Mtunzi wa vitabu Joram Kiango

hebu angalia mchakato mzima wa kisheria mkuu,ili hiz movie zichezwe,itakuwa bomba sana na itabamba sana,pamoja na zile movie z willy gamba,inahitajika mapinduzi ya kweli kwenye movie zetu,sio kila siku kina james bond,Hiyo movie ya joram sijaiona bado mkuu
 
Ben Mtobwa, mtunzi wa hadithi za mpelelezi Jorum Kiango hivi sasa ni Marehemu.
The best of Kiango series ni.
1. Malaika wa shetani
2. Salam kutoka kuzimu.
3. Tutarudi na roho zetu?

wazungu waliwahi kutafsiri hicho cha mwisho kwa kiingereza kikaitwa ZERO HOUR
 
Mnamkumbuka na Agoro Anduru na simulizi zake? hahahahaha

Umenikumbusha huyu mwandishi Agoro Anduru! Jina lake halisi ni Aggrey Andrew ila alitaka kuwa more African ndio akajiita Agoro Anduru.
Alitunga hadithi nyingi ila kuna kitabu kimoja kiliniacha hoi kwa hadithi zake tamu, kinaitwa "This is living and other stories!"
 
Mkuu unafikiri ni wasanii gani wa filamu wa hapa bongo wana sifa za kucheza movies za vitabu hivi?

Nitajie majina yao angalau wachache tu.
 
Dah..hawa watunzi.
Tumewapoteza.EDI GANZEL,BEN MTOBWA,A MUSIBA,HAMMIE RAJABU.
Walikua watunzi waukweli wa riwaya.

Hiyo ID yako Elungata inanikumbusha kitabu cha A E Musiba, Kikomo.
 
Last edited by a moderator:
mkuu nadhani bado hawapo,ila kama taratibu zote za kisheria zitafuatwa,watu hao waweza patikana pasi na shaka
Mkuu unafikiri ni wasanii gani wa filamu wa hapa bongo wana sifa za kucheza movies za vitabu hivi?

Nitajie majina yao angalau wachache tu.
 
ndiye huyu aliandika kitabu kiitwacho 'simu ya kifo'?

dah! mkuu sikufanikiwa kabisa kusoma hiki kitabu nilikisikia tu!

vitabu ambavyo siwezi kuvisahau vya enzi nikiwa primary school

hadithi ya allan quatermain na wenzake
mashimo ya mfalme suleiman
unyama wa mafia (part 1 hadi 4... mfano part two, mauaji ya kishenzi...)
mikononi mwa nunda
tutarudi na roho zetu
salam toka kuzim
njama (na vingine vyooote vya willy gamba kama hofu, mkataa pema, n.k)
salome masikini ( riwaya nzuri hata simkumbuki mtunzi )

nilipenda sana vitabu na enzi zile tulikua tunabadilishana vitabu kama tunavopeana muvies kali za siku hizi, at the end unajikuta umesoma vitabu viiiiingi sana!
 

hahaha mkuu Bullet precisely what i was referring to here, kitabu kizuri sana, kile tena sana
 
Mnamkumbuka na Agoro Anduru na simulizi zake? hahahahaha
Yap!

Huyu aliandika Temptation akizungumzia pia maisha yake yalivyokuwa na jinsi alivyokoswa mkuki na baba yake kwenye shamba la mahindi maana alikuwa kiziwi. Aaah! Yaani jamaa alikuwa anaandika bwana, ukikishika kitabu chake hutakaa ukiweke chini. Yaani nilipokuwa nakisoma kitabu hiki najiona kama niko Shirati/Rorya vile wakati hata sipajui. Pia aliandika kingine kinaitwa "Bed of Roses"

R.I.P Agoro Anduru!!!
 
joram alikuwa juu sana. Namfananisha na chase. Vitabu vyake havina mfano hadi sasa. Ni eddie ganzel (marehem) na yule wa willy gamba ndio waliweza kufananishwa kwa kiasi fulani
 
Ben R. Mtobwa alikuwa ni noma

Sent from my GT-N7100 using Tapatalk 2
 


Mkuu umenikumbusha mbali, siku hizi mambo kama haya huwezi kuyaona kabisa. Kila ukienda sehemu ni shigongo tu.
 
guys! msiseme siku hz hakuna watunzi, have u tried someone called HUSEN TUWA believ me angalau mtafarijika
 
guys! msiseme siku hz hakuna watunzi, have u tried someone called HUSEN TUWA believ me angalau mtafarijika

Bado kuna huyu Kajubi Mukajanga...bado yupo hata SASA na vriwaya sake Mpenzi NAMBA 1&Mpenzi NAMBA 2....siwasahau hadi Leo wahusika wakuu akina Fadhili Magoma na Diana..yaani utunzi ule ilikuwa unateka hisia ZA msomaji hadi basi....
 
Kulikuwa na vitabu kama KAMLETE AKIKATAA MLIPUE,SIJANYONGWA,SANDA YA JAMBAZI, FUNGUO ZA SIRI, AMA ZANGU AMA ZAKE, KIFO MKONONI,. Vitabu hivi ama kwa hakika vilikuwa vitamu,kama vile unaangalia movi kwenye 3D. Watunzi walikuwa makini sana,na kama mtu ulikuwa unajifunza karate,ulikuwa unajikuta kama unapatwa midadi kibaoo.
 
Joram Kiango anamtumia kama 'Stelingi' kwenye simulizi zake..akiziita harakati za joram Kiango labda nikukumbushe kidogo baadhi ya kazi zake,

>Najisikia kuua tena.
>Tutarudi na roho zetu?
nyingine ni(1) salamu kutoka kuzimu na(02) lazma ufe joram. ni vitabu vizuri kweli.
 
Huyu si ndo yule aliyeandika za willy gamba?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Hapana mkuu ,aliyeandika stori za willy gamba ni mzee Musiba mungu amrehemu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…