Mtunzi wa vitabu Joram Kiango

Mtunzi wa vitabu Joram Kiango

Huyu si ndo yule aliyeandika za willy gamba?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Za Willy Gamba zilitungwa na Al Marhum Elvis Musiba na vitabu kama Kikosi cha Kisasi, Njama nk
 
ndiye huyu aliandika kitabu kiitwacho 'simu ya kifo'?

Simu ya Kifo kiliandikwa na Almarhum Hussen Hassan Faraji Katalambula, enzi hizo kulikuwa na Magazeti ya Filamu na aliwahi kuandika hadithi za "Lawalawa" "Viva" nk. Baada ya hapo yakaja Majarida ya SANI ( Marehemu S.M.M Bawji) yenye waigizaji Komredi Kipepe, Ndumilakuwi, Pimbi (Dk Love), Lodilofa, Betina na Zena.
Upande mwingine kulikuwa na MCHESHI la Nico ye Mbajo.
 
Kwa hakika hamu ya kusoma riwaya na tungo za masimulizi yakiswahili imeniisha kabisa toka kuondoka kwa hawa magwiji,inawezekana wapo wanaofuata nyayo zao lakini kwa kweli sijasoma riwaya yoyote ya mtunzi mpya wa riwaya za kiswahili.
ngoja nami nisubiri majina ya watunzi wanaochipukia labda waweza fufua hamu ya kusoma riwaya hizi za kiswahili.

siku hizi hailipi kutunga riwaya.soko halipo,watu hawasomi wako busy facebuk,jamii forums e.t.c.
Utauza wapi?
 
Simu ya Kifo kiliandikwa na Almarhum Hussen Hassan Faraji Katalambula, enzi hizo kulikuwa na Magazeti ya Filamu na aliwahi kuandika hadithi za "Lawalawa" "Viva" nk. Baada ya hapo yakaja Majarida ya SANI ( Marehemu S.M.M Bawji) yenye waigizaji Komredi Kipepe, Ndumilakuwi, Pimbi (Dk Love), Lodilofa, Betina na Zena.
Upande mwingine kulikuwa na MCHESHI la Nico ye Mbajo.

Niko ye mbajo naye alikuja juu sana moja ya riwaya yake iliitwa-SIFI MARA MBILI.
 
Yupo na huyu Hussen Issa Tuwa sijui badao yupo hai.? Kuna hadithi zake nimewai kuzisoma kama mdunguaji,mkimbizi na nyingine nimeisahau.huyu jamaa ni mtunzi wa ukweli.
 
Enzi hizo jarida la SANI linawika nilikuwa nakaa mkoani Kagera, kwa hiyo kila mwezi ilinibidi nilipe nauli kutoka wilayani kwenda Bukoba mjini maana lilipatikana huko tu. Bei ya nauli ilikuwa kubwa kuliko bei ya jarida.
 
Yupo na huyu Hussen Issa Tuwa sijui badao yupo hai.? Kuna hadithi zake nimewai kuzisoma kama mdunguaji,mkimbizi na nyingine nimeisahau.huyu jamaa ni mtunzi wa ukweli.

mimi pia namkubali sana Hussein Tuwa, niliisoma mkimbizi. Vp hiyo ya mdunguaji naweza kuipata vp? Du ila Ben Mtobwa ni baab kubwa, namlinganisha na John Kiriamiti wa Kenya, jamaa ni noma sana tafuta my life in crime
 
Kwa hakika hamu ya kusoma riwaya na tungo za masimulizi yakiswahili imeniisha kabisa toka kuondoka kwa hawa magwiji,inawezekana wapo wanaofuata nyayo zao lakini kwa kweli sijasoma riwaya yoyote ya mtunzi mpya wa riwaya za kiswahili.
ngoja nami nisubiri majina ya watunzi wanaochipukia labda waweza fufua hamu ya kusoma riwaya hizi za kiswahili.

mkuu jaribu erick shogongo:target:
 
mkuu jaribu erick shogongo:target:
Asante mkuu,Nilijaribu nimeshindwa kutokana na maudhui ya riwaya zake nyingi kama utakuwa umesoma moja nyingine ukiaanza tu unajua mwisho itakuwa nini,hazina tofauti na filamu zetu za kitanzania.
ni mtazamo tu kiongozi.
 
Hapana,kiongozi mtunzi wa story za Willy Gamba anaitwa Elvis A.Musiba (RIP)
Ambayae kazi zake ni pamoja na
KIkomo
kikosi cah kisasi
Njama
Hujuma
na vingine
Nilisoma kikomo,kikosi cha kisasi,njama na kile cha kufa na kupona enzi zile nipo primary
 
Enzi hizo jarida la SANI linawika nilikuwa nakaa mkoani Kagera, kwa hiyo kila mwezi ilinibidi nilipe nauli kutoka wilayani kwenda Bukoba mjini maana lilipatikana huko tu. Bei ya nauli ilikuwa kubwa kuliko bei ya jarida.

Sasa Mkuu si ni nafuu ungekuwa unamuagizia dereva ama konda akuletee tu kuliko.
 
Kwanza kabosa naomba mods mbadilishe title ya hii post ili iendane na jina halisi la my Kiswahili hero.
Namfagilia saaaaan Joram Kiango, penye harufu ya hatari yeye ndo anacheka. Kijana aliyekulia nchini Marekani na kupata mafunzo huko, kisha kuanzisha kampuni binafsi ya upelelezi.

Tafadhali nirusuni niwawekee picha, maana mi ni mshabiki mkubwa wa hizi series. Na nilisikitika sana niliposikia jaam Ben R. Mtobwa amefariki, anyway. Things come and go, seasons change and people as well.

IMG_2845.JPG Hiki ni political, na ni kizuri kinoma, enzi hizo za uchaguzi wa vyama vingi unapoingia, this guy amejitahidi kuelezea hivyo vyama na waassi wake, then blending it with fiction. Kuwa Kina Inspekta Kombora na jeshi lake wameshindwa kazi, mpaka alipoingia kijana mtanashanti, Joram

IMG_2846.JPG Arusha ndo imezungumzwa humu, Nharenaro, maasi yanapovuka kiwango na mwasichana flani kuuawa kinyama, muda uleule, sehemu ileile, na polisi aliyeenda kufanya upelelezi anauwawa kwa style ilele. Joram atafanikiwa?

IMG_2847.JPG Hapa Afrika ndo inaangazwa, hujuma zote wanazofanyiwa, dhuluma na kila kitu, ukombozi ndo njia pekee ya kutoka humo. lakini mashujaa kutoka nchi mbalimbali walipopelekwa, hakuna anayerudi hai, Joramanatazamwa na Ulimwengu mzima, ataweza?

IMG_2848.JPG Taarifa za kutoka kwenye kikao nyeti cha watu wazito sana na wenye hadhi mtaani na nyadhifa nzito maofisini, wanakubaliana kutofanya chochote mpaka wamuue kwanza Joram, kisa na mkasa?

IMG_2849.JPG Hapa tuko mwisho wa Reli, Kigomam, Joram alidhani amekwenda mapumzikoni kufaidi samaki wa Ziwa Tanganyika, haikuwa hivyo, abadala yake akajikuta uso kwa uso na mumbe wa mauti.

Nakala zingine kuna watu wamezimisplace, ila hizi copy nikazimisha popote pale ninapohamia. I love them books. Kama kuna mtu ana ambazo sijaweka hapa, tafadhali.

Kwa mara nyingine nasisitiza mods wabadili title ya post, inaniumiza roho kusema ukweli. weka jina sahihi, Joram Kiango, ama ukishindwa sema kabisa Harakati za Joram Kiango.
 
Attachments

  • IMG_2845.JPG
    IMG_2845.JPG
    46.7 KB · Views: 81
mimi pia namkubali sana Hussein Tuwa, niliisoma mkimbizi. Vp hiyo ya mdunguaji naweza kuipata vp? Du ila Ben Mtobwa ni baab kubwa, namlinganisha na John Kiriamiti wa Kenya, jamaa ni noma sana tafuta my life in crime

mkuu hiyo ya mkimbizi na mimi ninayo nakala yake,lakini ya mdunguaji sidhani kama amewai kutoa kitabu chake ila niliisoma kupitia gazeti la kiu mwaka 2003-2004..ila Joram Kiango ni zaidi hasa hadithi za kijasusi namkubali sana.!
 
Kwanza kabosa naomba mods mbadilishe title ya hii post ili iendane na jina halisi la my Kiswahili hero.
Namfagilia saaaaan Joram Kiango, penye harufu ya hatari yeye ndo anacheka. Kijana aliyekulia nchini Marekani na kupata mafunzo huko, kisha kuanzisha kampuni binafsi ya upelelezi.

Tafadhali nirusuni niwawekee picha, maana mi ni mshabiki mkubwa wa hizi series. Na nilisikitika sana niliposikia jaam Ben R. Mtobwa amefariki, anyway. Things come and go, seasons change and people as well.

View attachment 75270 Hiki ni political, na ni kizuri kinoma, enzi hizo za uchaguzi wa vyama vingi unapoingia, this guy amejitahidi kuelezea hivyo vyama na waassi wake, then blending it with fiction. Kuwa Kina Inspekta Kombora na jeshi lake wameshindwa kazi, mpaka alipoingia kijana mtanashanti, Joram

View attachment 75271 Arusha ndo imezungumzwa humu, Nharenaro, maasi yanapovuka kiwango na mwasichana flani kuuawa kinyama, muda uleule, sehemu ileile, na polisi aliyeenda kufanya upelelezi anauwawa kwa style ilele. Joram atafanikiwa?

View attachment 75272 Hapa Afrika ndo inaangazwa, hujuma zote wanazofanyiwa, dhuluma na kila kitu, ukombozi ndo njia pekee ya kutoka humo. lakini mashujaa kutoka nchi mbalimbali walipopelekwa, hakuna anayerudi hai, Joramanatazamwa na Ulimwengu mzima, ataweza?

View attachment 75273 Taarifa za kutoka kwenye kikao nyeti cha watu wazito sana na wenye hadhi mtaani na nyadhifa nzito maofisini, wanakubaliana kutofanya chochote mpaka wamuue kwanza Joram, kisa na mkasa?

View attachment 75274 Hapa tuko mwisho wa Reli, Kigomam, Joram alidhani amekwenda mapumzikoni kufaidi samaki wa Ziwa Tanganyika, haikuwa hivyo, abadala yake akajikuta uso kwa uso na mumbe wa mauti.

Nakala zingine kuna watu wamezimisplace, ila hizi copy nikazimisha popote pale ninapohamia. I love them books. Kama kuna mtu ana ambazo sijaweka hapa, tafadhali.

Kwa mara nyingine nasisitiza mods wabadili title ya post, inaniumiza roho kusema ukweli. weka jina sahihi, Joram Kiango, ama ukishindwa sema kabisa Harakati za Joram Kiango.
mkuu wewe kweli mtu wa Joram, mimi ninazo tatu malaika mweusi,tutarurudi na roho zetu na joramu lazima ufe.ngoja nizitafute nyinginezo maana nikishika kitabu chake huwa siweki chini mpaka kiishe namkubali sana tu.
 
Mkuu, hicho kingine kinaitwa malaika wa shetani. It is true, ukianza kusoma hutotaka kuacha, ndo maana huwa sisomi kwenye daladala, lazima utapitishwa kituo tu, yaani lazima upende usipende
 
Back
Top Bottom