Mtwara Tunagombania Kivuli..

Mtwara Tunagombania Kivuli..

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,250
Ndugu zangu,
Mwanafalsafa Jean- Paul Sartre anasema; “ Hell is the other people” – Kwamba jehanam ni wale wengine, anataka pia tukubaliane, kuwa pepo yaweza kuwa ni wale wengine.



Na hakika, tofauti ya mwanadamu na mnyama iko kwenye kufiri. Mnyama anaongozwa na hisia, lakini mwanadamu anapaswa aongozwe na kufikiri. Ndio maana ng’ombe anaweza kumpanda mama yake. Ni hisia tu zitakazoongoza tendo lake.



Hivyo, mwanadamu kwenye mambo ya msingi hapaswi kabisa kuongozwa na hisia ikiwamo ushabiki. Anapaswa kfikiri.


Vinginevyo, ni ukweli, kuwa kijamii, mwanadamu anaweza kuwa kiumbe anayeishi kwenye mahusiano ya kirafiki na kiadui na wenzake. Na katika hilo la uadui, wanadamu, kama ilivyo kwa wanyama, wanaweza kushindania na hata kugombania vingi; iwe fedha, mashamba, wanawake na hata kivuli cha mti.

Ndio, unaweza kabisa kuwakuta wanadamu wawili wanagombania kivuli cha mti, kwamba nani mwenye haki ya kukaa kivulini. Na wanaweza kugombana mpaka akatokea mwendawazimu atakayekuja kuukata na huo mti wenyewe. Na wanadamu hao watabaki wakitazama juani.



Hoja yangu hapa, kuwa lililo la msingi ni kuwa wanadamu tunategemeana. Kwamba panapo kushindania jambo, mwanadamu, tofauti na mnyama, anapaswa kufikiri sana. Atangulize kwanza hekima na busara.


Na kwenye mgogoro wowote ule, mwanadamu ayape mazungumzo nafasi ya pekee katika kufikia muafaka, na si vurugu au mapigano. Kwenye mgogoro, na kwenye kuitafuta amani, panakosekana mazungumzo ina maana ya uwepo wa mazingira ya kuvunjika kwa amani. Hapa Serikali inapaswa iandae haraka mazingira ya mazungumzo katika kuitafuta suluhu.



Ndugu zangu,



Nilikuwa shuleni miaka ile ya 80 pale aliyekuwa Waziri Mkuu, Dr. Salim Ahmed Salim alipotembelea Mtwara na kukutana na umasikini uliomstusha sana. Kule Mtwara Dr. Salim alikutana na Watanzania waliovaa magunia na miguuni hawana hata kandambili. Na kwenye jua kali walijipanga kando ya barabara kumpokea. Kwenye jua kali walikusanyika kumsikiliza Waziri Mkuu wao.



Ni kule Mtwara inasemekana Dr. Salim, kwa mara ya kwanza, alipofikia maamuzi ya kutoa ruhusa ya mitumba kuingizwa nchini. Maana, kulikuwa na Watanzania wengine wengi nje ya Mtwara waliokuwa kwenye hali ya umasikini wa kufikia kuvaa nguo za viraka na kushindwa hata kuvaa viatu vya matairi ya magari.


Tunajifunza nini?



Kwamba ni kweli Mtwara na sehemu nyingine za nchi zimekuwa nyuma sana kimaendeleo. Na leo tunaposikia Mtwara kuna gesi, nakubaliana na Rais Jakaya Kikwete, kuwa gesi hiyo haiwezi kuwa ni ya WanaMtwara tu. Ni gesi ya Watanzania wote.


Ni vema na ni busara, na kwa kuwashirikisha wazee wa Mtwara, kuwa WanaMtwara wakasikilizwa. Kuna ya msingi ambayo WanaMtwara na Serikali wanaweza kukubaliana kwenye meza ya mazungumzo.

Hata kama tunakubaliana, kuwa rasilimali za nchi ziwasaidie pia watu wa eneo inakotoka rasilimali hiyo, lakini kamwe, tusikubaliane na hoja kuwa gesi iliyo Mtwara ni ya WanaMtwara. Kwamba dhahabu ya Geita ni ya watu wa Geita, twiga wa Ruaha ni wa Wahehe na kadhalika. Haya si mawazo mazuri kuyapandikiza katika nchi.



Ni mawazo ya hatari yanayoweza kupandikiza chuki, sit u miongoni mwa wananchi na Serikali, bali hata miongoni mwa wananchi wenyewe wa maeneo tofauti. Ni mawazo yenye kupandikiza pia fikra za kibaguzi.



Na tufikiri hili, je, kama gesi ile iliyopatikana kule Mtwara, Tanzania na Msumbiji nayo ingesema ni ya kwake, WanaMtwara wangesemaje kama watu wa mikoa mingine ya nchi hii nao wangesema wapelekwe wanajeshi wa Kimakonde, Kiyao na Kimakua tu wakambapane na majeshi ya Msumbiji kutetea ‘ Gesi ya Mtwara!’?



Naam, ya kule Mtwara isije ikawa yale yale ya kugombania kivuli.


Maggid Mjengwa,

Iringa,
0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz
 
Umeeleweka mkuu.
Ingawapo wapo watakaokuja kishabiki zaidi.
 
Safi sana mkuu,napenda hoja zenye mashiko sio ushabiki na kufuata upepo.
 
Na hakika, tofauti ya mwanadamu na mnyama iko kwenye kufiri. Mnyama anaongozwa na hisia, lakini mwanadamu anapaswa aongozwe na kufikiri. Ndio maana ng'ombe anaweza kumpanda mama yake. Ni hisia tu zitakazoongoza tendo lake.

Hivyo, mwanadamu kwenye mambo ya msingi hapaswi kabisa kuongozwa na hisia ikiwamo ushabiki. Anapaswa kfikiri.
http://mjengwablog.co.tz/
hapo kwenye red ndicho WanaMtwara wanachokikataa maana watu wanasema hawafikiri. Wakiongea wanasiasa wanasisitiza kuwa ni uchochezi, hawafikiri, watumie busara. Kwa hiyo watumie busara gesi iondoke!? Kwa uelewa wao wanaona hiyo ndio njia sahihi ya kujieleza baada ya kupuuzwa. Kumbuka ni wanasiasa ndio wanaingia mikataba ambapo wataalamu wanachukua nafasi ndogo sana na hao wanasiasa ndio wamaifanya nchi hii katika miaka 50 ya kuwepo kuwa tofauti na Kenya, Uganda, Rwanda nk
Bw. maggid, ungewauliza pia watu wa serikali ni kwa nini waliinflate gharama za mradi huu na wakajibu, naamini wanamtwara wangekaa kimya na kwa amani

 
Sidhani sana kama wana mtwara wanasema hawataki ges itumiwe na watu wengine nje ya mtwara. Nadhani kuna haja ya kufanya utafiti na kuja ni nini hasa wana mtwara wanakitaka. Wakati mwingine tunafanya makosa kuamini au kutegemea mawazo au sweeping statements za wana siasa akiwemo muheshimiwa Rais JK kujudge mambo.
 
nakubaliana na Rais Jakaya Kikwete, kuwa gesi hiyo haiwezi kuwa ni ya WanaMtwara tu. Ni gesi ya Watanzania wote.

Hata kama tunakubaliana, kuwa rasilimali za nchi ziwasaidie pia watu wa eneo inakotoka rasilimali hiyo, lakini kamwe, tusikubaliane na hoja kuwa gesi iliyo Mtwara ni ya WanaMtwara.

acheni upotoshaji na propaganda zisizoenda shule

unajua Dodoma,kagera,manyara,katavi,kigoma n.k wanawaunga mkono wanamtwara,kwa hiyo hawataki kunufaika na gesi kwa sababu itakuwa ya wanamtwara pekee.
 
no ges hawawez wakafaid wana mtwara pekee!watanzania wengine watafaid ges ya mtwara pale ambapo gas ile ita badilishwa kua umeme kwa pale pale mtwara so watanzania wengine watapata electric energy kwa njia ya nguzo!
-ata gesi yote ikitumika pale pale mtwara kwa shuguli za kiuchumi serikal si itakusanya kod na kwa kutumia iyo kod watanzania wengine watapata mgao wao kwenye bajet
 
Sidhani sana kama wana mtwara wanasema hawataki ges itumiwe na watu wengine nje ya mtwara. Nadhani kuna haja ya kufanya utafiti na kuja ni nini hasa wana mtwara wanakitaka. Wakati mwingine tunafanya makosa kuamini au kutegemea mawazo au sweeping statements za wana siasa akiwemo muheshimiwa Rais JK kujudge mambo.
Mkuu. Nadhani hao wanaosema kuwa watu wa Mtwara hawataki gesi isitumike na watu wengine, wanajua fika kuwa hilo si kweli, bali wanasema kwa makusudi tu kupotosha ukweli wa kile watu wa Mtwara wanachokitaka. Wanapotosha usemi huo ili jamii ione kuwa watu wa Mtwara hawana hoja za msingi na ni wachoyo.

Kitu amacho watu wa Mtwara wanachokitaka ni gesi kufuliwa pale pale Mtwara ili kuongeza ufanisi wa kiuchumi wa sehemu hiyo kwa sekta mbalimbali. Hakuania haja ya kujenga bomba la gesi ipelekwe mbali wakati kuna uwezekano wa kufuliwa hapo hapo.
 
no ges hawawez wakafaid wana mtwara pekee!watanzania wengine watafaid ges ya mtwara pale ambapo gas ile ita badilishwa kua umeme kwa pale pale mtwara so watanzania wengine watapata electric energy kwa njia ya nguzo!
-ata gesi yote ikitumika pale pale mtwara kwa shuguli za kiuchumi serikal si itakusanya kod na kwa kutumia iyo kod watanzania wengine watapata mgao wao kwenye bajet

Ukisema watu wa Mtwara wanataka kutumia gesi peke yao unakosea. Wao hawajasema hivyo. Wanachokitaka ni gesi ifuliwe pale kisha matokeo yake kusambazwa nchi nzima. Kusema kuwa waatu wa Mtwara wanataka watumie gesi peke yao ni upotoshaji wa habari!
 
Kibaraka amekuja tena kipotosha. Nani kakuambia wanamtwara wanasema Ges ni yao. Waataka gesi iwanufaishe tena sj kwa mikataba ya siri. Mkuu maneno mengi hayajengisl mshauri mku akae na wanamtwara,midano yako ni kuomba fadhira kwa viongozi wabovuwabovu
 
Na pata wasi wasi kama unaelewa ulicho andika na nakuamini sana kwa uwezo wako wa kueleaw na kuchambua mambo, lakini kwa hili kuna walakini, kwani nani kasema gesi iwe ya wana mtwara tu, kinachopigiwa makele ni kuto kufaidika, na tanzania ya leo wahamiaji wa Dar es salaan ni wengi kuliko wenyeji, kama ilivyo mtwara kunawatu wa makabila tofauti...hivyo kwa vyovyote kusema gesi ni ya wana mtwara ni kuongea hewa.
kwanini hiyo gesi isiwe mtwara ilikupanua shughuri za kimaendeleo za nchi?
na watu wa mtwara wana akili timamu kama walivyo hao wanao ng'ang'ania kila kitu
 
Mjengwa umeeleweka vyema;
Hakika Serikali na viongozi wake hawafikiri; wanatumia spinal code kwenye maamuzi ya mambo magumu; nasisitiza kwamba gesi ya Mtwara ni ya watanzania wote; na kwakuwa Mtwara pia ni Tanzania kuna haja gani ya kuisafirisha hadi Dar? Tafakari.
 
Na pata wasi wasi kama unaelewa ulicho andika na nakuamini sana kwa uwezo wako wa kueleaw na kuchambua mambo, lakini kwa hili kuna walakini, kwani nani kasema gesi iwe ya wana mtwara tu, kinachopigiwa makele ni kuto kufaidika, na tanzania ya leo wahamiaji wa Dar es salaan ni wengi kuliko wenyeji, kama ilivyo mtwara kunawatu wa makabila tofauti...hivyo kwa vyovyote kusema gesi ni ya wana mtwara ni kuongea hewa.
kwanini hiyo gesi isiwe mtwara ilikupanua shughuri za kimaendeleo za nchi?
na watu wa mtwara wana akili timamu kama walivyo hao wanao ng'ang'ania kila kitu

Viongozi wa serikali wamedumaa akili; akili zao zinawatuma kwamba Tanzania ni Dar tu. Mji wenyewe watu wamebanana kama siafu lakini serikali inangang'ania kila kitu kupelekwa dar wakati nchi yetu ina ardhi kubwa tu kufanyia shughuli mbalimbali.
 
Back
Top Bottom