Mtulia azidi kuungwa mkono

Mtulia azidi kuungwa mkono

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
*YALIYOSEMWA NA MGOMBEA UBUNGE (CCM) KINONDONI NDG. MTULIA KATA YA TANDALE TAR. 10FEB*

"Mimi ni wa hapa hapa, nimesoma shule hii ya Msingi ya Tandale. Naijua vyema Tandale, nazijua vyema shida zenu." - Mtulia

"Leo nimekuja kuombewa kura na Watu wanaoongoza nchi, nimekuja kuombewa kura na Waziri ambaye namwambia shida zenu moja kwa moja. Huo ni usaliti?" - Mtulia

"Nimetoka kwenye chama cha CUF kisicho na chochote chenye kuleta maendeleo, nimekuja kwenye Chama Cha Mapinduzi chenye Serikali, ilani ya uchaguzi na maendeleo." - Mtulia

"Leo hii nipo kwenye chama ambacho napewa pesa Tsh. Bilioni 25 kwa ujenzi wa barabara; napewa Tsh. Bilioni 3.5 kwa ujenzi wa masoko. Bilioni 1 ya gharama ya uchaguzi kitu gani mbele ya maendeleo hayo?" - Mtulia

"Nayajua matatizo yenu, mfereji wa Mwangosi utajengwa, mna matatizo ya barabara mbovu zote zitaenda kujengwa" - Mtulia

"Najua akina Mama na Vijana hamjapata pesa za asilimia 10 za mikopo toka Manispaa, nipeni kura za ndiyo za kutosha nikasimamie mpewe mikopo hiyo" - Mtulia

"Tsh. Bilioni 25 za ujenzi wa Barabara, Tsh. Bilioni 3.5 za kujenga masoko bora zipo tayari. Nichagueni niwe Mbunge wenu nikasimamie ujenzi huo" - Mtulia

"Nawaombeni mambo mawili. Moja, muende mkaniombee kura kwa wale waliopo majumbani wamchague Mtulia awe Mbunge. Pili, muwahi vituoni mapema mkiwa na kadi zenu za kupigia kura mkanipigie kura za ndiyo niwe Mbunge wenu" - Mtulia

"Mtulia ni mwenzenu, Mtoto wa kitaa mwenzenu, naombeni sana kura zenu za ndiyo tarehe 17 mwezi wa pili. Muwahi vituoni, mkanipigie kura za ndiyo." - Mtulia
IMG-20180210-WA0028.jpg
IMG-20180210-WA0019.jpg
IMG-20180210-WA0026.jpg
 
hafai kuwa kiongozi huyo.kama kanunuliwa na ccm si atauza watu huyo? kinondoni twende na salum mwalimu
 
Hao wote mbona wamevaa kijani c kwamba wameletwa na malori
 
Hao sio watu wa kinondoni,wameletwa too sehemu mbalimbali za Dar,Kuna wengine wametoka Pugu na Majohe
 
Msaliti hafai katika jamii tena anatakiwa kutengwa kabisa na jamii
 
kilichomfanya aache kazi ya kuwatumikia wananchi waliomchagua ni kitu gani? msaliti huyo hatufai hata kidogo anannunulika kwa vipande vya fedha.
 
kwani wakati ule alikuwa hajui shida za apo

mungu fanya miujiza
 
Back
Top Bottom