli, thawabu au u championi haviji kirahisi hata kidogo.

Au vipi mkuu?
 
Maridhiano ya nini?
Yaani mmeahindwa uchaguzi halafu kuwe na maridhiano yanayohusu nini hasa??
Maalim ameshakubali kuwa makamu wa kwanza wa Raisi na issue imeishia hapo
 
Ccm watakubali yote isipokuwa kurudia uchaguzi

CCM kurudia uchaguzi hawezi kukubali. Hawa ni wa kuwalazimisha tu.

CCM haongelei maridhiano kwa kupenda.

Anajua kuna wazanzibari wamedhamiria kupata haki yao. Lolote na liwe!

Maalim anaingia kwenye maridhiano haya "this time not from the point of weakness."

Hilo ni wazi.
 
Maridhiano ya nini?
Yaani mmeahindwa uchaguzi halafu kuwe na maridhiano yanayohusu nini hasa??
Maalim ameshakubali kuwa makamu wa kwanza wa Raisi na issue imeishia hapo

Anayeongelea maridhiano humjui?

Aliyetuma mashekhe kuomba mazungumzo humjui?

Unakurupuka tu kama umefurushwa shimoni?
 
Anayeongelea maridhiano humjui?

Aliyekuwa mashekhe kuomba mazungumzo humjui?

Unakurupuka tu kama umefurushwa shimoni?
Hakuna mwana CCM anayezungumzia maridhiano kwasababu hakukuwa na mafarakano!
Hayo maridhiano mnaota ndoto za mchana kweupe!
 
Shart namba 1 ,Ccm hawalitaki

Mkuu inafahamika masharti yote 3 CCM hawayataki.

Karata pekee Maalim anayo itakuwa ni kuendelea kukinukisha.

Matatu hayo ndiyo fair yatampa Mwinyi nobeli duniani.

Ikizingatiwa Mungu si Asumani hata uchaguzi kwenye mazingira ya haki, huru na kuaminika bado unaweza kushinda.
 
Yes, mwafaka ni lazima uende na masharti hayo.

Hakuna mwafaka katika mazingira ya kinafiki.

Mtu aliye serious na anataka kutenda haki ili kurekebisha mambo, ni lazima awe tayari ku - sacrifice pride na ego yake...

Wazanzibari, Zanzibar ni yenu. Acheni kusikiliza CCM Tanganyika. Wanawatumia tu kwa manufaa yao. Hawana nia njema na Zanzibar na Wazanzibari kwa jumla..
Dikteta wa Tanganyika hatukubali maridhiano
 
Maridhiano kwani wananchi wa Zanzibar wamemkosea nani?

Wao ndiyo waliopelekewa Jeshi kutoka Tanganyika, na kutendewa kila aina ya unyama bila wao kuwa na hatia yoyote.

Mkuu tulipo inabidi kuanzia mahali. Kwa sasa pa kuanzia ni maridhiano.

Wanasema mwanzo wa ngoma ni lele. Pia mwanzo wa safari ndefu ni ile hatua ya kwanza.

Muhimu hatua hii iwe ya muda mfupi unaofahamika kwa wote.

Kukinukisha ni karata nzito mno kuliko ya US Army combined!
 
Kama CUF walishindwa kuforce uchaguzi wa marudio ulio "huru na haki" mwaka 2015 baada ya kuibiwa live bila chenga, wasitegemee chochote mwaka huu.

CCM hawatokaa warudie uchaguzi wa mwaka huu baada ya kuiba vizuri na kumuachia Maalimu 19% pekee. Kama CUF walishindwa kuforce miaka hiyo Seif anapata 49.01% ya kura, mwaka huu na 19% yake ndio asahau kabisa.
 
Mwisho wa siku muafaka na MARIDHIANO hayaepukiki kwa MUSTAKABALI MWEMA wa taifa kwa kuwa na haya:

1.Pande zote ni lazima ziweke mezani SINTOFAHAMU inayopelekea kuwa na HAMKANI kila Wakati wa UCHAGUZI.
(kutoweka mezani hakutasaidia MARIDHIANO ya kibubusa kwani SINTOFAHAMU hizo zitaendelea kila "kipindi" kikifika.

2.Resolving conflicts na negotiations inataka KILA UPANDE UWEKE WAZI kinagaubaga sababu zinazopelekea HAMKANI HIZO kwa kujicommit kuwa HAZITOREJEA(hapa ndipo ilipo kazi ikiwa hakuna NIA THABITI PANDE ZOTE).
3.Waweke TERMS za kutorudia SINTOFAHAMU hizo na ikiwa zitarejea basi WASABABISHI wachukuliwe LEGAL ACTIONS na indictment Katika mamlaka za sheria ndani na kimataifa.
4.Waweke bayana TERMS za mapinduzi ya Zanzibar...na ikiwa yalikuwa kwa ajili ya RAIA WOTE basi waulizwe wanaopinga,wanapinga kwa Sababu ZIPI...
Na wanaokubali,wamechukua hatua zipi mbaya dhidi ya wale wanaowaona WANAYAPINGA hayo mapinduzi.

Kwani sidhani Kama MAPINDUZI ambayo ni faida ya RAIA WOTE na nchi yao,itokee kundi kubwa la raia hao(half) WAYAKATAE.

Pia je mapinduzi hayo HAYATOI nafasi kwa BAADHI YA KUNDI MOJA KUBWA kunufaika kijamii,kisiasa,kiusalama,kielimu kikazi , na kiuchumi zaidi ya Lile KUNDI jengine KUBWA?

👆👆

Bila ya kufanyika hayo basi utakuwa ni mchezo

Bila ya kufanyika hayo basi utakuwa ni mchezo wa KADENGE na usio na ITHIBATI yoyote kwa watu TIMILIFU VICHWANI....

N.B Karne ya 21 inahitaji AKILI NYINGI NA BUSARA zaidi ya MISULI na jazba.

Muuza Al Kasus

Umemaliza kila kitu mkuu.

Watu kama wewe ulipaswa kuwa miongoni mwa wajumbe upande wa Mwinyi au Maalim kwenye mazungumzo kwa ajili ya maridhiano.

Tatizo waliomo ni design ya kina jingaletu, yefodaya, na yale mengine yanayojiona eti akili kubwa.

Bure kabisa!
 
Anaezungumzia maridhiano ni ccm zanzibar na mbatia akawahoji wengine tunataka kurudia uchaguzi
Anayeongelea maridhiano humjui?

Aliyekuwa mashekhe kuomba mazungumzo humjui?

Unakurupuka tu kama umefurushwa shimoni?
 
Mabibi na mabwana kumekuwa na kauli zenye mantiki tokea kwa Dk. Mwinyi rais wa sasa Zanzibar. Kauli kama hizi:

1. "CCM tuepuke kushangilia kiasi cha kuwaudhi wenzetu."

2. "Niko tayari kwa maridhiano."

Bila ya nyongeza ya neno jingine lolote, hizi ni kauli za msingi sana. Kauli hizi za matumaini, zimemtoka mwenyewe kinywani mwake, akizitoa hadharani.

Kama kuna maneno yoyote mbele au nyuma yanayokwenda na kauli hizo, kwa wazanzibari waliojeruhiwa katika uporwaji ule wa haki, basi hayo na yakachukuliwe kuwa ni mbwembwe na madoido tu ya kiswahili cha mwambao hadi pale itakapothibitika vinginevyo.

Kwake Maalim Seif, maana mfupa huu si wa kiongozi mkuu wa ACT wala mshauri wa ACT (bwana Kamilius aka Kachero Mbobezi).

Macho yote kwake Maalim Seif.

Bottom line:

1. Uchaguzi urudiwe kwenye mazingira huru, haki na yenye kuaminika ndani ya muda unaokubalika.

2. Wahanga wa hujuma za uporwaji ule wanafidiwa kikamilifu.

3. Wahusika wa dhahama lililopelekea wahanga hawa wa hapo #2 wawajibishwe vilivyo.

Palipo na nia pana njia.

Kila la kheri kwenu Maalim Seif na Dk. Mwinyi:

1. Duniani pana nobeli inanukia.
2. Akhera pana thawabu kubwa kwenu.
3. Nchini mtakuwa machampioni halisi wa amani na mshikamano wetu.

Eeh mola wetu fukuzilia mbali roho mchafu tokea kwa mzandiki yeyote. Ukayawezeshe haya kutokea ndani siku kadhaa wala si miezi!
KWA KWELI DR HUSSEIN ALLY MWINYI TUZO YA AMANI YA NOBEL IPO MBELE YAKE ! NAAMINI ATAUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR . MAGUFULI AFUATE NYAYO ZA DR HUSSEIN ALLY MWINYI .
 
Yaani kwa sasa Maalim ni Lulu, mshijeshangaa akapewa ulinzi mkali.. na Mazungumzo ya kisiri yakaanza...aisee !! hii itakuwa kali kuliko ya Lipumba!!
 
KWA KWELI DR HUSSEIN ALLY MWINYI TUZO YA AMANI YA NOBEL IPO MBELE YAKE ! NAAMINI ATAUNDA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR . MAGUFULI AFUATE NYAYO ZA DR HUSSEIN ALLY MWINYI .
Mazungumzo hauatakuwa na maana yoyote ile kama watu wamekufa watu wamekuwa vilema ma wengine wananusuru uhai wao hospitallini.

Tibu mzizi...usitibu shina kiongozi!! Ugonjwa utarudi tu.
 
Umemaliza kila kitu mkuu.

Watu kama wewe ulipaswa kuwa miongoni mwa wajumbe upande wa Mwinyi au Maalim kwenye mazungumzo kwa ajili ya maridhiano.

Tatizo waliomo ni design ya kina jingaletu, yefodaya, na yale mengine yanayojiona eti akili kubwa.

Bure kabisa!
Mkuu wangu....

Mimi ni muumini wa CCM yenye kusimamia misingi mitatu mikuu ya imani zile kuntu zilizoandikwa ndani ya KATIBA YA CCM...

1.Binadamu wote ni Sawa.
2.Kila Mtu Anastahili Heshima ya "kutambuliwa"* na "kuthaminiwa utu wake"*
3."Ujamaa" na "kujitegemea"* ndiyo njia sahihi ya kujenga jamii "huru"na "Sawa"*..

*Misingi Adhimu.

Haijalishi CCM ina wanachama wenye mitizamo GANI....
Haijalishi CCM ina wanachama wanaosimamia MISINGI GANI....

KUBWA ni hizo Imani zake KUNTU NA MARIDHAWA kupita maelezo...

Imani hizo ziko MAKARATASINI na kila mtu ana WAJIBU wa KUZIISHI kwa MUSTAKABALI MPANA WA TAIFA LETU.....

Kwenye MARIDHIANO yoyote yale ni lazima kuwepo na *a WIN WIN SITUATION" na hapa ndipo ilipo NGONDO kwa baadhi ya watu.....

Ustaarabu wa majadiliano Ni lazima uongozwe na hiyo WIN WIN SITUATION bila kujalisha WAFANYA MARIDHIANO ni "wahafidhina", "wana mamboleo", "Misimamo ya kati na kadiri", "wajinga","wenye maono" ,"wasio na maono","wenye weledi","wasio nao" n.k.

Shuleni tulikwenda kufundishwa USTAARABU na baba wa taifa akatuasa juu ya MAADUI WETU WAKUU....(UJINGA MARADHI NA UMASKINI).

Mkuu wangu japo mimi bado ni kijana mdogo,ila nikipata hiyo FURSA ya kuwepo MAJADILIONI nitakwenda bila ya KUSITA 😂😂😂

Nakumbuka kipindi pale MAKAONI alipokuwa "anachinjwa" mh.Lowassa 7/2015, mimi ndiye niliyekuwa na KIPAZA SAUTI pale nje ya MAKAO MAKUU YA CHAMA(white house) Katika ile Barabara ITENGANISHAYO Nyerere Square na KITUO CHA MAFUTA....sikujali SWAUMU niliyokuwa nayo kipindi kile cha MFUNGO,niliwaongoza VIJANA wenzangu kutoa MATAMKO na kuhanikiza NYIMBO za kuilinda KATIBA YETU YA CCM kwa kumhoji mh.mwenyekiti Kikwete(kivifungu vya katiba)...ya kwamba,je ndani ya KATIBA ya CCM kuna kipengele cha KUKATA majina ya WATIA NIA YA URAIS yakiwa Katika KAMATI ya MAADILI bila ya KUWEKEWA "maksi" na kupelekwa majina yao NEC kwa ajili ya KUYACHAMBUA?!!!

Alhamdulillah sikupigwa wala kuvunjwa Miguu na ASKARI waliokuwa wamejazana pale nje ya uzio zaidi ya sisi kutomzuia LOWASSA "asichinjwe" lakini KAMA VIJANA tulitimiza WAJIBU WETU wa kufikisha UJUMBE KWA CHAMA CHETU PENDWA japo tulionekana WABAYA,TUSIOTII na hata kutumiwa na Lowassa....

👆👆
Hayo YAMESHAPITA.......

Mkuu ni wajibu wetu kuifanya TANZANIA BORA na hata CCM yetu kuwa KUNTU sawasawa na MALENGO YA KUANZISHWA kwake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom