Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 5,527
- 7,121
Jana asubuhi, Alexandra, Mtumishi wa Mungu katika jiji la Kiev, Ukraine, alinusurika kuuawa kwa bomu lililodondoshwa na drone ya Urusi, juu ya nyumba aliyokuwa amelala. Mlipuko wa bomu hilo uliiteketeza nyumba hiyo kwa sekunde chache tu.
Kwa njia inayoonekana wazi kabisa kuwa ni muujiza wa Mungu, Alexandra alirushwa nje ya nyumba hiyo pamoja na godoro alilokuwa amelalia!
Walioshuhudia tukio hilo wanakiri kuwa Alexandra amenusurika kuuawa kwa muujiza wa Mungu. Muujiza huo unathibitisha uwepo wa Mungu na ukweli wa ahadi yake ya kuwalinda na kuwaepusha na mabaya, wote wanaomwamini na kumtumaini. Ahadi hiyo imeandikwa katika:
Zab 121:7-8:
"Mwenyezi Mungu atakukinga na baya lolote; atayalinda salama maisha yako. Mwenyezi Mungu atakulinda katika shughuli zako zote tangu sasa na hata milele."
Na wote tuseme: "Amina"