Muafaka CUF na CCM Zanzibar, Kulikoni!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muafaka CUF na CCM Zanzibar, Kulikoni!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msandawe Halisi, Jan 13, 2011.

 1. Msandawe Halisi

  Msandawe Halisi JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Binafsi! Siungi mkono muafaka wa Cuf & CCM. Sura ya nzima ya sherehe ya mapindunzi jana, imenipa twasira pana juu ya huo muafaka. Sijui wewe mwana JF, Unauanaje Muafaka.
   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Yaani imekupa taswira katika eneo gani hasa, sijakuelewa mantiki ya hii hoja.
  hebu ipambanue kidogo..
   
 3. Msandawe Halisi

  Msandawe Halisi JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Mojawapo ni heshima aliyepewa Seif S Hamad kiitifaki na muheshimiwa Waziri Abood. Amemfanya S S Hamad kuwa chini ya makamu wa pili wa rais wa nzanzibar. Hiyo ni sura ya njee tu, wasiwasi wangu katika dhana nzima ya utendaji.
   
 4. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Kwani ni nani kati ya Seif S Hamad na Balozi Seid Idd aliyetangulia kufika uwanjani?.Kwa kuwa kwenye sherehe za Mapinduzi siku zote
  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hutangulia kufika uwanjani na Rais wa Zanzibar huwa wa Mwisho.

  Hii inaonesha kuwa kiitifaki Kwenye sherehe za Mapinduzi Rais wa Zanzibar huwa na Hadhi zaidi
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ivi wewe umelala ? Unazungumzia muafaka gani ,mbona makabrasha yalishafungwa zamani na sasa watu wanazungumzia mikakati ya kujenga nchi yao ,yaani wamekuacha wewe unahisabu nani kaingia mwanzo na nani kaingia mwisho uwanjani ,sasa kama hujui baada ya Raisi kuingia kuna wananchi kibao waliingia na mbali ya hivyo kuna wengine kati ya hao wananchi waliondoka mwanzo ,pole sana bro.
   
 6. Msandawe Halisi

  Msandawe Halisi JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45

  Bado nimelala, Nikizunduka muhafaka kwishilee. Muafaka bandia. CCM wataongoza kwa upumbafu wa wanasiasa njaa. Kueshimiwa ni haki ya msingi kwa binadamu hasa kwa nafasi yake aliyonayo.
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  hakuna mwafaka wa kichama zanzibar, bali ni mapatano kati ya seif upande mmoja na Amani karume na mama yake kwa upande mwingine. Ili kumwakikishia amani safe heaven akistaafu maana walijua kambi ya bilali ambayo imedhalilishwa sana kipindi cha urais wa Amani ingetawala Zanzibar na hivyo Mama alihofu kuwa wangemfanyizia Amani.

  Ili kutuliza dhoruba ndiyo maana JK aliamua kwa shingo upande kumwondoa Bilali + Nahonda zanzibar.
   
 8. N

  Nonda JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu MH,

  mwanzo wa post yako hapo juu na hitimisho ndio hili hapa,
  "Bado nimelala, Nikizunduka muhafaka kwishilee. Muafaka bandia. CCM wataongoza kwa upumbafu wa wanasiasa njaa. Kueshimiwa ni haki ya msingi kwa binadamu hasa kwa nafasi yake aliyonayo."

  Sasa unataka na sisi tuchangie nini tena?

  Hivi mkuu,hupendi kuona watu wanaishi kwa amani na kushirikiana?
  Ukiwauliza wenyewe Wazenj wanaonaje maisha kabla ya muafaka na leo hii? Natumai utaridhika na majibu yao.

  Wawacheni wazenj wavute pumzi kidogo, wameshagombana sana na pengine wanafahamu sasa kuwa kuna watu huwa hawapendi kuwaona wao wanaacha ugomvi, chuki, vitu vinavyowazuia kupata maendeleo yoyote ya maana.
   
 9. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,660
  Likes Received: 21,879
  Trophy Points: 280
  Ndio mkuu, Hata Shei alipokuwa anatajataja mafanikio yaliyofikiwa na matarajio ya baadae, alikuwa anasisitiza kuwa hizo ni sera za CCM. Jee za CUF zitatekelezwa lini ndani ya huo Mseto? (kama sio mchanyato)
   
 10. N

  Nonda JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Kimsingi anavyosema Shein ni sawa, kuwa chama kinachoshinda nafasi ya mwanzo, au kinachopewa nafasi ya mwanzo na tume ya uchafuzi ndiyo kinatekeleza sera zake, lakini kwa vile tunaelewa kuwa CCM ni "chama kinachojali wananchi" na "chama kistaarabu" basi hawatashindwa kuingiza na kutekeleza michango mizuri au sera za CUF katika utendaji au kutekeleza sera zake.

  Kama umesoma hutuba ya shein ya jana amesema kuwa yeye na makamo wake wote wawili wanafanya kazi vizuri na kwa pamoja. Bila shaka kuna majadiliano na mikakati ya pamoja inayoandaliwa katika kuendesha serikali yao. Hili ndio la msingi, nyimbo nyengine za majukwaani ni kutafuta kuhamasisha base tu ya wahafidhina na wakereketwa wa CCM. Si unazijua siasa za Zenj?
   
Loading...