Muacheni Magufuli afanye kazi

Omuchimati

JF-Expert Member
Aug 23, 2014
427
202
Salamu kwa Watanzania wote natumaini hamjambo na manaendelea na majukumu ya kujenga taifa lenu pasipo kuwa na shaka na mnafanya hivyo kwa moyo mmoja pasipo manung'uniko,kama ndivyo ni vyema na ni vizuri kumshukuru mwenyezi MUNGU anayetupa uhai na pumzi tunaendelea kuishi mpaka leo.

Lakini licha ya salamu zangu na kuwapongezeni kwa kazi nzuri mnayofanya ya kujenga taifa lenu kwa moyo wa uzalendo, nimesikia watu wakilalama haswa walioguswa na mkono wa John Pombe Magufuli wengine wakisema kuwa wameonewa, ufukuzaji wa wa watu wasio waadilifu hafuati utaratibu wa kimaadili, mi nauliza swali ni lini mtu au mtumishi wa umma akashindwa kufanya kazi kwa uadilifu akiwaonea wanyonge au akitumia madaraka alionayo kujinufaisha yeye binafsi na familia yake , huku mamilioni ya watanzania wakilia wakiwa wamekosa madawa hospitalini, mishahara kiduchu, ukosefu wa madawati kwa wanafunzi ambao tunawaita ndio taifa kesho, eti aondolewe kwa staha!!!!!!!! ni staha ya namna gani anapaswa kuonyeshwa mtu muovu wa namna hiyo , asiyewapenda watu wa nchi yake? nasikia mnalia mnasema yatamkuta kama yale yaliomkuta Edward Ngoyai Lowassa, eti kwamba alifanya hivyo aliwaumiza watumishi na ndio maana bunge lilipopata upenyo wa kumuadabisha kulikuwa hakuna huruma.

Mnasema eti walioumizwa nao wanajipanga na mikakati ya kumdhoofisha Rais wetu mpendwa DR. John Pombe Magufuli,sasa mi nawapa tahadhari mjipange sana lakini mwisho wa siku mtajipangua wenyewe,mwacheni Rais wetu afanye kazi, nchi ilikuwa imeoza, au mnasema hivyo kwasababu walipoiba mligawana nao kidogo, saa hivi hata hicho kidogo hakipo, ndipo mnaanza kulalama, acheni nyumba isafishwe ilichafuka kuliko hata jalala, mwacheni Rais wetu afanye kazi, mnaofananisha Rais wetu au Waziri wetu mkuu MHE Kassim Majaliwa na Edward Ngoyai Lowassa hakika mumepotea njia na mnahitaji maombi, kumbuka Lowassa hajawahi kuwa msafi hata siku moja, na wakati lile pigo linamakuta ilikuwa haki yake, that was his fate, because he created it himself,

MWACHENI MAGUFULI AFANYE KAZI.
 
Tunataka Magu amfanyie kazi ras wa jiji LA darisalama pamoja Na wanasheria wake walohujumu uchaguzi wa Meya, bila kumsahau Jecha Salim Jecha, baada ya hapo tutamuacha afanye kazi yake
 
hata huyo kwenye avatar yako unamuaibisha sana toa weka picha ya wadhalimu waccm kama ulie mtaja hapo,huna point
46 at work
 
Tunataka Magu amfanyie kazi ras wa jiji LA darisalama pamoja Na wanasheria wake walohujumu uchaguzi wa Meya, bila kumsahau Jecha Salim Jecha, baada ya hapo tutamuacha afanye kazi yake
usitie shaka hayo yote soon yatabaki historia.
 
unaikosea haki hiyo picha na muhusika mwenyewe anaheshima kubwa sana hapa dunia,wewe jambazi la lumumba huna hadhi yakuweka hiyo picha na kwambia
INGENJA nashukuru kwa matusi yako, lakini nikwambie kitu kimoja siwezi kuacha kuandika ninapoona uovu unaendelea ndani ya taifsa langu,naamini katika maandiko ipo siku watu watanielewa, na kwa upande mwingine matusi yako ni sawa na petrol inayochochea hari na nguvu ya kuendelea sababu naamini umeguswa.
 
Salamu kwa Watanzania wote natumaini hamjambo na manaendelea na majukumu ya kujenga taifa lenu pasipo kuwa na shaka na mnafanya hivyo kwa moyo mmoja pasipo manung'uniko,kama ndivyo ni vyema na ni vizuri kumshukuru mwenyezi MUNGU anayetupa uhai na pumzi tunaendelea kuishi mpaka leo.

Lakini licha ya salamu zangu na kuwapongezeni kwa kazi nzuri mnayofanya ya kujenga taifa lenu kwa moyo wa uzalendo, nimesikia watu wakilalama haswa walioguswa na mkono wa John Pombe Magufuli wengine wakisema kuwa wameonewa, ufukuzaji wa wa watu wasio waadilifu hafuati utaratibu wa kimaadili, mi nauliza swali ni lini mtu au mtumishi wa umma akashindwa kufanya kazi kwa uadilifu akiwaonea wanyonge au akitumia madaraka alionayo kujinufaisha yeye binafsi na familia yake , huku mamilioni ya watanzania wakilia wakiwa wamekosa madawa hospitalini, mishahara kiduchu, ukosefu wa madawati kwa wanafunzi ambao tunawaita ndio taifa kesho, eti aondolewe kwa staha!!!!!!!! ni staha ya namna gani anapaswa kuonyeshwa mtu muovu wa namna hiyo , asiyewapenda watu wa nchi yake? nasikia mnalia mnasema yatamkuta kama yale yaliomkuta Edward Ngoyai Lowassa, eti kwamba alifanya hivyo aliwaumiza watumishi na ndio maana bunge lilipopata upenyo wa kumuadabisha kulikuwa hakuna huruma.

Mnasema eti walioumizwa nao wanajipanga na mikakati ya kumdhoofisha Rais wetu mpendwa DR. John Pombe Magufuli,sasa mi nawapa tahadhari mjipange sana lakini mwisho wa siku mtajipangua wenyewe,mwacheni Rais wetu afanye kazi, nchi ilikuwa imeoza, au mnasema hivyo kwasababu walipoiba mligawana nao kidogo, saa hivi hata hicho kidogo hakipo, ndipo mnaanza kulalama, acheni nyumba isafishwe ilichafuka kuliko hata jalala, mwacheni Rais wetu afanye kazi, mnaofananisha Rais wetu au Waziri wetu mkuu MHE Kassim Majaliwa na Edward Ngoyai Lowassa hakika mumepotea njia na mnahitaji maombi, kumbuka Lowassa hajawahi kuwa msafi hata siku moja, na wakati lile pigo linamakuta ilikuwa haki yake, that was his fate, because he created it himself,

MWACHENI MAGUFULI AFANYE KAZI.
Nakuunga mkono asilimia mia moja!
 
Back
Top Bottom