Ally Kombo
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 11,429
- 2,653
Manabii hawafanani labda ni muhimu kuelewa Nabii ni nani? Lakini huyu wanayemwita Nabii si Nabii bali ni Mtume na neno la Mungu/Yesu Kristo wa Nazareth anasema kuna huduma tano ambazo ni Manabii,Mitume,Wachungaji,Walimu na Wainjilisti na hizi ni huduma ambazo zipo kwaajili ya kuujenga mwili wa Kristo.Bila huduma hizo ndani ya Kanisa,Kanisa halijakamilika si maneno yangu bali ni Neno la Mungu ambalo kila mkristo anapaswa kulijua na kulisimamia Waefeso 4:11-12.
Mimi nimeuliza na wewe unauliza !? Silas A.K
'Hizi ni aya za Mwenyezi Mngu tunakusomea (wewe Muhammad) kwa haki. Na hakika wewe (Muhammad) ni miongoni mwa Mitume.
Qur'an: 2:252.
'Hakika Mwenyezi Mungu alimteua Adam na Nuhu na Ukoo wa Ibrahim, na Ukoo wa Imran (babu yake Yesu) juu ya walimwengu wote.
Qur'an:3:33
'Na bila shaka tulimtuma Nuhu na Ibrahim, na tukaweka dhuriya zao (kizazi chao) Unabii na Kitabu.
'Tena tukafuatisha nyuma yao Mitume wengine, na tukamfuatisha Yesu mwana wa Mariamu, na tukampa Injil. Na tukajalia nyoyo za waliomfuata (Yesu) upole na rehema.
Qur'an: 57:26-27.
'Hakika Sisi tumekuletea wahyi (ufunuo) wewe (Muhammad) kama tulivyowapelekea wahyi Nuhu na Manabii waliokuwa kabla yake. Na tulimpelekea wahyi Ibrahim na Ismail na Is'haq na Yakuub na wajukuu zake, na Yesu na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, na Daudi tukampa Zaburi.
'Na Mitume wengine tuliokwisha kukuhadithia kabla yake, na Mitume wengine hatukukuhadithia. na Mwenyezi Mungu alinena na Musa kwa maneno.
'Mitume hao ni wabashiri na waonyaji, ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletewa Mtume. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu, Mwenye Hekima.
Qur'an: 4:163-165.
Hivyo ndivyo walivyo Manabii katika Uislaam, je [/B Silas A.K ndivyo tafsiri yenu kikristu kuwa Maboya ni sawa na Musa !?
Last edited by a moderator: