Mtunzi wa vitabu Joram Kiango

Mtunzi wa vitabu Joram Kiango

Kyenju

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2012
Posts
5,143
Reaction score
2,547
Habari wana jf, napenda kujua kama kuna mtu ana habari za mtunzi maarufu wa zamani kidogo wa riwaya aitwaye JORAM KIANGO, na vitabu vyake vinapatikana wapi.
 
vitabu vipo vingi tu mitaani,ila historia yake siijui jamaa namkubali sana kwa ututnzi wa hadithi.!!
 
sio Kihango....ni Kiango.....mtunzi ni Ben Mtobwa(kama sijasahau)....na vitabu vingi vipo bookshops....

Nashukuru kwa kunisahahisha jina maana muda mrefu sana enzi za primary miaka ya 1990.
 
Joram Kiango anamtumia kama 'Stelingi' kwenye simulizi zake..akiziita harakati za joram Kiango labda nikukumbushe kidogo baadhi ya kazi zake,

>Najisikia kuua tena.
>Tutarudi na roho zetu?
 
Joram Kiango anamtumia kama 'Stelingi' kwenye simulizi zake..akiziita harakati za joram Kiango labda nikukumbushe kidogo baadhi ya kazi zake,

>Najisikia kuua tena.
>Tutarudi na roho zetu?
Kazi zake nyingine ni
Dar Es Salaam Usiku
Pesa zako zinanuka
Salaam kutoka kuzimu
Kikwete: Safari ya Ikulu (Biograph & Autobiography)
Mwandishi huyu amefariki kama sikosei mwezi wa kumi na moja 2008
RIP Ben R. Mtobwa.
 
Joram Kiango anamtumia kama 'Stelingi' kwenye simulizi zake..akiziita harakati za joram Kiango labda nikukumbushe kidogo baadhi ya kazi zake,

>Najisikia kuua tena.
>Tutarudi na roho zetu?

Hasa hii ya tutarudi na roho zetu, inanikumbusha mbali enzi za primary school.
 
Kazi zake nyingine ni
Dar Es Salaam Usiku
Pesa zako zinanuka
Salaam kutoka kuzimu
Kikwete: Safari ya Ikulu (Biograph & Autobiography)
Mwandishi huyu amefariki kama sikosei mwezi wa kumi na moja 2008
RIP Ben R. Mtobwa.

Asante kwa kuongezea, jamaa alikua mtunzi mzuri sana,nakiri kwamba nazikubali sana kazi zake!
 
Kazi zake nyingine ni
Dar Es Salaam Usiku
Pesa zako zinanuka
Salaam kutoka kuzimu
Kikwete: Safari ya Ikulu (Biograph & Autobiography)
Mwandishi huyu amefariki kama sikosei mwezi wa kumi na moja 2008
RIP Ben R. Mtobwa.

Huyu si ndo yule aliyeandika za willy gamba?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ebwana kitambo hicho kulikuwa na vitabu vizuri vya hadithi, vilisisimua sana na mwitiko wa kusoma vitabu ulikuwa ni mkubwa mno tofauti na sasa. Vitabu kama Ekaya za Abunwasi, Bulicheka navyo pia vilisisimua.
 
ndiye huyu aliandika kitabu kiitwacho 'simu ya kifo'?
 
Dah..hawa watunzi.
Tumewapoteza.EDI GANZEL,BEN MTOBWA,A MUSIBA,HAMMIE RAJABU.
Walikua watunzi waukweli wa riwaya.
 
Huyu si ndo yule aliyeandika za willy gamba?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Hapana,kiongozi mtunzi wa story za Willy Gamba anaitwa Elvis A.Musiba (RIP)
Ambayae kazi zake ni pamoja na
KIkomo
kikosi cah kisasi
Njama
Hujuma
na vingine
 
Sijui, ngoja wadau watatuambia maana mimi baadaye miaka ya 1994 niliondoka nchini.
Simu ya kifo ni kitabu kilichotungwa na F.H.H Katambula (Faraji Hussein Hasan Katambula) RIP
Daah karibu watunzi wengi mahiri wa zama hizo wameshatoweka ingawa kazi za mikono yao zinaendelea kuwafaidisha wahindi na waswahili wenye bookshops pekee.
 
Dah..hawa watunzi.
Tumewapoteza.EDI GANZEL,BEN MTOBWA,A MUSIBA,HAMMIE RAJABU.
Walikua watunzi waukweli wa riwaya.
Ebanaa dah!....vichwa vya ukweli katika ulimwengu wa riwaya na masimulizi zama hizo ambazo angalau Watanzania walikuwa wanasoma vitabu
 
Simu ya kifo ni kitabu kilichotungwa na F.H.H Katambula (Faraji Hussein Hasan Katambula) RIP
Daah karibu watunzi wengi mahiri wa zama hizo wameshatoweka ingawa kazi za mikono yao zinaendelea kuwafaidisha wahindi na waswahili wenye bookshops pekee.

Da! watunzi wote wa enzi hizo tayari wamekwishatutoka? Ni uzuni sana, kwasasa ni watunzi gani ambao tunaweza tukasema angalau wanafuata nyayo zao.
 
sio Kihango....ni Kiango.....mtunzi ni Ben Mtobwa(kama sijasahau)....na vitabu vingi vipo bookshops....

Absolutely, Ben Mtobwa ni marehemu, vitabu vyake vipo kwa wingi tu bookshops, pale Dar duka la TPH mtaa wa Samora.
Arusha vipo pale Book Point karibu na St Thomas Hospital; tena kipo hata kile anachozungumzia jinsi alivyokuwa mahabusu baada ya kuzingiziwa kesi.
 
Da! watunzi wote wa enzi hizo tayari wamekwishatutoka? Ni uzuni sana, kwasasa ni watunzi gani ambao tunaweza tukasema angalau wanafuata nyayo zao.
Kwa hakika hamu ya kusoma riwaya na tungo za masimulizi yakiswahili imeniisha kabisa toka kuondoka kwa hawa magwiji,inawezekana wapo wanaofuata nyayo zao lakini kwa kweli sijasoma riwaya yoyote ya mtunzi mpya wa riwaya za kiswahili.
ngoja nami nisubiri majina ya watunzi wanaochipukia labda waweza fufua hamu ya kusoma riwaya hizi za kiswahili.
 
Back
Top Bottom