Mtwara, Lindi, Ruvuma _Tukijitenga kisiasa tutaendelea

AridityIndex

Senior Member
Mar 22, 2011
149
38
HESHIMA KWENU WANAJAMVI

Nimefikiri kwa kina kuhusu umasikini wa watu wangu katika mikoa niliitaja hapo juu nimejaribu kuoanisha na rasilimali tulizo nazo.

1.Umeme wa gesi wa uhakika
2.Marine park, Mnazi bay
3.Sellou reserve,
4.Ruvuma river,
5.Hee natural habour Mtwara & Lindi
6. Zao la biashara korosho,ufuta nazi na karanga
7.Zao la chakula la uhakika mihogo
8. Uranium kule Namtumbo
9. Ardhi yenye rutuba ruvuma
10. Bahari kwa ajiri ya uvuvi
11. Closer to land locked countries malawi, zambia
12. Closer to non farming country comoro

Pamoja na rasilimali zote hizi, siasa za Tanzania zimeendelea kulifukarisha eneo letu mbaya zaidi tumeshuhudia wanasiasa wa Tanzania wakijadili kuingiza umeme wetu kwenye grade ya taifa wakati katika eneo letu wanaonufaika na umeme huu hawazidi asilimia 15.

Lakini pia nimeshughudia mijadala ya upanuzi wa bandali ya Dar wakati yetu ikidoda tu tena ina ubora wa asili kuliko hiyo Dar kieneo na kina.

Nimewahi tembelea nchi kama za Asia na nikaona manispaa zaidi ya tatu zenye uchumi imara kwa kutegemea rasilimali za bahari tu yaani Uvuvi na utalii.

hebu check hiyo orodha nadhani mnajua ni jinsi gani vinavyoweza kutuendeleza pindi tukijitenga kisiasa kutoka mikononi mwa Tanzania.

Naombeni michango yenu kimawazo wakati tukiandaa mikakati, ku-implement.
 
huenda pia mkafufua reli iliyojengwa na mjerumani kwenda nachingwea!sijui kwa nini watu wa huko mnawakubali watawala wa ccm wakati wao wanahitaji korosho na gesi yenu tuu!
 
Kujitenga sio suluhisho eneo hilo linatakiwa kuunganishwa kuwa kwenye kanda maalumu ya kiuchumi na pia nyie wenyewe watu wa huko amkeni pelekeni watoto wenu shule , jengeni shule na fanyeni mikakati wa kuleta huduma na biashara maeneo yenu huo ndio uzalendo tena mnaweza hata kuanzisha vyama vya maendeleo kwa ajili ya watu wa huko - mimi sio mkazi wa huko lakini naweza kukusaidia kufanya set up ya vyama na ushawishi wa kupeleka maendeleo maeneo hayo Wanabidii | Google Groups
 
mataifa yanahangaika kujiunga into blocks wewe watuma au wafikiria kujitenga.
siamini kama wewe ni Mtanzania mwenye uchungu na hii nchi.
 
Wanaharakat wazaliwa wa mikoa husika hawataki kuishi kwao ili kuleta mabadiliko na kuondoa u regionalism wanaogopa huko kisa uchawi etii. Mi mwenyewe ni mzaliwa wa Ruvuma(mkoa), mbinga(wilaya), ngumbo(kata), mkili(kjj) lakiní kwa śasa niko mwanza na nmepigania kwa kura yangu 1 hadi Wenje kaiingia madarakani. Ss hatuko kama wa#€aga. Kule ni ccm tu upinzani umebhungulia kabuli, wengi tumewapoteza coz ya siasa.
 
Tuongee kitaifa na sio ki-kanda au kimkoa. Tanganyika ni nchi moja. Kumbuka hata maneno ya hayati baba wa taifa kuhusu zanzibar kujitenga na Tanganyika au Tanganyika kujitenga na zanzibar.
Nchi za ulaya na Marekani tunaona zinaunganisha nguvu ili kumuadhibu Ghaddafi, mtu ambaye hata kwa Marekani yenyewe hafui dafu.
Umoja ni nguvu.
 
" Tatizo la VIRUSI vya ugonjwa wa ubinafsi ni mbaya hata kuliko ukimwi,na unaenea kwa kasi mno, na ni pale tu mtu anapopata mabadiliko ya ghafla ambayo hakuyatarajia hata siku moja. HOJA YAKO KUHUSU RASLIMALI ni nzuri,tatizo lako ni ubinafsi.
Nina imani mkishajitenga,mtaendelea kujitenga hadi utakapobaki wewe peke yako na kaburi,hapo ndio utagundua ubaya wa Virus hii na tayari itakuwa too late kwako.
 
Back
Top Bottom