Mtwara: Vurugu kubwa zazuka, Mahakama, nyumba ya Waziri vimeteketezwa...

Hii nchi inakoelekea nikumbaya zaid ccm na serikali wanatakiwa wajitafakari na wala sikutumia ubabe
 
Sintofahamu bado inazidi kuitesa Mtwara,

Vurugu zimeendelea tangu asubuhi kuanzia saa tatu leo tar 25.01.2013, kituo kimoja cha polisi kimeteketezwa kwa moto, Mwandishi wa Channel Ten amejeruhiwa na polisi na kushonwa nyuzi saba pia gari ya polisi imeharibiwa vibaya kwa mawe.

Hali ni tete sana.

Updates

Nyumba ya Waziri Hawa Ghasia imevunjwa na wananchi pamoja na nyumba ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara.

Pia polisi wameingia kwenye nyumba ya mwanajeshi na kumtoa na kumpa kichapo na kilichotokea ni mjeshi kupiga simu na kuwaita wenzake sasa kinachoendelea ni mpambano kati ya polisi na wanajeshi!

My take:
Huu ndo mwaka wa nguvu za umma?

Naiskitikia Tanzania na watanzania wenzangu,ee mungu tunyooshee mikono sisi waja wako wa Tz
 
Hii nchi kila kukicha kuna vituko na hata maafa vioneshavyo jinsi gani bado tumeshindwa kabisa kutumia Sayansi na Teknolojia katika maisha yetu ya kila siku (ukiondoa matumizi ya simu za mikononi na internet)...

Juzi kwenye issue ya gesi huko Mtwara, gari imechomwa moto kuzuia kuchukuliwa kwa Bibi toka Msimbati...Imesemekana Bibi alitamka kuwa gesi itakuwa maji ikiletwa Dar bila hiari ya wananchi..(imani za uchawiii hizo).

Leo Mh Diwani kazua mengine hadi nyumba zinachomwa...UCHAWI TENA......Safari yetu ya maendeleo kama jamii bado ni ndefu saaaaanaa!!!!!

mambo mengine mkuu SURUMA ukiambiwa yanatokea kwenye dunia ya karne ya 21 huwezi kuamini,ni kama vile jamii hizi still zipo kwenye karne 8 kurudi nyuma,mambo yakipumbavu pumbavu lakini yanapata washabiki wengi tena watu wazima wenye akili zao.
 
Last edited by a moderator:
hii ya polisi dhidi ya wanajeshi ndio patamu hapo.mungu utuepushe na vita kwani naona kila kona nchi moto inawaka mwanza,mtwara,rufiji na morogoro muda si mrefu tutasikia sehemu zingine na bado tunasema tanzania kisiwa cha amani.
 
Wanajamvi kinachotokea leo hii hapa mjini Mtwara ni hatari, ni milipuko mikubwa ya mabomu ya machozi kutoka kwa police na wananchi wanawarushia mawe police.

Chanzo cha mgogoro huu ni imani ya kishirikina, imetokea wanga kukamatwa na kuwekwa ndani ndipo wananchi wakakusanyika kwenda kuwashuhudia.kutokana na mkusanyiko mkubwa wa raia ndipo police wakaanza kutawanya raia kw kutumia mabomu mfululizo,kuvunja milango na kuchukua chochote kitu,kupiga raia na kusababisha uharibifu wa mali za raia.

Unyama huu wa police umewakasirisha wananchi na kuamua kulipa kisasi kwa kuwarushia mawe police. Ifahamike kuwa mabomu na mikikimiki ya raia imeanza tangu asubuhi na hakuna dalili ya ghasia kuisha pia watu ni wengi sn na hatujui giza likiingia ni nini kitaendelea.

JAMANI POLICE WAMEZIDIWA NA WANAJESHI WAMEINGIA MTAANI.

HABARI TULIZO NAZO SASA HIVI NI KUWA, MAHAKAMA IMECHOMWA MOTO, NYUMBA YA RPC IMECHOMWA MOTO, NYUMBA YA HAWA GHASIA IMECHOMWA MOTO, NYUMBA MWENYEKITI WA CCM IMECHOMWA MOTO NA MAPAMBANO YANAENDELEA.

Amini usiamini hali ni tete na mgogoro unakolezwa na gas.
 
Aisee poleni wanamtwara,. Ila hapo kwenye mapigano ya polisi na wanajeshi pamenifurahisha kweli kama movie vile natamani ningekuwepo hapo nishuhudie mpambano.

.
Ka nchi kyetu hakooo kanatumbukia shimoni. Huku Kariakoo nako mgambo wa jiji walikuwa wanazichapa na polisi wa kituo cha msimbazi mchana huu.
Huu utovu wa nidhamu katika majeshi yetu kwa sasa inawazekana kusababishwa na amiri jeshi tulie nae kuwa dhaifu?
.
 
Tumebarikiwa na mungu kwa kupata Rais dhaifu! Aliepalilia udini na utamtafuna kabla hajafa
 
.
Ka nchi kyetu hakooo kanatumbukia shimoni. Huku Kariakoo nako mgambo wa jiji walikuwa wanazichapa na polisi wa kituo cha msimbazi mchana huu.
Huu utovu wa nidhamu katika majeshi yetu kwa sasa inawazekana kusababishwa na amiri jeshi tulie nae kuwa dhaifu?
.
Ni kweli mkuu jamaa ni dhaifu knoma!
 
Back
Top Bottom