Mtwara Mkoa masikini unaoendesha serikali ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtwara Mkoa masikini unaoendesha serikali ya Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AridityIndex, Aug 17, 2011.

 1. A

  AridityIndex Senior Member

  #1
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tangu nikiwa mdogo nilikuwa nikiambiwa mikoa ya kusini hasa mkoa wa Mtwara ni masikini sana, na kutokana na umasikini huo serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania haiwezi kuendeleza kusini kwa kujenga miundo mbinu mbalimbali kama barabara, kupanua bandari, reli, hospitali, Shule pamoja na vyuo vya elimu ya juu, maji na nisharti. Sababu kubwa ni kwamba mkoa huu unachangia kiasi kidogo cha mapato ya serikali. sina hakika sana kama majibu haya yaliyotolewa na wengi yalikuwa ya kweli lakini yalielekea kuwa ya kweli maana yalisemwa na wengi tena wengine wenye nafasi kubwa kubwa kwenye ofisi zao.

  Ahaa!!! leo hii kwa mujibu wa takwimu za TRA "TRA Quaterly Revenue collection 2011_2011". Mkoa wa Mtwara ni wa 7 katika kuchangia kwenye pato la taifa kwa kodi. Kwa lugha nyepesi ndio wanunuzi wakubwa wa mashangingi ya serikali, au ndiyo wachangiaji wakubwa wa mafuta ya Jet stream ahaa na posho za wabunge, looh na posho za vyama vya siasa.

  Swali langu: Imekuwaje mbona hayo maendeleo tuliyonyimwa tangu uhuru kwa kisingizio cha uchangiaji mdogo kwenye pato la taifa hayaletwi
  hivi sasa tunapochangia kwa kiasi kikubwa au vigezo vimebadilika?

  Tafadhali naombeni mchango wenu na ushauri wenu kwetu sisi wana Mtwara.

  Nimeambatanisha jedwali la makusanyo kwa mujibu wa report za TRA: www.tra.go.tz

  [TABLE]
  [TR]
  [TD]Region
  [/TD]
  [TD]Million TShs
  [/TD]
  [TD]Million TShs
  [/TD]
  [TD]Million TShs
  [/TD]
  [TD]Million TShs
  [/TD]
  [TD]Ranking
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [/TD]
  [TD]Direct Tax
  [/TD]
  [TD]Indirect Tax
  [/TD]
  [TD]Customs and Excise
  [/TD]
  [TD]Total
  [/TD]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Ilala
  [/TD]
  [TD] 56,801.9
  [/TD]
  [TD] 32,545.3
  [/TD]
  [TD] -
  [/TD]
  [TD] 89,347.2
  [/TD]
  [TD] 1
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Kinondoni
  [/TD]
  [TD] 32,858.7
  [/TD]
  [TD] 16,414.7
  [/TD]
  [TD] -
  [/TD]
  [TD] 49,273.4
  [/TD]
  [TD] 1
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Temeke
  [/TD]
  [TD] 12,987.0
  [/TD]
  [TD] 10,677.7
  [/TD]
  [TD] -
  [/TD]
  [TD] 23,664.6
  [/TD]
  [TD] 1
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Arusha
  [/TD]
  [TD] 15,101.3
  [/TD]
  [TD] 10,111.9
  [/TD]
  [TD] 9,383.1
  [/TD]
  [TD] 34,596.3
  [/TD]
  [TD] 2
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Coast
  [/TD]
  [TD] 1,478.9
  [/TD]
  [TD] 562.4
  [/TD]
  [TD] 91.1
  [/TD]
  [TD] 2,132.5
  [/TD]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Dodoma
  [/TD]
  [TD] 3,787.6
  [/TD]
  [TD] 1,385.8
  [/TD]
  [TD] 17.5
  [/TD]
  [TD] 5,190.8
  [/TD]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Iringa
  [/TD]
  [TD] 3,471.4
  [/TD]
  [TD] 1,941.9
  [/TD]
  [TD] 20.5
  [/TD]
  [TD] 5,433.9
  [/TD]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Kagera
  [/TD]
  [TD] 967.1
  [/TD]
  [TD] 1,082.9
  [/TD]
  [TD] 1,938.7
  [/TD]
  [TD] 3,988.7
  [/TD]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Kigoma
  [/TD]
  [TD] 694.5
  [/TD]
  [TD] 342.1
  [/TD]
  [TD] 786.5
  [/TD]
  [TD] 1,823.1
  [/TD]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Kilimanjaro
  [/TD]
  [TD] 6,834.2
  [/TD]
  [TD] 2,947.3
  [/TD]
  [TD] 11,389.3
  [/TD]
  [TD] 21,170.8
  [/TD]
  [TD] 3
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Lindi
  [/TD]
  [TD] 284.2
  [/TD]
  [TD] 154.5
  [/TD]
  [TD] 22.9
  [/TD]
  [TD] 461.5
  [/TD]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Mara
  [/TD]
  [TD] 1,264.0
  [/TD]
  [TD] 914.4
  [/TD]
  [TD] 13,882.2
  [/TD]
  [TD] 16,060.7
  [/TD]
  [TD] 4
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Mbeya
  [/TD]
  [TD] 2,605.4
  [/TD]
  [TD] 2,241.0
  [/TD]
  [TD] 7,446.3
  [/TD]
  [TD] 12,292.8
  [/TD]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Morogoro
  [/TD]
  [TD] 5,359.6
  [/TD]
  [TD] 2,427.2
  [/TD]
  [TD] 70.2
  [/TD]
  [TD] 7,857.0
  [/TD]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Mtwara[/TD]
  [TD] 7,608.5 [/TD]
  [TD] 6,838.5 [/TD]
  [TD] 270.4 [/TD]
  [TD] 14,717.4 [/TD]
  [TD] 7
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Mwanza
  [/TD]
  [TD] 8,905.0
  [/TD]
  [TD] 3,889.9
  [/TD]
  [TD] 4,577.3
  [/TD]
  [TD] 17,372.2
  [/TD]
  [TD] 5
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Ruvuma
  [/TD]
  [TD] 667.1
  [/TD]
  [TD] 469.8
  [/TD]
  [TD] 32.7
  [/TD]
  [TD] 1,169.6
  [/TD]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Shinyanga
  [/TD]
  [TD] 1,355.0
  [/TD]
  [TD] 1,068.8
  [/TD]
  [TD] 37.8
  [/TD]
  [TD] 2,461.6
  [/TD]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Singida
  [/TD]
  [TD] 331.0
  [/TD]
  [TD] 269.1
  [/TD]
  [TD] 51.3
  [/TD]
  [TD] 651.4
  [/TD]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Tabora
  [/TD]
  [TD] 1,087.4
  [/TD]
  [TD] 896.2
  [/TD]
  [TD] 15.1
  [/TD]
  [TD] 1,998.7
  [/TD]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Tanga
  [/TD]
  [TD] 2,849.7
  [/TD]
  [TD] 2,231.8
  [/TD]
  [TD] 9,755.7
  [/TD]
  [TD] 14,837.3
  [/TD]
  [TD] 6
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Rukwa
  [/TD]
  [TD] 748.1
  [/TD]
  [TD] 235.4
  [/TD]
  [TD] 97.6
  [/TD]
  [TD] 1,081.2
  [/TD]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Manyara
  [/TD]
  [TD] 686.2
  [/TD]
  [TD] 263.6
  [/TD]
  [TD] -
  [/TD]
  [TD] 949.9
  [/TD]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  mmakone chi ntu....
   
 3. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hahaha...hapo ndio utajua jinsi tulivyo maskini!!
   
 4. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Binafsi sikubaliani kuwa huo ndo utaratibu. Angalia kwa mfano miradi inayoendelea mkoa wa Pwani hlf linganisha na mchango wake. Na mbona mikoa ya kanda ya ziwa wamekuwa wakiambiwa kuwa kidogo kinachopatikana kinagawanywa kuendeleza maeneo yote ya nchi?! Ndo mana sehemu za madini zote huoni unafuu wake... Halafu nikiangalia kwa haraka jedwali uliloweka hapo juu Mtwara inaangukia nafasi ya tisa au zaidi, siyo ya saba...
   
 5. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Ahsante kwa data. Kumbe Arusha ni ya 2 ?
   
 6. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Tunataka yale ya Niger Delta yaje Tanzania.....waache waendelee kutuuuza!
   
 7. Ligogoma

  Ligogoma JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2,133
  Likes Received: 849
  Trophy Points: 280
  Hakuna mkoa ninaousikitikia kama Lindi, mapori yote yale yenye magogo aghali yanakuja kukamatiwa Dar then yanalipiwa Dar wanaweka list ya hayo malipo katika mikoa/wilaya za Dar! Hii mbaya sana, korosho na ufuta vinanunuliwa Lindi, kuna bandari pale lakini cha ajabu wanaenda kulipia Mtwara sababu bandari ya pale ndo angalau inafanya fanya kazi kidogo!! Kwa hiyo takwimu zote zinakwenda Mtwara

  Kuna uvuvi na mbuga ya Selous (kama sijakosea spelling) ambayo kwa asilimia kubwa ipo katika mkoa wa Lindi lakini malipo yanafanyikia Morogoro, Mbeya ama Pwani yaliko mageti ya kuingilia hifadhini Lindi hakuna kitu kama hicho, WHY? Ndo mana utaona mapato yake ni kidogo ila ni mkoa muhimu saaana nchini!!!

  Mimi bado kilio changu kipo kwa sisi wazawa wenyewe wa mikoa ya kusini, tumeitupa mikoa yetu wenyewe!!!! Tatizo letu tukifanikiwa hatukumbuki kwetu, tunakimbilia kuweka miradi na kujenga katika mikoa mingine kabisa na kwetu tunasahau!!!

  Kuna matajiri wakubwa saaana Arusha na Moshi ambao ni watu wa kusini ila hawataki wajulikane hivyo, wanajifanya ni watu wa kaskazini!!! MMoja wao nilikwenda mpaka kijijini kwao Mtwara, sikuamini nilichokiona, ila umkute Moshi au Arusha hiyo miradi yake na nyumba alizonazo si mchezo, mwambie kajenge kwenu mtagombana!!! Na wengi tu wapo hapo Dar, story na kwao hawana wakitaka kwenda vacation wanakimbilia kaskazini!!!
  Wamesahau huko nako kulijengwa na watu wa huko huko na msitegemee wapare au wachaga au wanyakyusa waje wawajengee nyie!!!
   
 8. Ligogoma

  Ligogoma JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2,133
  Likes Received: 849
  Trophy Points: 280
  Tatizo lingine, watu wa kusini ukiacha Wangoni wengi wetu tuna jealous mbaya za kurudishan nyuma wenyewe kwa wenyewe na nime experience hili kwa macho yangu!!! Wenzetu wa Northern (sorry si kwa mazingira ya ubaguzi) wakikutana mahali wanafight wataungana na kuwa kitu kimoja na kufight pamoja!! Na hata wakikutana mahali kwenye issue ya kupata mchongo utawapenda!! Real kutoka moyoni mwangu kwa hilo nawakubali vibaya watu wa Northern!!!

  Wenzetu na sie kwa kupigana chini kwenye michongo utawataka!!! Siop siri na huo ndiyo ukweli halisi na unajulikana waziwazi kuwa utawala wa Mkapa wachaga walimtumia ipasavyo first lady halafu mzee wa nchi (kipindi hicho) akawa anabana mbaya!!! I real hate this man coz aliongeza umasikini mikoa ya kusini!!! Alifanya nini zaidi ya barabara na hata hivyo utawala wake wote mpaka leo haijakamilika!!! Daraja lile ndo linazidi kutuondolea man power kusini na ndo hao wanaishia kuuza maji na mitumba mabarabarani huko Dar na mikoa mingine!!! Na dada zetu kuishia kuwa kina mama lishe na wauza mihogo/matango mabarabarani!!!!

  Nilipograduate, nilisota miaka nne kitaa na vyeti vyangu walionisaidia ni marafiki tu tena Wachaga hahahahaaaaa!!! Niliingia sekta moja hivi mmakonde mwenzangu alinibania mbaya, nilifanya vyema interview but yule jamaa sintokaa nimsahau!!!! Na ndo mana alikufa kifo cha aibu
   
 9. naumbu

  naumbu JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 3,304
  Likes Received: 3,786
  Trophy Points: 280
  We punainem inaelekea mitihan ulikua unafeli kwa kutosoma instructions kwa makin angalia column ya mwisho wameweka rank au hujui maana yake?chingas zenye hela zipo nying dsm esp wenye asil ya asia lkn hawakumbuk kwao akijitambulisha ujue kimaslah zaid kwa mbunge au wazir wa kusin.kila munu ave na kwao jaman
   
 10. l

  lajabell Member

  #10
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  [​IMG]
   
 11. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Dawa ni serikali za majimbo tu ndio zitaondoa huu unyonyaji wa dsm
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kifupi Mtwara ungeweza kufanya vizuri zaidi na Tanga kama inavofanya Dar es salaam. sababu kubwa ni kuwa wao wana bandari.

  kama Tanzania ingeamua kwa dhati kabisa kuzitumia vizuri fursa hizo za bandari za Mtwara na Tanga na kujenga miundo mbinu bora ya barabara basi nafikiri zingeaa juu zaidi katika kuchangia katika pato la taifa lenu ukilinganisha na sasa.

  hakika kupanga ni kuchagua. Umasikini mnajitakia wakti Mola amewajaalia kile ambacho Uganda, malawi, burundi. rwanda na nchi nyingine nyingi hawana
   
 13. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Sie tuliesoma pale saba saba sec. at least ndio tunataka kufabya ka aniversari ka miaka 25 ili tuanze mbinu za kujenga vzr shule yetu. Sisi watu wa kusini tabu sana. hata kukutana tunaogopana
   
 14. A

  AridityIndex Senior Member

  #14
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa mchango wako kutoka huko mferejini maringo
   
 15. A

  AridityIndex Senior Member

  #15
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kivipi mkuu chapakazi unaweza kufafanua kidogo.....ili kuoanisha na kilicholalamikiwa au kuulizwa na mtoa mada.
   
 16. A

  AridityIndex Senior Member

  #16
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  .

  Punainen-red......kwa hukubaliani na huu mtazamo ..yes inawezekana hauko kimaandishi lakini ukawa ndiyo mtazamo (attitude) ya wapanga miradi ya maendeleo. Labla kuhusu miradi ya mkoa wa pwani nadhani hapo unaongezea kwenye swali langu je vile vigezo vya awali vimebadilika na sasa siyo mchango katika pato la serikali tena????.


  Kujibu hoja ya hiyo mikoa mingine kuambiwa kidogo chao kinapelekwa kwingine sina hakika maana.....uliozoeleka ni kwamba mikoa ya kusini ni masikini sana na ni wakusaidiwa lakini ona hizo takwimu kwa hiyo nadhani wahusika waulizwe ni wapi wanazipeleka maana hata kusini wanachukua kingi zaidi na hakuna wanachofanya bandari feki, airport feki, vyuo hakuna, hospitali feki, barabara feki, reli hakuna viwanda vya mbolea, nondo na cement hakuna......hii ilitumika kuombea kura 2010.
   
 17. A

  AridityIndex Senior Member

  #17
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yes, arusha ni ya pili na nimeweka dar kama mkoa mmoja ingawa watu wa TRA wanaigawanya katika mikoa 3; Ilala, Temeke na Kinondoni.
   
 18. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nakusihi uvute subira kwani baada ya mwaka mmoja tu resources za Mafuta na Gesi ndizo zinategemewa kufadhili AHADI NA NGONJERA ZOTE TULIZOSIKIA kipindi cha kampeni iliyopita. Kwa namna hiyo inategemewa kwamba CDM watafungwa migoli ya kisigino come 2015.
  Kwa hiyo, then Mtwara inategemewa kuwa mkombozi. hii ngonjera kanisimulia **** flani akiota mchana kweupeee!
   
 19. A

  AridityIndex Senior Member

  #19
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli Kinyungu jamaa wanapanda magari yao kwenda kujadili tatizo la maji Tandahimba wakati kimsingi wala hawalijuwi hilo eneo lenyewe linaonekanaje ndiyo maana hawatilii mkazo matatizo yetu maana hawakujuwi kwetu na hawajuwi values za natural resources zetu kama bandari, Rufiji basin, ruvuma basin, Gas, Korosho, ufuta, nazi, mihogo nk. leo hii watu wanaimba eti watu wa kusini ni wavivu lakini ukiwauliza ni lini serikali ilipeleka chakula cha msaada hupati jibu. Nikiwa nasoma sekondari tulikuwa tukipewa adhabu ya kufukia maembe ili kusafisha mazingira na hadi leo kule migombani watu wanafukia machungwa kusafisha mazingira. Mihogo tumelazimika kupunguza kasi ya uzalishaji maana ilikuwa ikioza tu hakuna sehemu ya kuuzia barabara ya kutoa bidhaa kusini hakuna bandari haifanyi kazi.
   
 20. A

  AridityIndex Senior Member

  #20
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  .

  Barubaru umenena mambo ya msingi kabisa ni kweli tuna rasilimali nyingi na za maana ambazo hata nchi nyingi za Africa, asia na europe hawana lakini mipango haieleweki bandari ni natural resource mojawapo tu bado tuna gesi, mbuga za wanyama na mazao ya kueleweka ya biashara bila kusahau mito yenye uwezo wa kuzalisha chakula cha kutosha.

  Mbali ya kuwa kupanga ni kuchagua nadhani tuna tatizo la mipango mingi kufanywa kwa upendeleo, nilipokuwa chuoni niliweza kufanya research ya haraka haraka nikagundua zaidi ya 90% ya wanafunzi na wakufunzi pale wametembea karibu mikoa yote isipokuwa Lindi na Mtwara na hao ndiyo wako maofisini leo hii ndiyo tunaowategemea kupanga mipango ya kuliendeleza eneo hili maana ndiyo waliohodhi mamlaka na wanakomba kila kitu kinachopatikana kule kama ulivyoona kwenye hizo takwimu.
   
Loading...