Mtume alijuaje Yesu Kristo hakuuwawa msalabani na Warumi?

Mtume alijuaje Yesu Kristo hakuuwawa msalabani na Warumi?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
57,243
Reaction score
90,303
Wayahudi waliomshitaki Yesu kwa Herode na Pontio Pilato, wanafunzi wake walioukuwa wafuasi wake wanaotembea naye kila siku na Warumi waliokuwa wakoloni watawala wa Judea ambao ndio walimuhukumu Yesu wote wanashuhudia kwamba Yesu Kristo alitundikwa na kuuwawa msalabani, wanachotofautiana tu ni kama alifufuka kweli baada ya siku tatu kama alivyohaidi.

Inakujae mtu wa uarabuni ambaye hakuwepo wakati wa tukio lenyewe na hana rejea yoyote ya tukio hilo aje miaka 600 baadaye mbeleni na kusema Yesu Kristo hakuuwawa msalabani bali yalikuwa ni mazingaombwe tu yaliyopelekea mfuasi wake mmoja kuchukua sura yake na kusulubishwa badala yake huku Yesu Kristo mwenyewe akitoroka!
 
Mtume kudai Yesu hakusulubiwa ni sawa na mwanafunzi kuja darasani miaka 600 baadaye na kumpinga mwalimu, wanafunzi, na hata kamera za usalama zilizonasa tukio.

Warumi waliomsulubisha, Wayahudi waliomshitaki, na wanafunzi wake waliomzika , wote walikuwepo. Mtume hakuhudhuria, hakushuhudia, na hana ushahidi , antoa tu dai lisilo na mizizi ya kihistoria wala ushahidi wa kimantiki.
 
Allah subuana wa taalah ndiye aliyempa Mtume mtukufu Muhamad habari za kutokusulubiwa kwa Isa bin Maryam.

Una swali lingine?
Wabilah Tawfiq.
 
Hivi kumbe suala la waislamu kuwachambua wakristo halijaaza leo
 
Jibu liko wazi tu kitendo cha rohomtakatifu kusahau vazi alilo vaa siku hiyo lilikua ni zambarau au nyekundu ni jibu tosha
 
Ndie aliyempa habari pia kuwa mariam mama yake Yesu ni kaka na dada wa Haruni yule wa wakati wa Musa
Allah subuana wa taalah ndiye aliyempa Mtume mtukufu Muhamad habari za kutokusulubiwa kwa Isa bin Maryam.

Una swali lingine?
Wabilah Tawfiq.
 
Wayahudi waliomshitaki Yesu kwa Herode na Pontio Pilato, wanafunzi wake walioukuwa wafuasi wake wanaotembea naye kila siku na Warumi waliokuwa wakoloni watawala wa Judea ambao ndio walimuhukumu Yesu wote wanashuhudia kwamba Yesu Kristo alitundikwa na kuuwawa msalabani, wanachotofautiana tu ni kama alifufuka kweli baada ya siku tatu kama alivyohaidi.

Inakujae mtu wa uarabuni ambaye hakuwepo wakati wa tukio lenyewe na hana rejea yoyote ya tukio hilo aje miaka 600 baadye mbeleni na kusema Yesu Kristo hakuuwawa msalabani bali yalikuwa ni mazingaombwe tu yaliyopelekea mfuasi wake mmoja kuchukua sura yake na kusulubishwa badala yake huku Yesu Kristo mwenyewe akitoroka!
Wahyi.
 
Sawa sawa na habari za mwalimu nyerere

Atokee mtu apinge habari hizo kama zilivyo andikwa na mjomba wake Joseph butiku Kisha azikubari zile ziliondikwa na vitukuu wa Joseph kabila wa Kongo

Itakuwa ni maajabu sana yaan mtu anapinga habari za YESU KRISTO kama zilivyo andikwa na YOHANA nduguye YESU aliyekuwa pamoja na YESU mpaka mauti alafu anaenda kukubali habari za YESU zilizoandikwa na Mohamed

Kazi kweli kweli
 
Mimi nilitegemea baada ya miaka 600 alipokuja nabii mwingine anayewapa siri ya yaliyojiri huko nyuma kuwa Kristo hakuuliwa na yale maaskari dhalimu ya Kirumi na Makuhani manafiki, nilitegemea mgefurahi na kuimba Hosana Hosana kwa kuwa Yesu yule mtu mwema alisurvive uonevu ule, lakini cha ajabu nyie mnaichukia hiyo habari njema kwa sababu mnafurahia,mnapenda na mnatamani Yesu afe msalabani!.
Nyie ni watu wa ajabu sana kushadadia na kutamani Yesu auliwe msalabani
 
Wayahudi waliomshitaki Yesu kwa Herode na Pontio Pilato, wanafunzi wake walioukuwa wafuasi wake wanaotembea naye kila siku na Warumi waliokuwa wakoloni watawala wa Judea ambao ndio walimuhukumu Yesu wote wanashuhudia kwamba Yesu Kristo alitundikwa na kuuwawa msalabani, wanachotofautiana tu ni kama alifufuka kweli baada ya siku tatu kama alivyohaidi.

Inakujae mtu wa uarabuni ambaye hakuwepo wakati wa tukio lenyewe na hana rejea yoyote ya tukio hilo aje miaka 600 baadaye mbeleni na kusema Yesu Kristo hakuuwawa msalabani bali yalikuwa ni mazingaombwe tu yaliyopelekea mfuasi wake mmoja kuchukua sura yake na kusulubishwa badala yake huku Yesu Kristo mwenyewe akitoroka!
Waliomuua si ni mayahudi?
 
Back
Top Bottom