Mu-Israeli
JF-Expert Member
- Mar 21, 2012
- 2,454
- 975
Dar es salaam imeshindikana kuwa hivyo itawezekanaje Mtwara?
Mtwara mwaka 3013
Mwaka 2020 ni miaka 7 kuanzia sasa na pengine sababu iliyokushawishi kudhani hivyo ni ugunduzi wa mafuta ghafi na gesi huko Mtwara.
Nadhani ndoto kama hizo pia walikuwa nazo wananchi wa Mwadui na Shinyanga kwa ujumla wakati tu Almasi ilipogunduliwa huko.
Sio hao tu bali pia wananchi wa Mererani(wakati huo Arusha), Geita na kwingineko kwenye rasilimali madini.
Hivyo kwangu mimi mada hii naiona kama ni ndoto, ukizingatia ya kwamba sio ndoto zote humuitaji muotaji awe amelala.
Pia tutaandama mtatupotezea na kuharibu mazalio ya Samaki nchanga
Siku jua likichomoza magharibi...
Mawazo yako ni mazuri sana ila mipango mingi ya Serikali haifanikiwi kwa kuwa hakuna watu wa kufikiria mbali na kupanga nini kifanyike baada ya miaka kadhaa,wengi hufikiria mipango ya muda mfupi,jiji la Dar es salaam ukiona ramani yake enzi ya mkoloni utaona kuwa walipanga mipango ya muda mrefu tofauti na lilivyo sasa.Itawezekana kwani Mtwara haijajengwa sana, hivyo itapangwa na kujengwa vizuri kwa pesa za gesi na mafuta..
BTW, mnajua kuwa, pamoja na gesi, Mtwara kuna mafuta kibao ...??
Polisi mko wapi? Njooni muone uchochezi wa huyu jamaa.Hii ndio Mtwara ya mwaka 2020..??