GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,773
- 118,549
Watu sita wanahofiwa kufa maji, huku mwili mmoja ukiopolewa baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kuzama ndani ya Ziwa Victoria.
Watu hao walikuwa wakitoka kwenye harusi Kijiji cha Mwiruruma, kuelekea katika kitongoji cha Bulomba Kijiji cha Igundu wilayani Bunda Mkoa wa Mara.
Mkazi wa Kijiji cha Igundu, Mapambano Kasala ameiambia Mwananchi Dijital kwa simu leo Jumatatu Septemba 16, 2024 kuwa tukio hilo lilitokea jana Septemba 15, 2024, saa moja jioni.
Amesema mtumbwi huo ulikuwa umebeba watu zaidi ya 20 na baada ya kuanza safari ulizama baada ya kuzidiwa uzito.
Chanzo: Mwananchi