*YALIYOSEMWA NA MGOMBEA UBUNGE (CCM) KINONDONI NDG. MTULIA KATA YA TANDALE TAR. 10FEB*
"Mimi ni wa hapa hapa, nimesoma shule hii ya Msingi ya Tandale. Naijua vyema Tandale, nazijua vyema shida zenu." - Mtulia
"Leo nimekuja kuombewa kura na Watu wanaoongoza nchi, nimekuja kuombewa kura na Waziri ambaye namwambia shida zenu moja kwa moja. Huo ni usaliti?" - Mtulia
"Nimetoka kwenye chama cha CUF kisicho na chochote chenye kuleta maendeleo, nimekuja kwenye Chama Cha Mapinduzi chenye Serikali, ilani ya uchaguzi na maendeleo." - Mtulia
"Leo hii nipo kwenye chama ambacho napewa pesa Tsh. Bilioni 25 kwa ujenzi wa barabara; napewa Tsh. Bilioni 3.5 kwa ujenzi wa masoko. Bilioni 1 ya gharama ya uchaguzi kitu gani mbele ya maendeleo hayo?" - Mtulia
"Nayajua matatizo yenu, mfereji wa Mwangosi utajengwa, mna matatizo ya barabara mbovu zote zitaenda kujengwa" - Mtulia
"Najua akina Mama na Vijana hamjapata pesa za asilimia 10 za mikopo toka Manispaa, nipeni kura za ndiyo za kutosha nikasimamie mpewe mikopo hiyo" - Mtulia
"Tsh. Bilioni 25 za ujenzi wa Barabara, Tsh. Bilioni 3.5 za kujenga masoko bora zipo tayari. Nichagueni niwe Mbunge wenu nikasimamie ujenzi huo" - Mtulia
"Nawaombeni mambo mawili. Moja, muende mkaniombee kura kwa wale waliopo majumbani wamchague Mtulia awe Mbunge. Pili, muwahi vituoni mapema mkiwa na kadi zenu za kupigia kura mkanipigie kura za ndiyo niwe Mbunge wenu" - Mtulia
"Mtulia ni mwenzenu, Mtoto wa kitaa mwenzenu, naombeni sana kura zenu za ndiyo tarehe 17 mwezi wa pili. Muwahi vituoni, mkanipigie kura za ndiyo." - Mtulia
View attachment 693616View attachment 693617View attachment 693618